Darasa la saba waliopata maksi 60 nao kubebwa kwenda sekondari - Agizo la Kikwete


Tatizo nini? Ni hiyo technolojia ya kusiriba au hawakuelewa masomo?
 
Tusubiri yatoke ili tuweze kusema ambacho wengine tushakisema kwa muda sasa.
 
Watakuja hapa na kabinti kamoja kwenye top ten ili ndo uwe mjadala , wasichana wanaweza .
 
Hakuna cha ajabu hapo, mawaziri kila siku wanafanya mambo bungen quantitatively hawazingatii ubora, wao na propaganda.

Kwa takwimu za kupika kupanda kwa uchumi 6-7.8% wakati hatuna lolote la maana ku-reflect huko kupanda, ni matokeo ya kudanganya.

Kupika ubora wa huduma za afya quantitative representation, wakati huduma ni mbaya ever to happen all over the country.

Kupika ubora wa elimu quantitative representation, wakati hali ahalisi ni ovyo kabisa, walimu wenyewe wanalala njaa unategemea nini?

CCM na serikali yake wanavuna wanachopanda, ukweli utabakia kuwa ukweli sio kila kitu kinaenda kwa propaganda.
 
Nafikiri bado mamlaka husika haijatoa taarifa kamili kwani hizi ni tetesi tu tusubiri muda ufike ndipo tulonge.
 
Wanasiasa wameua elimu. Sasa wanajipachika shahada za juu wao wenyewe hata bila kisomo.. Dr Kikwete; Dr Magufuli, Dr Nape, Dr Salma.... ORODHA NI NDEFU... ongeza...
 
Sijaielewa njia ya OMR nieleweshen wanafanyaje
 
Hili halina ubishi hasa form2 kwa alama 30 Za ufaulu.shuleni kwetu tunawatoto 397.naamini watafaulu watoto70-80.
 
kumbee!ndio maana lowassa ametaka mfumo wa elimu ufumuliwe.
 
Imebidi zoezi la selection lisimamishwe ili wanaohusika waangalie ni i cha kufanya, sijui ndo kuchakachua?!!! Ukipanda mchicha huwezi kuvuna njegere, ukipanda propaganda utavuna propaganda...
 
Chama cha Mapinduzi ndio mfaidika wa kwanza wa matokeo haya.
 
CHANZO CHA MATOKEO MABAYA:

1: Naibu Waziri >> Mulugo... hana elimu

2: Walimu >> Maslahi na mishahara duni

3: Wanafunzi >> hawana tena concentration,
most wako busy na SIMU, FACEBOOK, SOCCER, TV comedy programmes, na mapenzi ktk umri mdogo.....

All day mwanafunzi anachat na cm, fb, kuangalia soccer,
na TV comedy..... FAILURE IS MUST....!!!!

So UTANDAWAZI FOR A FOOL IS A DISASTER.... 95% ya wanafunzi Tz wako hapa

Na UTANDAWAZI FOR A CLEVER GUY MAKES HIM/
HER GENIUS...... 5% ya wanafunzi Tz wako hapa
 
Tusubiri yatoke ili tuweze kusema ambacho wengine tushakisema kwa muda sasa.

.......

Mkuu hizi tetesi ndio zenye ukweli wa matokeo halisi, hayo unayosubiria unaweza ukakuta tayari yameshachakachuliwa(Standardization)
 
Watakuja hapa na kabinti kamoja kwenye top ten ili ndo uwe mjadala , wasichana wanaweza .

Kama kabinti kenyewe si ka kwangu patachimbikaje.....

Litakalotokea haitakuwa ajabu hata kidogo maana maadalizi yetu siku zote ni ya zima moto. Hiyo technolojia ya OMR watoto hawakuwahi kuona hiyo fomu halisi kwanza inafananaje badala yake walikuwa wakitumia vivuli vya fomu hiyo ambvyo ni black and white zilizotolewa vivuli (photocopy).....

Kwa umri wa watoto wetu siku hizi darasa la saba miaka 11 au 12 siku ya mtihani analetewa fomu ina mirangi, kwake kinakuwa ni kitu kigeni. Hivyo kukosea ujazaji wake ni dhahili. Jambo jingine ni kwamba sijui kwa mfano mtihani wa hisabati msahihishaji atajua vipi kama jibu lililoandikwa katika hiyuo fomu ya OMR mtahiniwa alilifanyia kazi kwa hatua zote hadi kufikia jibu lililojazwa au pengine ni wakati gani msahihishaji atawasiliana na majibu yaliyojazwa katika fomu ya OMR kuhakiki majibu yale kwa kuwa fomu ya OMR inasahihishwa kwa teknolojia ya ku-scan....

Kiukweli nadhani maswali ni mengi kuliko majibu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…