DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Kwanini wasiweke dustbins?
 
Magari mengi yamepakiwa na unakuta abiria ni wengi kituoni,inaondoa hadhi ya hiyo huduma,mnarundika watu kama daladala alfu mnajiita mwendo kasi ,mashine hazifanyi kaz za nini ?mliowaweka kutoa huduma pia hawana care kwa wateja wao ,igine makanpuni mengine ktk lugha kwa hao watoa huduma wenu dirishan na hao walio kwa mashine
 
NAwwpongeza sana kwa hatua hii

Naomba DART muweke toll free number ya kupokea maoni na malalamiko ya wateja sisi.
 
Hongereni kwa kuja jamii forum. Tutawapa kero zetu zote kwa utekelezaji.

Karibuni sana
 
1. Mnaowaweka kwenye kukatisha tiketi, customer care ni zero. Ni tumiungu watu fulani hivi.
2. Kurudisha chenji kamili nako ni ishu. Wakipewa 10,000/- hamsini hamsini zile wanaachiwa sana. Unless otherwise mtu uje na chenji kamili
 

Me Nina maswali machache Tu

Hivi mnasikia Raha gani, kupaki magari pale feri au kariakoo mpaka folen izunguke mara 50, Yan watu wanafika 200 ndio gari linasogea kupakia?

Mnapata Raha gani mnapotoka Kimara kwenda jangwani depot gari likiwa tupu kabisa na kuna Abiria kwenye stend ambao wengine wanaishia magomeni?

Mnapata faida gani, mnapowajaza watu stend wakati magari mengi yapo Tu yamepaki madereva wanachat?
 
1.Hakuna mfumo mzuri wa mzunguko
wa mabasi.
2.Hakuna modification nzuri ya
mabasi,basi ndani linachakaa bila
ukarabati mzuri
3.Mifumo ya umeme inakufa kwenye
mabasi hakuna repair.
4.Uwekezaji wa tehama kwa mifumo
ya uendeshani uongezwe ili kuleta
urahisi wa abiri kujua mwelekeo wa
basi.Hii ya vibao ni old system.
5. Kuwepo na mabasi ya VIP na nauli
iwetofauti hii itasaidia kupunguza
magari madogo barabarani.Kwa
mfumo huu wa kujaza watu kama
ng'ombe mtu anaona Bora
aendelee kutumia private car.
 
1.Hakuna mfumo mzuri wa mzunguko
wa mabasi.
2.Hakuna modification nzuri ya
mabasi,basi ndani linachakaa bila
ukarabati mzuri
3.Mifumo ya umeme inakufa kwenye
mabasi hakuna repair.
4.Uwekezaji wa tehama kwa mifumo
ya uendeshani uongezwe ili kuleta
urahisi wa abiri kujua mwelekeo wa
basi.Hii ya vibao ni old system.
5. Kuwepo na mabasi ya VIP na nauli
iwetofauti hii itasaidia kupunguza
magari madogo barabarani.Kwa
mfumo huu wa kujaza watu kama
ng'ombe mtu anaona Bora
aendelee kutumia private car.
 
Mimi naona hilo nikutokua makini kwenye kupanga ratiba. ..wanajua kua asubuhi wengi wanatoka kimara/mbezi hivyo magari mengi yanatakiwa kutoka kule. ..
Kimara...manzese ..nisehemu zenye watu wengi. ..
Wapangaji ratiba wanafikiri kila siku kupo vilevile...watoke maofisini wajevituoni wajionee. ..kuna sehemu watu wanakua wengi lkn haikua kwenye ratiba.
 
Kwa upande wangu huwa ninapata tabu kujua basi lipi express na lipi sio express madereva wanaassume wote wapandaji ni wenyeji wa kila siku. Unakuta hicho kibao cha express kimeandikwa kwenye kipande cha box kilichochakaa na wakati mwingine hicho kibao hakionekani. Pia ukiuliza walinzi na madereva wanakushangaa. Pia kwa kuwa ni za kugombania kama hukuona kibao unaingia kwanza ndipo uulize.

Andikeni kwenye vibao vya kudumu na vinavyoonekana tena viwe vya kisasa. Pili, kama kuna sound system muwe mnatangaza.
 
Inabidi wachapwe ao walinzi, ila jwa jiji kama la dar kudhibiti 100prcnt uongo ao walinzi hawaendi kula jkt walikuwa wanagawa kipondo heavy naona wangeweka camera na onyo ili atakaekamatwa ni faini,
 
Magari mengi ya mwendokasi huwa yanapita kwa kasi huku yakiwa matupu sasa si yachukue tu abiria hata yawasogeze? Pia Magari ni machache na customer care ya wakataji tiketi, walinzi na madereva ni zero wanafikiri wananchi ni watu wa kufokewa na kuburuzwa kumbe hawajui hao ndio mabosi zao.
 
Kuwepo na utaratatibu wa abiria kupangana ndni ya gari watu wanajazana mlangoni kiasi kwamba ni hatari, vibao vile vya location viboreshwe kama ni express iwe na alama ya kuonekana hata red n k

Wekeni fence kuzunguka kituo kama ilivyo kituo cha ubungo maji wote wapitie zebra
Magari yanayobeba samaki yawe special aisee magari ya kivukoni asubuh yananuka shombo
Wekeni utaratibu wa kupeana mizigo mfano mtu anampa mzigo kwa anaesafari na asiesafiri,(kama fees iwepo ndogo )
Walinzi wenu walipeni vizuri wanalalamika sana and low motivation,

All in all mradi ni mzuri ukifanyiwa kutatutwa changamoto zilizopo
 
Sidhani kama mnaweza timiza hili.

Watu wengi hawatumii mwendokasi kwasababu ya utaratibu wenu mbovu.

Watu kujazana vituoni, kujazana kwenye mabasi.

Tafrani tupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…