Dar: Polisi wakamata watu 32 kwa wizi wa Bil 2.082, ndani ya benki ya NMB

Dar: Polisi wakamata watu 32 kwa wizi wa Bil 2.082, ndani ya benki ya NMB

Ukiishi kama zamani usasa hauwezi kukupata OSAMA BINLADEN,lkn pia kua na elimu ndogo sio sababu maana wasingeweza hata kutokomea na huo mzigo isipokua mipango baada ya kupiga haikua madhubuti
polisi wetu nao hawako modern sana ndio mana jamaa walifanikiwa kufika mbali sema hayo ma shilingi nayo yamewaangusha siku hizi mchakato wa kuyabadili umekua mgumu so ukienda nayo nje ya nchi hamna mtu anayataka ingekua enzi za beura de change wangezibadili ziwe dola then unaingia zako Zambia hapo au Zimbabwe maisha yanaendelea huku ukisubili mtiti upoe
 
Kampuni zote za Ulinzi Zina Bima, Ndiyo maana kampuni ikipigwa Inaenda Bima inalipwa, Na Walinzi wanajua Hilo, Kampuni yetu ilipigwa M.l 800. Lakini ililipwa ndani ya mwezi mmoja na Bima.

Ila hii Bima haiwazuii Polisi kuacha kazi yao kupambana na uhalifu.
 
Kuna usemi unasema "hatua zote tisa"

Umeamua kutenda kitu hiyo ni hatua ya kwanza, kwanini usimalizie tisa?

Ushaamua kuiba kiasi kama hicho, unachotakiwa umalizie hatua za kukata mawasiliano na ndugu, kupotea nchini, kuacha ujinga, kuacha kuwaza nini kitatokea usipowaona ndugu zako...

Sasa umefanya hatua ya kwanza, zinazofuata ni kununua power tiller, sanlg na flat screen ya Sunda? Upo sawa kweli?
Majamaa ni mafala sana
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA WATU 32 KWA TUHUMA ZA MABILIONI YA BENKI YA NMB JIJINI DSM.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu 32 kwa tuhuma za wizi wa fedha kiasi cha Tsh Tsh Bil 2.082.00

Mnamo tarehe 08/06/2020 majira ya saa tisa mchana huko katika Benki ya NMB tawi la Mbezi

Beach wafanyakazi watano wa kampuni ya ulinzi ya SECURITY GROUP OF AFRICA @ SGASecurity Tanzania Limited wakiwa na gari namba T 853 DPX MITSUBISH CANTER walikabidhiwa kiasi cha fedha Tsh Tsh 2 /= kwa maelekezo ya kuzisafirisha kutoka NMB tawi la Mbezi Beach ili wazipeleke tawi la NMB Benki House - CASH CENTRE iliyopo maeneo ya Posta Mpya.

Mara baada ya kukabidhiwa fedha hizo wafanyakazi hao badala ya kuzipeleka walipoelekezwa, walitoweka na fedha hizo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM siku hiyo ya tarehe 08/06/2020 majira ya saa 12 jioni lilibaini kutelekezwa kwa gari hilo maeneo ya Mbagala rangi tatu jirani na Shule ya SAINT MARY.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum kupitia kikosi kazi chake cha kupambana na ujambazi lilianza ufuatiliaji mara moja ikiwa ni pamoja na kufika eneo lilipoonekana gari hilo na kubaini kuwa wafanyakazi hao watano wamekula njama na kuiba kiasi cha fedha Tsh kutoka kwenye sanduku moja la chuma kati ya masanduku manne waliyokabidhiwa.

Aidha, masanduku matatu yaliyokutwa katika gari hilo yalifunguliwa na kukutwa na kiasi cha fedha Tsh 1,302,000,000 /= pia katika gari hilo zilikutwa silaha mbili aina ya Short gun Pump Action yenye risasi 12 na Short gun Protector yenye risasi 05, pamoja na sare za kampuni hiyo.

Watuhumiwa hao walikamatwa Mkoa wa Mbeya na Kigoma wakiwa wamenunua vitu vifuatavyo:-

(i).Trckta Power Tiller aina ya TRA-Change Model 7C/15 lenye thamani ya Tsh 20,000,000/=

(ii),Pikipiki moja aina ya SANLG

(iii).TV flat screen moja aina SUNDA na vitu mbalimbali vya matumizi ya ndani kama kitanda, godoro,jiko la gesi,rnakochi n.k

Mpaka sasa katika shauri hili Jumla ya Tsh 1,497,680,000/= zimeokolewa, mbali na thamani ya vitu vilixyonunuliwa kutoka sehemu ya fedha zilizoibiwa.

Jumla ya "'atillnuniwa 32 wamekamatwa na kuendelea kuhojiwa juu ya ushiriki wao kuhusiana na tukio hili

Aidha Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali ili kuwakamata watuhumiwa wote waliohusika na tukio hili.

ONYO KUHUSU MAANDAMANO YANAYOHAMASISHWA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es salaam linatoa onyo kali kwa kikundi au mtu yeyote atakayeshiriki maandamano hayo batili tarehe 07/07/2020 kwa madai ya kudai Tume huru ya uchaguzi waaache mara moja vinginevyo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

LAZARO B. MAMBOSASA- SACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

06/07/2020
View attachment 1498964View attachment 1498965
View attachment 1498948View attachment 1498950View attachment 1498951
Hii siyo movie kweli ?
 
Simu baba,
Hii midude siyo mizuri inaacha alama (traces) kila mahali.
Ukitupa handset na SIM Card wao wanaangalia ndugu na rafiki zako tu.
Wanasikiliza simu zao na kusoma jumbe zao zote.

Ukifanya tukio hama nchi badili ndugu na marafiki.
Usiwasiliane tena na mtu yeyote uliyewahi kuwasiliana nae na simu yako ya zamani. Usitumie email yako ya zamani n.k.
Usitumie computer yako au modem zako za zamani.

Usiende kijijini kwako au kwa mkeo, badili hadi mwanamke au mume kulingana na jinsia yako.
Duh,,,ni hatari
 
Makampuni ya ulinzi waanze kutumia gari ambazo zitakua na chemba za kuhifadhia hela, ambazo hizo chemba zitakua zinafunguliwa kwa password ambayo itakua siri kati ya pesa inapotoka na inapokwenda bila wasafirishaji kuijua.
 
Makampuni ya ulinzi waanze kutumia gari ambazo zitakua na chemba za kuhifadhia hela, ambazo hizo chemba zitakua zinafunguliwa kwa password ambayo itakua siri kati ya pesa inapotoka na inapokwenda bila wasafirishaji kuijua.
Watu wanaenda kukata hiyo chemba kwa moto wa gesi wanavuta mkwanja kama kawaida.
Kumbuka hapo wao ndiyo walinzi hivyo hakuna wa kuwastua au kuwahisi ni wezi ni vile unasikia wanafanikiwa kuchepuka route na kwenda kutelekeza gari mbali na sehemu waliyotakiwa kupeleka pesa.
 
Nilipofikia kwenye kununua power tila nikakumbuka kuna mafala Fulani zamani waliteka ndege na bastola toy na embe ndio Bomu 🙄🙄🙄
Watu wanadhani mgao wao ulikuwa mkubwa, hapo kuna mlolongo mrefu wa wahusika wa mchezo sasa ukija kuigawa hiyo milioni 700Tsh unapata pesa ndogo tu. Kumbuka wahusika ni watu 32. Najua wengine wanahusishwa kwa uzembe tu.

Walitakiwa wapige yote bilioni 2 wasepe mazima.
 
Back
Top Bottom