Pangaea
JF-Expert Member
- Jun 14, 2012
- 202
- 41
Taarifa toka chanzo cha uhakika zimebainisha kuwa matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka huu ni mabaya kuliko wakati wowote katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.
Matokeo ya mtihani huo uliofanyika kwa mara ya kwanza kwa njia ya ''KUSIRIBA'' yaani OMR yalitarajiwa kuwa yangetoka toka wiki iliyopita au mapema wiki hii Lakini kwa hali ilivyo imebidi kusubiri kwanza ili mamlaka zione cha kufanya.
Hali kama hii huenda pia ikayakumba matokeo ya kidato cha pili ambayo yanatarajiwa kutoka mapema mwakani ambapo kwa sasa mwanafunzi atakaekosa wastani wa jumla wa alama 30 atalazimika kurudia darasa kabla ya kuondolewa kabisa ikiwa atafeli kwa mara ya pili...........
Ni kweli taarifa za uhakika zilizopo ni kuwa matokeo ta kidato cha pili na yale ya darasa la saba ni mabaya hasa.
Mwaka huu wanafunzi wengi wa std vii wameshindwa kufikia the minimum pass mark ambayo ni 100.
Huu ndio uzuri wa technology hamna kupepesa macho.Huko form two ndio usiseme matatizo ya sekta ya elimu yako wazi.