Kaka labda nikupe elimu ambayo huijui tafadhal kuwa makini nisikilize.
BAKWATA sio chombo cha waislamu na haitawahi kuwa kwa sababu hakikuundwa na waislamu. Mfano mzur nikuulize tu, hivi inawezekana vipi wakristu muundiwe baraza na serikali tena inayojinasibu kwamba haina dini?
Hii kitu ina historia ndefu kidogo nyuma ktk vuguvugu la uhuru, ikumbukwe wakat wa kupigania uhuru baadhi ya wazee wengi wa DSM walihusika na ukomboz wa nchi yetu then kilichokuja kutokea ni kugeukana miongoni mwao baadae. Yaan hawakushirikishwa ktk matunda ya uhuru, ikumbukwe DSM ilikua na wazee wengi ambao ni waislam wakaanza kuonesha hasira zao kwa serikal ya Nyerere wakiona km amewageuka hawakumbuk tena ktk uongoz wake. Nyerere alichokifanya ni kitu simple tu "divide and rule" akawaundia BAKWATA akiwataka waislam ku-obey hcho chombo na serikali itacomply tu kile kiongeacho na BAKWATA. Hapo ndio utata ulipoanza, wengine wakakubal wngne wakakataa.
Hicho chombo kina mkono mkubwa wa serikal, km mfuatiliaji wa siasa za nchi hii utakubaliana na mm kwamba kiko pale kwa manufaa ya wachache na ndio maana muislam unayejielewa huwez kukubal kutawaliwa na BAKWATA. Wao kaz yao ni kutafuta aya na hadith znazowapa favour kwao ila co umma wa kiislamu.
Hivi BAKWATA ingekua chombo cha kiislam kingeshindwa walau kuhoji uhalali wa masheikh wa uamsho kuwa rumande hadi leo tena kwa kesi nyepesi namna ile?
Kwahyo ndugu yangu kuhusisha uislam na BAKWATA ni kutukosea bora tu utuache uizungumzie km tawi la CCM na shirika la serikali.