Darasa la saba waliopata maksi 60 nao kubebwa kwenda sekondari - Agizo la Kikwete


Ni kweli taarifa za uhakika zilizopo ni kuwa matokeo ta kidato cha pili na yale ya darasa la saba ni mabaya hasa.

Mwaka huu wanafunzi wengi wa std vii wameshindwa kufikia the minimum pass mark ambayo ni 100.

Huu ndio uzuri wa technology hamna kupepesa macho.
Huko form two ndio usiseme matatizo ya sekta ya elimu yako wazi.
 
Hili ni pigo kwa Taifa ya serikali tawala ya Jakaya Mrisho Kikwete!

Hili halikubaliki hata kidogo!

Ndiyo faida (MATUNDA) ya serikali legelege ya ccm! Kilichopandwa ndicho kitakachovunwa!
 
Sasa hivi tupo kwenye zoezi la ku-standardize, Nawahakikishia kuwa matokeo yatakuwa mazuri kuliko wakati wowote tangia uhuru.
 

Tatizo letu watanzania tunanzani watoto wa kitanzania ni washamba sana kila kitu hawawezi. Hivi kutumia OMR ni kitu ambacho wanafunzi wanaweza kushindwa? Ninavyoelewa, karatasi za majibu hupelekwa kwa Maafisa Elimu wa Mikoa, kama wana mashaka na teknolojia si wachukue sampuli wasahihishe kwa mkono? Watanzania ni kulalama na kutafuta visingizio, mwaka jana hawakutumia hizo fomu lakini tulishuhudia wimbi la wasiojua kusoma na kuandika wanaenda sekondari.
Tuangalie kwa kina shule zetu, je walimu wanafundisha au kazi kuwatumia wanafunzi kuwafanyia kazi zap hasa huko vijijini?
Wakaguzi mpoooo mnaona watoto wanavyolkmishwa mashamba??????????
 
Mkuu naunga mkono hoja kwa aslimia 100
 
ina takiwa waziri ijiuzuru mara moja,walimu wanauza juisi tu mashuleni na kuchapa pombe, huku wanadai wapewe masilahi makubwa na Kugoma hivi walimu wana mgomea nani serikali ,wanafunzi au wazazi walala hoi madhara ya Mgomo ndiyo hayo ya kufeli kwa watoto .kwa hapo serikali ijiulize,kuwafuta kazi walimu wote na mwalimu atakaye ajiriliwa kwa sasa lazima awe na Digrii moja
 

Wanaweza kila kitu hata kulima na kutumikishwa kwingine wanaweza sasa mbona nawe unalalamika? Kwani kutumikishwa, kulimishwa hasa huko vijijini nayo si sehemu ya elimu, hasa elimu ya kujitegemea.....

Naamini binadamu yeyote mwenye akili timamu ana uwezo wa kufanya chochote hata kile ambacho hajawahi kufikiria kama anaweza kukifanya ilimradi amepatiwa mafunzo sahihi! Nilichosema si kulalamika bali ni kuelezea ukweli halisi na ninaendelea kuamini kwamba kwa aina ya vivuli (photocopy) vya fomu nilivyoviona wanagu mwenyewe wakitumia kama sehemu ya mazoezi, ni wazi kwamba hata baadhi ya walimu wao ambao hawakupata fursa ya kushiriki katika sensa hii na iliyotangulia, watakuwa walizishangaa fomu halisi za OMR zilizotumika katika mitihani ya wanafunzi wao mwaka huu!! Naomba isieleweke vibaya kwamba kushangaa ni sawa na ushamba, lahasha, ni ukweli usiopingika kwamba teknolojia hii hapa kwetu haijazoeleka kiasi cha kuzikuta karatasi za namna hii pahali pengi. Hivyo naendelea kuamini ikiwa baadhi ya watoto wetu waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu hawakupata fursa mapema ya kuziona na pengine kuzifanyia majaribio karatasi halisi za OMR tutarajie kiwango cha kufeli kuongezeka na mojawapo ya sababu ni teknolojia.

Ili kuepusha hili karatasi za rough walizofanyia kazi hasa kwa mitihani kama ya hisabati na mingine yenye asili hiyo, ni lazima zikasahihishwe na hili linaweza kuchukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa katika kutoa matokeo. Watoto wetu wa siku hizi wa darasa la saba wengi ni wadogo kuweza kumudu umakini wa hali ya juu unaotakiwa katika kujaza fomu za kusomwa na mashine sensitive kama za OMR....
 
Tunapiga hatua moja mbele,tunarudi nyuma hatua tatu na kujipongeza! Huu ni msiba!
 
Mkuu hizi tetesi ndio zenye ukweli wa matokeo halisi, hayo unayosubiria unaweza ukakuta tayari yameshachakachuliwa(Standardization)

ku standardize si kuchakachua! A standard paper need to be standardized
 

MKUU hapo kwenye red utalalamika sana wewe pamoja na baadhi ya watanzania wenye mawazo kama yako. Walimu wameshavunjika moyo, hawasomeshi tena kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya unayoitaka wewe na magamba wenzio. Mgomo baridi unaendelea mashuleni kwa saana tu, tena walimu wenye digrii angalau moja ndio wagomaji wazuri hivyo pendekezo lako hapo kwenye bluu pia halina mashiko. Nakushauri utafute njia mbadala zaidi ya hiyo uliyopendekeza, tena kwa watanzania kuendelea kuwadharau na kuwashutumu walimu ni kama kumwagia petrol nyumba inayoungua badala ya kutafuta 'fire extingusher'
 
Wanaowabeza walimu wasubiri hayo matokeo yanayompa Kawambwa kigugumizi cha kuyatangaza ndipo watajua faida za kubeza walimu.
Hata hivyo kupanga ni kuchagua, kama tunaona elimu yetu iwe ya watu wanaomaliza D7 bila kujua KKK basi tuendelee kuwadharau walimu
kwa nguvu zetu zote ili tuendelee kuvuna matunda hayo na mengine mabaya zaidi
 
Mpango walikurupuka bila kujipanga matokeo yake ndio yanaonekana na bado hawa hawaelewi mm nawafananisha na mbuzi wanackia ila hawaelewi ukitaka waelewe MZIGIMZIGI ndio unafaa. Akili ya kawaida ilibidi waanze na majaribio wao nchi nzima wakati mtoto anamaliziza KKK hazijui ataweza siriba? Mgomo wa walimu umeanza mapema bado ya kidato cha nne 2012 ndio tutapata majibu SENSA imeharibika wamejifanya ipo poa
 
Kama kawaida ikiwa imepita miezi michahce tangu kufanyika migomo ya walimu matokeo ya darasa la saba yamekuwa kituko na kusababisha watoto waliopata maksi 60 katika masomo yote nao kupelekwa sekondari. Agizo hili limetolewa na mkuu wa nchi kwa siri kubwa ili kuficha aibu inayotokana na majigambo aliyoyatoa kipindi cha mgomo chanzo cha habari hii kutoka kwenye halmashauri moja nchini kimeeleza. Kwa yeyote anayetaka kuthibitisha habari hii atembelee halmashauri mojawapo kuulizia kuhusu afisa elimu wa shule za msingi aone. Chanzo hicho kimeendelea kunena hata posho kwa ajili ya kuchakachua matokeo hayo zimekwishatumwa kabisa na maafisa elimu hao wameambiwa wasiitoe habari hii nje.

Jamani elimu ya Tanzania ndo hiyo tunaizika hii ni kutokana kutaka idadi kubwa ya wanafunzi na siyo wanafunzi ambao wameiva kwa ajili ya kuendelea na ngazi nyingine ya elimu ya Tanzania ya CCM.
 

Pass mark huwa ni ngapi? maana 60 sio dhaifu kiasi hicho!
 
"If you want to kill a nation,simply kill education" tanzania imekufa kilichobaki ni siasa za maji taka na ufisadi tu
 
Katika Nchi zote Duniani isipo kuwa Tanzania, Siasa hutenganishwa na Elimu,Ila huku siasa imeingizwa kwenye ishu za elimu na matokeo yake ndo haya, wale watoto wao wanao soma kwa Kodi zetu, huko Ughaibuni ndo watakao kuja kutawala hii nchi, na huu ni mkakati wa makusudi kabisa, na wala si ishu ya bahati mbaya
 
ndio maana kuna vijana wanaotoa matamko ya ovyo-ovyo,i think ni product ya pass mark kama hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…