DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

Aisee hiyo kitu ipo kabisa na Mola huwa anasikia!
Nimeshuhudia watu wakianguka
Mtu mwenye ukaribu na Mwenye Enzi Mungu sio wa kuchezea
Soma kitabu cha Samueli
kitabu cha samweli aya gani inaruhusu albadir?

mambo ya laana ni chanzo cha dhambi kama Mungu hakupenda iyo laana itamrudia mwenyewe mark my word
 
sifikirii na sidhani kama mange atadhurika

jambo la aibu sana kiongozi wa dini kumtamkia mfuasi ukomo kisa mna personal interest alitakiwa amsahihishe tu na kumsaidia kimawazo lakini suala la ukomo wa mtu hilo ni jambo la Mungu tena
Wacha uzamani kijana kuwa na fikra huru.shekhe yuko sahihi sana tena sana maana huyu mama alizidi aise kutuchafulia hali ya hewa mtandaoni.
 
Hii misemo mingine sio ya kupuuzia kwa kweli!
Si unakumbuka kesi ya kina Nyaga Mawala na wanawake wa kimasai?
Ehh Maulana Mola wangu tunusuru walahi!
Hatari Sana mkuu,Mungu atuepushe kwakweli
 


Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.

=====

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhadi ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM ni ya uongo.

Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.

Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.

Sheikh Alhadi amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).

Alhadi amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenye maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.

9fa01087c47ad41440355f2544575127.jpg

Hawa ma shekhe ukisikia mambo walio yafanya lazima umhurumie huyo Mange lakini Tusubiri Muda Tu
 
ILA huyu mkuu wa dini ni CCM haswa. Tunamfahamu sana hata baadhi ya Waislamu huwa hawamkubali kabisa kwa kuegemea kwenye siasa za CCM.
Angejikita kuiombea dua ccm ishinde kinondoni ingekuwa La maana zaidi kuliko kumjibu mdada wa Insta.
 
Sisi wenye imani yetu tuacheni na imani yetu... huku pwani mtu akikupiga ugeuki nyuma... albadil ina kanuni zake katika kumsomea mtu... ndio maana watu wengi walikuwa na imani potofu kuwa waislamu wana majini, waislamu wachawi nk... ni kwa vile Qur'an ina mambo mengi... una weza jikinga na waovu una weza itumia kum'adhibu mtu vile vile...

ukichukulia hii dini ina toa mianya ya kuadhibu pale unapo enda kinyume... na ndipo hapa mahakama ya kadhi ilikuwa ina pigiwa kelele... ndipo hapa chuo kikuu cha kiislamu morogoro kime chukua hatua zidi ya uovu wa wanafunzi ktk kulinda maadhili ya chuo na dini kwa ujumla....

ukitka kuisoma pia una takiwa kutoa taadhari kwa muusika kuwa ahache kile ambacho unaisi wewe amekitenda kibaya na una kusudio la kutoa adhabu pale atakapo endele kukaidi... na notisi huwa ya siku saba... ukiona kimya basi una endelea na kusudio lako la kumsomea kisomo...

kisomo chenyewe ukisomewa ni hatari mno... una weza kuwa chizi wa maisha nk...!

tahadhari:
tuwe tuna heshimiana, tusiwe wa kukorofishana na kujiona mungu mtu... hekima ni kitu kizuri... hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha...

ngoja sheikh kipoozeo aje...
 
Wacha uzamani kijana kuwa na fikra huru.shekhe yuko sahihi sana tena sana maana huyu mama alizidi aise kutuchafulia hali ya hewa mtandaoni.
mjomba ukibishana na mpumbavu na wewe utakuwa hivyo hivyo sheikh angetumia busara zake kama kiongozi wa dini kuonyesha mfano kama kiongozi wa dini kwa wafuasi wake
lakini sio kwa kupovuka na vitisho
umetokea sura gani maalim?
 
Alipashwa amuombee kwa mwenyezi Mungu amrejeshe kwenye mstari na sio kumlaani,
Mtume alipigwa mawe na akawaombea waliompiga Mungu awasamehe, Yesu pia aliwaombea wakosaji wasamehewe

Mtume alipigwa mawe lakini aliwaombea kwa Mungu wamsamehe huyu kasemwa Instragram na kamtu kadogo tu ka Mange katishia kuua. Kusoma na kuyafahamu maandiko ni jambo moja kuyatekeleza na kuyaishi maandiko ni jambo lingine kabisa
 
Duh !
Na pia mlengwa awe na kosa la ukweli na haki
Na zile za kigoma na sumbawanga si dini yao inarihusu ama?
Lakini sidhani km hilo ndo tatizo linalomsukuma yy kufanya hivyo, labda kuna lingine la kitambo hili limetifua tu lile lingine,
Nawaza tu wakuu
 
Na ukisimamia kwenye haki!
vyovyote vile... ndio maana kila mtu ana pata wasaa wa kumuomba yeye, hata kama ni mla rushwa, au nyongaji, muuaji... ndivyo inavyo kuwa... jiulize kwanini mapadre wanao najisi watoto mungu hawa angamizi hapo hapo...

mungu wetu ni mwenye huruma, upendo... nk... mungu alitaka kuwa angamiza wana wa israel lakini baadae musa alimuomba hasifanye hivyo na kupelekea kubadili maamuzi yake... rejea pale wana waisrael wakitoka utumwani misri
 
Kila mchuma janga hula na nduguze,juzi tumemzika jamaa kwa dhulma ya wizi...kaenda kuvamia kwa ndugu zetu wakigoma nao wakajibu mapigo Mara baada ya kutangaza kwa siku tatu mfululizo.RIP frank jembe langu.
Haya mambo yapo mkuu. Nashangaa kuna mijitu inabeza humu. Ukizunguka katika mikoa ya nchi hii ndio utakapokuwa na nidhamu/heshima kwa vitu na mali za watu.
 
Mtumishi Wa mungu anamtisha mtu badala kumwombea abadilike jamani au ni Mtumishi Wa ccm

Sasa kama Sheikh anao uhakika kuwa mungu wake atamsikiliza katika sala zake za "kumunyamazisha" Mange atuambie lini hasa Mange "atanyamazishwa". Kwa nini aseme tu eti mwaka huu hautaisha? Kwani mpaka anaenda mbele ya media hajaongea na hiyo "mahakama ya haki?" Kama hajaongea nayo amepata wapi uhakika kwamba atasikilizwa? Watu waache myths za kizamani ka za wahenga wetu kuwa mwanamke akila mayai atajifungua mtoto akiwa hana nywele au kwamba mzazi mmojawapo katika ndoa akichepuka huku wazazi wakiwa na mtoto Mdogo basi huyo mtoto atabemendwa.
 
Back
Top Bottom