DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Kadi zenu bei ghari sana kwanini tusitumie N card pia
Bei ya kadi inatokana na teknolojia iliyotumika ambayo ni ya mwaka 2023 ambayo itaiwezesha hapo baadaye kuunganishwa na watoa huduma wengine mfano SGR, Airport,Feri n.k, hatuwezi kutumia kadi nyingine kwani mfumo huu unaendana na kadi zake na umefungamanishwa na mifumo ya ukusanyaji nauli sambamba na mifumo ya kungozea magari hivyo hautaweza kuchanganywa na kadi uliyoitaja.
 
Viti vya wazee, wagonjwa na makundi maalumu wanakaa vijana kisha wanajifanya wako bize na simu ili wasiamshwe. Mlivyoanza huduma kulikuwa na watu wanaosimamia sheria katika mwendokasi. Sasa hivi ni bora liende, kwa nini?
 
Mmomonyoko wa maadili uko kwa kiwango kikubwa sana sio kwenye Mwendokasi pekee hata kwenye aina nyingine za usafiri nishida sana kwa vijana kuwaheshimu wakubwa na hata wenye mahitaji maalum, wasimamizi wapo ila tatizo kizazi ambacho tuko nacho kwa sasa, hili linahitaji mjadala mkubwa wa kitaifa, wewe ukiwa kama mmoja ya watu wenye kuchukizwa na suala hili tushirikiane kuwaelimisha ili turejee kwenye misingi ya kuheshimu utu kama ilivyokuwa zamani.
 
Mnaleta usumbufu mkubwa kufumua barabara zote mpaka service road hii njia ya tegeta. Hivi mnawezaje kufukua lami yote na kujenga vinjia vyembaba kama keko lori likiharibika basi hakuna kupita siku hiyo
 
Vipi zile KADI zenu mmepunguza bei!? Naelewa Wakati ule ilikuwa 5000 bila salio, ila hivi Sasa naambiwa ni 5000 huku salio likiwa 3000, ni kweli!?
 
Kile kipande Cha kigogo Sambusa Hadi pale round about Mbuyuni kitajengwa lini maana miaka inakatika hakuna kinachoendelea
Mpaka Leo Pako vile vile akuna matengenezo pale so sad 😢
 
Hongereni.kwa kurejesha mfumowa k kuingia kwa kadi naQR. Je wale tuliokuwa na kadi za zamani na zina hela, mna mpango gani wa kuturejeshea?
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, (X)TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Mabasi mengi siyo machakavu sana, mnaweza kuingia mkataba na Dar Coach Builders wakafanya refurbishment kwenye body ambazo haziko vizuri naimani mengi yatarudi kama mapya maana Dar Coach Iko vizuri sana kwenye hilo ama New Force Enterprises wako vizuri kwenye body repairs.
 
Vipi zile KADI zenu mmepunguza bei!? Naelewa Wakati ule ilikuwa 5000 bila salio, ila hivi Sasa naambiwa ni 5000 huku salio likiwa 3000, ni kweli!?
Ni kweli sasahivi tuko kwenye promotion ya mwisho wa mwaka bei ya kadi ni ile ile Tsh 5,000/= lakini unapewa na ofa ya safari 4 bure yaani ni kama umeinunua kwa Tsh 2,000/= na Tsh 3,000/= ni nauli yako, safari moja ya njia kuu ni Tsh 750 hivyo safari nne inakua Tsh 3,000/=. Tunawakaribisha sana kuchangamkia ofa hii ya kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kwani ni ya muda tu.
 
Mabasi mengi siyo machakavu sana, mnaweza kuingia mkataba na Dar Coach Builders wakafanya refurbishment kwenye body ambazo haziko vizuri naimani mengi yatarudi kama mapya maana Dar Coach Iko vizuri sana kwenye hilo ama New Force Enterprises wako vizuri kwenye body repairs.
Tunashukuru kwa ushauri mzuri tutauzingatia, hata hivyo tuko kwenye hatua za mwisho za kumpata mtoa huduma ambaye ataongeza idadi ya Mabasi mapya 170 kwa ajili ya kuimarisha huduma katika wamu ya kwanza ya mradi.
 
1734562417098.jpeg
 
Tangu sept 2 mpaka leo Dec 22 zimepita zaidi ya siku 90.Je, taratibu za manunuzi ikiwa na maana ya mkataba wa mtoa huduma mpya, zimekamilika??.Je mtoa huduma mkataba wake unaanza lini utekelezaji ikiwa ni pamoja na kuona ameanza kuingiza mabasi mapya kwenye mfumo??..tunataka kuona matokeo
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, (X)TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
WAKATISHA TICKET wenu hawarudishi chenji kwa visingizio kwamba hawana chenji 200,50,Abiria wengi wanaziacha
 
Tangu sept 2 mpaka leo Dec 22 zimepita zaidi ya siku 90.Je, taratibu za manunuzi ikiwa na maana ya mkataba wa mtoa huduma mpya, zimekamilika??.Je mtoa huduma mkataba wake unaanza lini utekelezaji ikiwa ni pamoja na kuona ameanza kuingiza mabasi mapya kwenye mfumo??..tunataka kuona matokeo
Haya maswali hayatakiwi Tanzania.
 
Ni kweli sasahivi tuko kwenye promotion ya mwisho wa mwaka bei ya kadi ni ile ile Tsh 5,000/= lakini unapewa na ofa ya safari 4 bure yaani ni kama umeinunua kwa Tsh 2,000/= na Tsh 3,000/= ni nauli yako, safari moja ya njia kuu ni Tsh 750 hivyo safari nne inakua Tsh 3,000/=. Tunawakaribisha sana kuchangamkia ofa hii ya kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kwani ni ya muda tu.
Bei ya kadi bei ya kadi
Nyie mnachojuwa ni kuwakamua tu watu
Service yenu mbovu mnawatesa abiriaaaa ..usafiri wenu ni wa kijehenamuuu
Abiria mnawaona kama manyani
Tu

Ova
 
Wekeni hayo mabasi yenu AIC maana madirisha Huwa madogo na watu wanakuwa wengi sana jambo ambalo ni hatari.
Hafu kingine kwanini mabasi yenu mengine hupita vituoni matupu bila kusimama au kuchukua abiria hamuoni mnafanya biashara kichaa
Ni kweli unakuta wanapita baadhi ya root wakiwa tupu na mara nyingi unakuta kuna abiria, sijui huwa wanakimbizana na nini, ila nina uhakika angekuwa mtu binafsi asingekubali hasara ya namna hiyo kwa sababu hao madereva wana uhakika na mishahara yao halafu shirika lina mafuta ya kuchezea ndo maana wanafanya hivyo na kwa mwenendo huo lazima warekodi hasara.
 
August 2023 Afisa Uhusiano wa DART alisema ujenzi wa BRT awamu ya 5 ungeanza Disemba 2023 na kukamilika 2025 mwishoni. Kazi imefika hatua gani? DART Mwendokasi
 
Back
Top Bottom