Hata wewe unaweza kufanywa teja. Unaenda hotelini unaagiza chakula, unaletewa, mhudumu anakuja na jagi na bakuli anakunawisha mikono, unaanza kula, ukimaliza. Anakuja tena anakunawisha mikono, anakupa na tishu ukaushe mikono, anakuongeza nyingine ukaushe midomo. Tambua, tishu zote unazopewa anakuwa ameshazipakaa madawa ya kulevya.
Unaondoka, kadiri siku zinavyosogea unaanza kuhisi ukila chakula cha hoteli ile, huwa unajisikia vizuri sana, huachi kwenda,
siku moja unaamua kumuuliza mhudumu, chakula chao wanaweka nini, hakwambii, anaishia kutabasamu, anatafuta mbinu za kukuzoea, akishaipata, siku moja anakuletea unga kidogo kwenye pakti, anakwambia nusa, unanusa, unajipata ile raha uliyokuwa unaipata kwa kunusa madawa kwenye tishu bila kujijua inaongezeka maradufu kwakuwa sasa umenusa kitu chenyewe direct, kuanzia hapo, ukifika hotelini, unaagiza chakula na pakti ya madawa, ukirudishiwa chenji, pakti ya madawa inazungushwa kwenye noti za change yako, unasepa, ushakuwa mteja tayari.