Tunaendelea kuwasisitiza abiria wetu kuachana na mazoea ya kutumia tiketi za karatasi kwani zinachafua mazingira na kupoteza muda kwa sasa tumezindua huduma ya Kadi janja ambazo zinapatikana katika vituo vikuu vya Kimara, Morocco,Gerezani, Kivukoni na Ubungo terminal, matumizi ya Kadi yanasaidia pia tatizo la upatikanaji wa chenchi, okoa muda wa kupanga foleni kununua tiketi kuwa mjanja nunua kadi janja kwa Tsh 5,000/= tu ,ujanja ni kuchanja tuache mazoea. Ikumbukwe awali malalamiko ya kurudishwa kwa huduma ya Kadi yalikua makubwa mno sasa zimekuja zitumike, na itafika wakati tiketi za karatasi haziatumika tena hivyo wakati ni sasa hujachelewa.