Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 19,009
- 22,509
huduma ukiiongelea kwa ujumla hatuwezi kujua unataka eneo gani hasa liboreshwe, ila kwa ujumla wake kuna changamoto za uchache wa Mabasi ila kama ulivyoona kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii tumekwishasaini mikataba na watoa huduma ambao wataleta Mabasi ya kutosha, kabla ya mwezi wa tisa mambo yatakuwa mazuri sana sio kwa awamu ya kwanza tu bali hata wenzetu wa Mbagala wataanza kufurahia matunda ya uwekezaji huu mkubwa wa serikali yao.....huduma zenu ni kama. Zinafifia Kila uchwao....
Mna mipango gani... Mbeleni?
Mara ya mwisho tulikuwa tunatumia kadi, ule mradi ukafa, sasa hivi mnatulazimisha kuntumia kadi ilhali pesa zetu zilipotea, kwa nini wanaoweza kutumia kadi mpya watumie na wasioweza watumie tiket?huduma ukiiongelea kwa ujumla hatuwezi kujua unataka eneo gani hasa liboreshwe, ila kwa ujumla wake kuna changamoto za uchache wa Mabasi ila kama ulivyoona kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii tumekwishasaini mikataba na watoa huduma ambao wataleta Mabasi ya kutosha, kabla ya mwezi wa tisa mambo yatakuwa mazuri sana sio kwa awamu ya kwanza tu bali hata wenzetu wa Mbagala wataanza kufurahia matunda ya uwekezaji huu mkubwa wa serikali yao.
Hivi Ndugu zetu huwa mna akili timamu kweli?? Ma bus hamna ila mme ng'ang'ana kuuza kadi, hii si ni sawa na kuwauzia watu miujiza ya kwamba yesu atarudi kuwakomboa??!!Tunaendelea kupokea maoni yenu ya namna ya kuboresha mradi huu wa kimkakati, tumekuwa kimya kwa muda sio kwamba hatuoni maoni na ushauri wenu la hasha! tulikuwa tunahakikisha mambo ya msingi yanafanikiwa, kwa sasa tumeshasaini mikataba na watoa huduma watatu kwa ajili ya kuleta Mabasi katika awamu ya pili ya mradi kuanzia Gerezani Kariakaoo hadi Mbagala sio hadithi tena Mabasi yanatengenezwa usiku na mchana huo ughaibuni na habari njema ni kwamba ndani ya kipindi kifupi kijacho mtaanza kuona utekelezaji wake. Kwa awamu ya kwanza pia tumesaini mkataba na kampuni ye Emirates National Group (ENG) ya Abudhabi nao wanapambana usiku na mchana kuhakikisha wanaleta mabasi ya kutosha, hakika yajayo yanafurahisha.
NB: tarehe 30/6/2025 tunasitisha matumizi ya tiketi za karatasi hivyo kwa wale ambao hawajanunua kadi wajitahidi kununua kwa bei elekezi ya Tsh. 1,000/= yaani buku tu, ili kuepuka usumbufu usio wa lazima, kwa upande wa wanafunzi wao wataendelea kutumia tiketi za karatasi hadi pale ambapo tutawaandalia utaratibu wao mahsusi ambao tutawajulisha baaaye. Kwa msaada zaidi na mawasiliano endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii Facebook kwa anuanai ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka, X,Instagram, na Linkedlin kwa anuani ya DART Mwendokasi, kadhalika katika You Tube kwa anuani ya @DARTTV, pia kwa kutumia namba yetu ya Bure 0800110147.
Cha ajabu na zaidi hawataki barabara zitumike na mapolicmm nayo yako kukamata magari yanayopita hapo. Kweli wacha tuone vituko vya nchi hiiHivi Ndugu zetu huwa mna akili timamu kweli?? Ma bus hamna ila mme ng'ang'ana kuuza kadi, hii si ni sawa na kuwauzia watu miujiza ya kwamba yesu atarudi kuwakomboa??!!
Kimara wameumbiwa kuteseka tu
Wamepotea swali lako hapo juu gumuCha ajabu na zaidi hawataki barabara zitumike na mapolicmm nayo yako kukamata magari yanayopita hapo. Kweli wacha tuone vituko vya nchi hii
Show inaelekea kuwashinda au?
Rais yupo ofisini hana hata habari
Walinzi si watumwa kazi hio ni kuacha mara moja ukishakipwa mshahara wako na kwenda kufanya kazi zingineSasa leteni magari mambo yaende vizuri muache ulocal, pia muwalipe walinzi wenu mmewaonea sana kampuni mliongia nayo ubia ya Ct haijawalipa hawa vijana miezi lukuki wanatia huruma sana.
Tayari imewashindaShow inaelekea kuwashinda au?
Lkn za CDM huwa anaswma anaziona.Rais yupo ofisini hana hata habari
Basi wampe mwingine km show imewashinda wanang'ang'ani nini au kwa sababu ipo chini ya Mtoto wa Kigogo fulani?Tayari imewashinda
Dakika sifuri tu.Lkn za CDM huwa anaswma anaziona.
Hizo habari zenu za kupata tabu yeye hazimuhusu, hawezi kusoma anasoma taarifa zinazomuhusu ukiandika kwa kumtaja kuhusu huo mradi na kumkosoa kiasi cha kitishia uhai wako kwa kutekwa na kupotezwa kabisa hapo lazima atasoma tuDakika sifuri tu.
Wewe mtu kachoma gazeti la picha yake ila kamuona n kapotezwa lakini kilio cha wananchi pale kimara hakuna mabasi hajaona miaka nenda rudi burdani tu.