DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Pakua Mwendokasi App urahisishe ukataji wa tiketi kwenye Mwendokasi.
 
Attachments

  • app 2 (1).jpg
    app 2 (1).jpg
    18 MB · Views: 30
Kwa nini mmeondoa wale Askari Polisi waliokuwa wanasimamia utaratibu pale kituo cha Kivukoni?
 
Askari wapi hao maana kwenye vituo vyetu kuna askari wetu wa kampuni ya CT , ulikuwa unamaanisha utaratibu upi unaosimamiwa na polisi?
 
Kuna askari polisi adi gerezani mida ya rush hour wanakuwaga nafikir ndo aliomaanisha ukiacha hao Ct
Askari wapi hao maana kwenye vituo vyetu kuna askari wetu wa kampuni ya CT , ulikuwa unamaanisha utaratibu upi unaosimamiwa na polisi?
 
Tuliposema mkae mkao wa kula tulimaanisha, sasa tumeshakabidhiwa mzigo na tayari umeshapakiwa kwenye meli uko njiani unakuja mwezi ujao ama kwa hakika mambo yatakuwa mazuri sana, tuendelee kuiamini serikali wakati ikiendelea kutafuta mwarobaini wa upungufu wa Mabasi katika mradi mzima wa mwendokasi, huu ni mwanzo tu, yajayo yanafurahisha.
 
Attachments

  • VIDEO-2025-07-22-17-16-52.mp4
    15.3 MB
Askari wapi hao maana kwenye vituo vyetu kuna askari wetu wa kampuni ya CT , ulikuwa unamaanisha utaratibu upi unaosimamiwa na polisi?
Kama wiki tatu zilizopita nakumbuka kulikuwa na Askari Polisi sio CTpale Kivukoni, na walikuwa wanasimamia abiria wa Kimara kupanga foleni kupanda mabasi. Na ulikuwa ni utaratibu mzuri sana, wa kuwapa nafasi wenye mahitaji maalum kama wagonjwa na wazee.
 
Boresheni spika zenu za matangazo .... Ikibidi fungeni loud spika
 
Je naweza kubadili namba ya simu kwenye kadi yangu? Alienitengenezea kadi alikosea namba ya simu.

Kingine naomba waambieni watoa huduma wenu wa gerezani wa kule ndani ambao wanascan kadi za kwenda mbezi mwisho waache dharau, Haiwezekani wanaacha abiria wanapita bila kiscan kadi huku wao wanapiga soga huku wakisubiri gari ije then wanawatoa abiria nje ya kituo na kuanza kuscan kadi.

Leo nimewasema sana wale watoa huduma wenu, cha ajabu badala waombe radhi kwa usumbufu waliosababisha kwa abiria wakanigomea kuniscania kadi yangu na hivyo kunilazimu nipande gari ya kimara then niunge to mbezi mwisho.
 
Tuliposema mkae mkao wa kula tulimaanisha, sasa tumeshakabidhiwa mzigo na tayari umeshapakiwa kwenye meli uko njiani unakuja mwezi ujao ama kwa hakika mambo yatakuwa mazuri sana, tuendelee kuiamini serikali wakati ikiendelea kutafuta mwarobaini wa upungufu wa Mabasi katika mradi mzima wa mwendokasi, huu ni mwanzo tu, yajayo yanafurahisha.
hapa safi -- muwe mshajipanga sasa huku nyumbani

maandalizi ya mapema ili yakifika yaanze kazi kwa haraka
 
Kwa kuwa hamna mabasi kwa sasa toeni nafasi kwa daladala kufika kwenye maeneo kama mbezi posta na mbezi kkoo.

Hii ya watu kulundikana hadi kuingilia madirishani sio sawa.
Halafu wenyewe akina Kisena na JK wakose mapato au sio!? Hawawezi kubali.
 
walisema mwezi wa nane kuna ndinga zitaingia, kampuni ya mofat wamewapa ruti ya gerezani mbagala.

mwendokasi una hali mbaya sana ni kuskilizia tu kama ni kweli --- hiyo ruti ya mbezi nayo simanzi tu
Yale yale. Watu hawajulikani wametokea wapi wala uzoefu wao biashara ya usafirishaji abiria haujulikani, leo wanapewa Mradi.! Kumbe ni miradi yao wenyewe, ufisadi tu. Yale yale ya kuwapaamina Kisena na wahuni wengine mradi wa Mwendokasi, sasa unajifia.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mabasi yanakuja kama tunavyosisitiza kila wakati, na kama ni mfuatiliaji mzuri wa mitandao tayari kuna mzigo uko tayari uko kwenye hatua za kupakiwa na mengie yanatengenezwa kwa kasi kubwa.Mifumo ya kielektroniki ipo ndio maana tumezima mtambo wa tiketi za karatasi sasaivi tunatumia kadi janja tu na pia tuna app yetu inaitwa Mwendokasi App inapatikana kwenye App store na Android vyote hivyo ni kuepuka kabisa matumizi ya tiketi za karatasi sasahivi dunia imehama malipo mengi sio kwa fedha taslimu ni mifumo ya kielektroniki tu.
Hayo magari yenu ya gas mnayotufungia vioo kwa kutuaminisha kuna AC ndani mtakuja kuua watu bure. Haiingia akilini. Ni sawa na kuwajaza watu ndani ya chumba huku ukiwasha AC. Utakuja waua watu bure.
 
Tuliposema mkae mkao wa kula tulimaanisha, sasa tumeshakabidhiwa mzigo na tayari umeshapakiwa kwenye meli uko njiani unakuja mwezi ujao ama kwa hakika mambo yatakuwa mazuri sana, tuendelee kuiamini serikali wakati ikiendelea kutafuta mwarobaini wa upungufu wa Mabasi katika mradi mzima wa mwendokasi, huu ni mwanzo tu, yajayo yanafurahisha.
Kwa nini vituo vyenye upande mmoja wa kuingilia upande wa pili msiweke mageti ya kuzunguka yanayoruhusu mtu kutoka tu sio kuingia. Unakuta basi linasimama hapo hapo ukishuka inabidi urudi mwisho wa kituo utoke halafu urudi pale pale au mbele ya basi liliposimama.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Yale yale. Watu hawajulikani wametokea wapi wala uzoefu wao biashara ya usafirishaji abiria haujulikani, leo wanapewa Mradi.! Kumbe ni miradi yao wenyewe, ufisadi tu. Yale yale ya kuwapaamina Kisena na wahuni wengine mradi wa Mwendokasi, sasa unajifia.
hiyo hali imeshazoeleka sasa
 
Je naweza kubadili namba ya simu kwenye kadi yangu? Alienitengenezea kadi alikosea namba ya simu.

Kingine naomba waambieni watoa huduma wenu wa gerezani wa kule ndani ambao wanascan kadi za kwenda mbezi mwisho waache dharau, Haiwezekani wanaacha abiria wanapita bila kiscan kadi huku wao wanapiga soga huku wakisubiri gari ije then wanawatoa abiria nje ya kituo na kuanza kuscan kadi.

Leo nimewasema sana wale watoa huduma wenu, cha ajabu badala waombe radhi kwa usumbufu waliosababisha kwa abiria wakanigomea kuniscania kadi yangu na hivyo kunilazimu nipande gari ya kimara then niunge to mbezi mwisho.
Kubadili namba inawezekana kabisa unatakiwa kufika na kadi yako mahali uliposajilia kadi mwambie muhusika wa usajili tatizo lako yeye atawasiliana na watu wetu wa Tehama watakurekebishia bila shaka. Kuhusu watoa huduma wetu tunaendelea kuwapa elimu kila mara ya namna ya kuhudumia wateja , wakati mwingine ukipata changamoto yoyote piga namba yetu ya bure 0800110147 ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa haraka.
 
hapa safi -- muwe mshajipanga sasa huku nyumbani

maandalizi ya mapema ili yakifika yaanze kazi kwa haraka
kila kitu kiko sawa maandalizi yamekamilika na watu wetu wa operesheni wamejipanga vilivyo kuhakikisha mambo yanakuwa sawa.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mnauliza kero wakati watu wanapitia madirishani na tai zao ili kuwahi kazini.

Serikali irudishe Costa za kwenda mjini hasa huku morogoro road.

For sure wanaomhujumu Mheshimiwa ni mwendokasi na Tanesco.
 
Back
Top Bottom