Dar watu wana roho mbaya sana, nimeamua nikalale stendi kesho nirudi zangu mkoani

Dar! Bora hata ungemla shemeji yako kimasihara kuliko Jogoo,Hapo ndio umeharibu....Rudi tu bro. Umenikera sana.
 
[emoji38][emoji38][emoji38]! Mkuu nimeuunga unga huo undugu wako kwa wenyeji wako nimeishia kucheka tu!

Ni mjukuu wa shemeji yake na binamu wa mamako wa kambo!

Mlikuwa mnafahamiana kabla?
 
Safari njema mkuu! Mungu akutangulie katika safari yako ili uweze kufika salama [emoji120]
 
Yaani mgeni akija ndio akulishe? Watu wa Dar dhiki sana.
Sijui kwa nini hata kwenye thread za mambo ya utani huwa unakuwa na negative perceptions kama kule kwenye Jukwaa la Siasa na u-CCM wako. Kwa taarifa yako mimi niko Jiji la Mwanza lenye kila aina ya chakula.
Hapo nilikuwa ninamkumbusha tu mleta mada kuwa waliotunga hizo methali, nahau au misemo hawakuwa wajinga. Zamani wakati wewe hujazaliwa au pengine ulikuwa bado mdogo watu waliokuwa wanakuja kutembelea ndugu zao kutoka kijijini walikuwa wanakuja na debe la mahindi, au unga, maharage, mkungu wa ndizi, viazi n.k kutegemea na sehemu anayotoka. Ili mwenyeji asiwe na mzigo wa kulisha wageni. Siyo kwamba mwenyeji anategemea wageni kwa ajili ya maisha yake ya kila siku.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],Kweli wewe una tabia mbaya hata huyo mwenyeji wako ana moyo sana.Hivi unawezaje kuamka asubuhi na kukamata kuku wa mwenyeji wako na kisha kumchinja bila kuruhusiwa na mwenyeji wako??,Halafu inaonekana unakula Sana[emoji23][emoji23],Hivi unga kilo mbili unajua ugari unakuwa mkubwa sana!!!,Kwa ulaji huo ilipaswa ubebe debe la unga na maharage umpelekee mwenyeji wako.Halafu huo undugu ni wa mbali sana.
 
[emoji38][emoji38][emoji38]! Mkuu nimeuunga unga huo undugu wako kwa wenyeji wako nimeishia kucheka tu!

Ni mjukuu wa shemeji yake na binamu wa mamako wa kambo!

Mlikuwa mnafahamiana kabla?
Hatufahamiani mkuu, niliambiwa tu kwamba nikifika Dar nimtafute.
Ila siumeona tulivyo ma udugu wa karibu chief...😊
 
Safari njema mkuu! Mungu akutangulie katika safari yako ili uweze kufika salama [emoji120]
Asante sana mkuu, hapa nipo safarini tayari tunaelekea Pandambili. Nimepanda Frester Bus la kwenda Bukoba. Na muhindi nimenunua wa kuchemsha nakula polepole....
 
Kwani hawakujua kama mimi ni mgeni hadi nijichinjie kuku..??
Alafu ugali walikua wanapika mdogo sana mkuu, na kwao sikanyagi tena hadi wakome....πŸ˜•
 
We jamaa wa wajabu sana mambo ya bush unaleta mjini wap na wap halafu hii gahawa
 
Mnapata faida gani kwa story za kutunga? Hamna mshamba hata atoke kijiji gani afanye hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…