Dar: Soko la Mabegi Karume laungua moto alfajiri ya Aprili 8, 2022

Dar: Soko la Mabegi Karume laungua moto alfajiri ya Aprili 8, 2022

Hili jambo lichunguzwe kwa umakini kuna nini juu ya hili swala la kuungua masoko,maana imekuwa ni mfululizo sana ...
 
Na wakijenga watachomewa tena, hapo ni kuhama tu hakuna namna.
 
Haya masoko kuungua moto kila wakati maana yake nini?

Zile tume zinazoundwa kutafuta chanzo cha tatizo inaonesha mara nyingi huja na majibu ya uongo ndio maana masoko bado yanaendelea kuungua kwasababu chanzo cha ukweli huwa hakisemwi.

Huku kulindana kutaendelea kuwasababishia machinga hasara kila siku, haiwezekani kila wakati matukio ya moto yanajirudia licha ya pesa za walipa kodi kupotea kwa kuwalipa hao wajumbe wa tume, huu ni ufisadi.
 
Vijana wanjinyima wanapata rizki bado wanachomewa moto mitaji yao, mnataka wawe majambazi?

Wana familia, wana watoto, wana ndugu na jamaa wanawategemea.

Hii nchi ipo siku vijana uvumilivu utawaisha.
Uvumilivu utaisha, itafika huo WAKATI ... wanasiasa wana-dharau sana VIJANA
 
Jamani huu utani sasa,na inatia aibu kwa kweli
 
Chanzo cha moto huo ni nini mkuu au tunalaumu tu maadam tuna uhuru wa kuandika mawazo yetu?
Si mnachoma Makusudi kwani nani asiyejua mipango yenu ... mnalipwa kwa kodi zetu alafu mnatuchomea biashara zetu , mnataka tukale wapi wakuu
 
Kila mkoa anaokwenda Amos Makalla masoko yanaungua kwanini? Kuna uhusiano gani kati ya Makalla na kuungua kwa haya masoko?
 
Vibanda vya wafanyabiashara wadogo 'Machinga' na mama lishe zaidi ya 30 vimeteketea kwa moto katika Soko la Karume Jijini Dar es Salaam, asubuhi ya leo Aprili 8, 2022...
ni mwaka mmoja tu ila mambo tunayoyaona dah Rest in peace Anko JPM
 
Ni

Ni upande wa pili tofauti na ule ulioungua mwezi wa january ambao ulikuwa ukiuzwa nguo na viatu

Kwahiyo wanachoma taratibu, kwa awamu kutokana na sehemu wanazozihitaji, kwa style ileile, yote yanachomwa usiku...

Baada ya leo, ratiba inasemaje, lipi litafuata, sehemu gani? Muda, of course itakuwa usiku.
 
Serikali ya awamu yamotomoto yaani jana tumehitimisha karume Day leo nae kawahitimisha wamachinga wauza mabegi [emoji38][emoji38][emoji23]
 
Vibanda vya wafanyabiashara wadogo 'Machinga' na mama lishe zaidi ya 30 vimeteketea kwa moto katika Soko la Karume Jijini Dar es Salaam, asubuhi ya leo Aprili 8, 2022.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ACP), Muliro Jumanne Muliro amekiri kutokea kwa moto huo na kusema chanzo cha moto hakijajulikana lakini uchunguzi unaendelea, japo taarifa za awali zilionyesha kuwa moto ulianza kwenye kibanda kimoja na kisha kusambaa.

"Kwa mazingira yalivyo pale, vibanda vingi vimebanana na vipo kila baada ya hatua mbili, hivyo moto unapotokea ni rahisi kusambaa, bahati nzuri ni kuwa umeshadhibitiwa, na watu wa usalama wapo eneo la tukio," amesema Muliro.

Naye, Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, Elisa Mugisha amesema timu yake imeudhibiti moto huo ambao pia umeunguza mabanda ya wafanyabiashara wa mabegi.

=================================

Majira ya muda wa saa 11 alfajiri ya leo, moto umewaka na kuteketeza soko la wamachinga wauza mabegi karume.

Matukio ya picha


Moto bado unaendelea kuwaka huku vikosi vya zimamoto na uokoaji vikiendelea na harakati ya kuuzima

View attachment 2180170
moto moto! Wenzangu mumewahi kuridhishwa na matokeo ya uchunguzi?
 
Back
Top Bottom