DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Hivi mnafurahi wananchi tunavyokaa kituo Cha mwendokasi saa Moja Hadi saa mbili na nusu asubuhi kusubiri basi la mwendokasi. Hii Tanzania ni nchi ya hovyo kabisa . Mradi mdogo hivi unawashinda? Siku tutakamata mfanyakazi wenu mmoja tumpige tumvunje mguu ndipo mtakuwa na akili.
 
Utawaonea mkuu kama maboss wao tu
 
Tupo kila siku mkuu na kwenye nyuzi nyingi huko juu tumeshaelezea ni lini hasa watanzania wataanza kuonja mafanikio ya serikali yao na kusahau machungu, endelea kutufuatilia kwa karibu pia katika mitandao yetu ya kijamii, facebook,instagram, (X) na linkedlin kwa anuani ya @DARTMwendokasi, kwenye Youtube @DARTTV na pia tuna namba ya bure 0800110147 karibu sana.

👀
 
Hii kampuni itakuwa inaongozwa na majitu hopeless kabisa! Hivi inakuja akilini kweli saa 6 mchana magari yanapark kituoni? Na wakati huo abiria wapo wamejazana kituoni! Dereva anakaa kupiga soga!
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Hivi mnafurahi wananchi tunavyokaa kituo Cha mwendokasi saa Moja Hadi saa mbili na nusu asubuhi kusubiri basi la mwendokasi. Hii Tanzania ni nchi ya hovyo kabisa . Mradi mdogo hivi unawashinda? Siku tutakamata mfanyakazi wenu mmoja tumpige tumvunje mguu ndipo mtakuwa na akili.
Mkuu haya majitu hayajitambui! Hizi kazi zinatakiwa ziwe wazi kwa Afrika Mashariki yote ili Wakenya wachukue nafasi zao!
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Leteni magari mapya aisee. mnaleta usumbufu mkubwa sana kwa abiria. Hizi gari zenu za mbezi-feri/gerezani ni mbovu sana aisee. zinaharibika ovyo njiani. zingine ikipiga mvua zinaingiza maji ya mvua ndani na milango ishaanza kugoma kufunga. itoshe kusema hii biashara hamuiwezi.
 
Ukweli tu usemwe, fleet manager wa dart ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu! Mnaona fahari gani kukalisha watu kituoni saa 2? Magari yapo yamepaki tu kisa nini nini?
 
Huo msongamano wa abiria kwenye kituo chenu cha Kimara mida ya asubuhi,inaashiria jinsi gani kazi ya uendeshaji wa huo mfumo wa mabasi ya mwendo Kasi imeishawashinda,achieni ngazi mwachieni muwekezaji.
 
Septemba 1 ndo hii, mrejesho upo vipi
Hatari sana
Screenshot_20250901_131910_Chrome.jpg
 
Hayo mabus yataoza mpaka hivyo vingine vikamilike.
Sijui wanawaza nini pumbavu hawa
Jul 24 niliwapa ushauri huu

hapa safi -- muwe mshajipanga sasa huku nyumbani

maandalizi ya mapema ili yakifika yaanze kazi kwa haraka

Jul 28 wakajibu hivi
kila kitu kiko sawa maandalizi yamekamilika na watu wetu wa operesheni wamejipanga vilivyo kuhakikisha mambo yanakuwa sawa.

MAjibu ni vitendo sio maneno maneno,

Leo imepigwa until further notice
 
DART walisema BRT awamu ya 5 ingeanza kujengwa Disemba 2023. Mpaka leo kimya. Watu wameshindwa kukarabati nyumba zao.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Jul 24 niliwapa ushauri huu

Jul 28 wakajibu hivi

MAjibu ni vitendo sio maneno maneno,

Leo imepigwa until further notice
Sasa leo wanasema hamna kilichokamilika.
Hilo kurugenzi ni wale maprofesa vitambi tu. Kula vitumbua na maharage kuhonga ndo kazi nyepesi kwao.
Angalia huo upuuzi sasa, mabasi yamefika yako garage.
Abiria wapo wanangoja huduma.
 
hawa watu ushauri wanapewa , maoni wanapewa na wao uhalisia wanauona na utaalamu walionao lakini bado wanakua wazito,

admin mwenyewe leo kaingia online lakini anapita kimya kimya
 
na kipindi hiki ambapo wanajiandaa na hii phase 2 ya mbagala, chukueni muda huu kukaa na jeshi la polisi na trafiki kwa ujumla , zile taa za barabarani zianze kuheshimiwa, na pikipiki na magari waanze kuzoea kutotumia njia ya mwendo kasi, hii itasaidia usalama wa vyombo na raia
 
change za mia 200,100 na shs 50 zimeenda wapi ?

mwanzoni vituo vyenu vilijaa coins kibao sasa hivi karibia vituo vyote havina change za coins ,mnashindwa hata na madalala ,konda wa daladala atahakikisha kwa namna yoyote lazima atafute na kutoa change lakini kwenu mwendokasi kwa wasafiri wasio na kadi mna majibu mepesi tu ,change hamna biashara haiendeshwi hivyo, hakikisheni hamkosi change za coins vituoni

pia chaguzi za mabus mliyochagua kuyatumia inaonekana hayaendani na hali ya hewa ya joto maana mengi mnayapaki tukiuliza minong'ong'ono mnapooza injini ,upooza injini abiria wamejaa vituoni huko ni kutojali wateja wanaokaa vituoni masaa mpaka 2 vituoni na inaondoa bashasha ya uharaka ya usafiri na kuleta ucheleweshaji kwa abiria kuwahi majukumu Yao.

Mwisho jifunzeni time management, mmesafiri mmeona hayo mabus yanavyoendeshwa mnakwama wapi?
 
Back
Top Bottom