DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Huu mradi ni wa mabillion ya pesa
Phase 1 ya mwendokasi mlioperate kwa hasara mkashindwa kununua magari mapya na huduma ikawa mbovu kupindukia

Suluhisho
1.Badilisheni nauli kituo hadi kituo iwe TZS 1,300 - 1,500
2.Ongezeni operator mwingne kuwe na ushindan
Iongezwe nauli tena? How and why?!
Kwa nini isiwe kupunguza gharama zisizokuwa na ulazima
 
TANGAZO.

Kwa kutambua mchango wa Sekta binafsi katika utoaji wa huduma ya usafiri, pamoja na kero ya msongamano katika eneo letu la MBAGALA, Serikali imezielekeza Daladala zote zilizokuwa zikitoa huduma kituo cha MBAGALA Ragi Tatu, kuhamia rasmi ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mwendokasi tarehe 1 Julai 2026.

Lengo la zoezi hili ni kuziunganisha daladala katika mfumo wa usafiri wa kisasa wenye tija zaidi kwa waendeshaji na Wananchi wanaotumia huduma hii.

Utekelezaji wa ZOEZI hili utaondoa usumbufu wa abiria kutembea umbali mrefu kutafuta usafiri wa kuunganisha waliokuwa wakiupata.

Wakala wa DART unawaomba ushirikiano wenu ili kufanikisha zoezi hili. Usikiapo tangazo hili mjulishe na mwingine.

Imetolewa na Wakala wa
Mabasi Yaendayo Haraka(DART)
​
 
Acheni ubabaifu....Ongezeni Mabasi yawe hata 1000 yanayofanya kazi kila siku ili kuondoa adha ya usafiri katika jiji la Dar es salaam
 
Acheni ubabaifu....Ongezeni Mabasi yawe hata 1000 yanayofanya kazi kila siku ili kuondoa adha ya usafiri katika jiji la Dar es salaam
Ubabaifu uko wapi ndugu? aliyekwambia tuna shida ya Mabasi ni nani? na je huoni namna watoa huduma wetu wote wanavyozidi kuongeza idadi ya Mabasi? na Je? unajua kule Mbagala peke yake kuna idadi gani ya magari? fanya utafiti wako ikiwezekana uende uone idadi kubwa ya mabasi mapya yasiyokuwa na kazi, wanasema ukiwa huna taarifa wala hujafanya utafiti huna mamlaka ya kusema wala kulaumu. Elimu kidogo tu ni kwamba mradi wa DART unatekelezwa katika awamu sita, Kimara kwenda Kivukoni, gerezani na Morocco ni awamu ya kwanza, Mbagala Gerezani na Kivukoni ni awamu ya Pili, Gongolamboto Kwenda mjini ni awamu ya tatu , ile ya kuelekea Tegeta ni awamu ya Nne, nakadhalika na kadhalika, na kila awamu ina idadi yake ya Mabasi kulingana na utafiti wa kina uliofanyika kujua idadi ya Mabasi itakayotosheleza, nakushauri ingia kwenye mitandao yetu ya kijamii Faebook, Instagram,Twitter (X) kwa anuani ya @DARTMwendikasi pamoja na tovuti yetu ya www.dart.go.tz utapata madini zaidi na kuuelewa zaidi huu mradi. Serikali makini huwa haifanyi mambo yake kwa kubahatisha.
 
TANGAZO:

Tunapenda kuwajulisha wadau wote wa usafiri wa umma Jijini Dar es Salaam, watumiaji wa usafiri wa Mwendokasi pamoja na wadau wote wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuwa tutakuwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya 50 ya Biashara (DITF) kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere katika Barabara ya Kilwa maarufu Kama Sabasaba, kuanzia tarehe 28 Juni hadi yatakapofungwa rasmi.

Tunapatikana katika Banda la Kilimanjaro Mkabala na banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania, tukiwa na watoa huduma wetu Kampuni za Mofat na UDART, njoo tuzungumze kuhusu maendeleo ya mradi huu wa kimkakati ikiwemo fursa lukuki za biashara na uwekezaji, pia tutapokea maoni na ushauri kuhusu huduma zetu.

Wataalam wetu watakuwepo kutoa Elimu ya namna ya kutumia Programu tumizi ya Mwendokasi App katika kukata tiketi zako za safari sambamba na masuala yote yanayohusu matumizi ya kadi janja. Usipange kukosa “njoo tuzungumze”.

DART usafiri wa umma Nadhifu​
 
Taarifa kwa Umma
 
Attachments

  • TAARIFA-KWA-UMMA-SWAHILI.jpg
    TAARIFA-KWA-UMMA-SWAHILI.jpg
    507.2 KB · Views: 14
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, (X)TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: [email protected].

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Mnasababisha ajali nyingi kwa kuruhusu bodaboda na bajaji kupita upande wa MWENDOKASI.
 
Niwaambie ukweli mchungu au mapambio kuwafurahisha maana hamkawii kudai mnatukanwa!!
 
Mradi wa Mwendokasi Awamu ya Pili wazinduliwa Rasmi. Mh.Rais Asisitiza wananchi kuwa walinzi wa miundombinu.
 
Attachments

  • PHOTO-2026-08-07-16-44-28 (1).jpg
    PHOTO-2026-08-07-16-44-28 (1).jpg
    346.2 KB · Views: 10
  • PHOTO-2026-08-07-16-44-28.jpg
    PHOTO-2026-08-07-16-44-28.jpg
    345.9 KB · Views: 6
  • PHOTO-2026-08-07-16-44-29 (1).jpg
    PHOTO-2026-08-07-16-44-29 (1).jpg
    343 KB · Views: 6
  • PHOTO-2026-08-07-16-44-29.jpg
    PHOTO-2026-08-07-16-44-29.jpg
    339.7 KB · Views: 11
TANGAZO.

Kwa kutambua mchango wa Sekta binafsi katika utoaji wa huduma ya usafiri, pamoja na kero ya msongamano katika eneo letu la MBAGALA, Serikali imezielekeza Daladala zote zilizokuwa zikitoa huduma kituo cha MBAGALA Ragi Tatu, kuhamia rasmi ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mwendokasi tarehe 1 Julai 2026.

Lengo la zoezi hili ni kuziunganisha daladala katika mfumo wa usafiri wa kisasa wenye tija zaidi kwa waendeshaji na Wananchi wanaotumia huduma hii.

Utekelezaji wa ZOEZI hili utaondoa usumbufu wa abiria kutembea umbali mrefu kutafuta usafiri wa kuunganisha waliokuwa wakiupata.

Wakala wa DART unawaomba ushirikiano wenu ili kufanikisha zoezi hili. Usikiapo tangazo hili mjulishe na mwingine.

Imetolewa na Wakala wa
Mabasi Yaendayo Haraka(DART)
​
Tatizo mnafanya mambo kwa kukurupuka na ndio maana mnashindwa. Haiingia akilini watu wa TLB ya njia halafu uwahamishe tu kiboya kama wajinga. Kiko wapi sasa, mbona bado daladala wanapiga kazi!?
 
Asante kwa kuja.
Ni lini hayo mabasi mtayapeleka Mwanza pia ili wananchi wapate huduma ya usafiri..??
Sababu jiji la Mwanza limekua na tayari limechangamka na mkituletea hizo Bus zikaanzia route ya Kisesa, Igoma, Neshno, Buzuruga, Mabatini, Nata, Pepsi, Mkuyuni, Nyegezi, Buhongwa, Nyashishi hadi Usagara and Return.
ASANTE POTI! 😅
 
Mradi wa Mwendokasi Awamu ya Pili wazinduliwa Rasmi. Mh.Rais Asisitiza wananchi kuwa walinzi wa miundombinu.
DART.
Ni sawa mnasimamia mradi wa usafiri wa haraka hapa Daslama lakini shida ni moja hamjanyooka. Kivukoni ikifika Ijumaa, Jumamosi na Jumapili na Holidays zote ni kama na ninyi mko Holiday vile.

Mnasababisha mrundikano wa watu kituoni na hata upandaji gari ni wa virugu kwamaana hakuna anaye fuata mtiririko wa lines. Mimi kama mteja mkereketwa na kwa niaba ya wateja wenzangu tunaomba mlitazame kwa umakini sana hilo.

Muongozaji awepo mpaka muda wa kufunga huduma na sio apotee tu na yeye toka ijumaa mpaka jumatatu. Lakini pia sisi wakazi wa Kibaha mnaturudishia lini usafiri!?
 
Je umepakua Mwendokasi App kwenye simu yako? hakika hutajuta pakua sasa Mwendokasi App ili urahisishe ulipaji wa nauli vituoni kama huna kadi ya Mwendokasi. Mwendokasi App ni njia rahisi na salama. Kwa maelezo zaidi tufuatilie kwenye mitando yetu ya kijamii kwa anuani za DART Mwendokasi, ama piga simu bure 080010147 kwa msaada zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: cZg
4. Habari natamani kujua kadi sasa hivi zinapatikana?
 
Njia ya Mbagala magari yanaishia Boma kwanini yasiendelee had I Morocco maana kawawa road imekamilika?
 
Back
Top Bottom