Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawa ni wa Dar tu...Lini mtaanza route za mikoa? Dar Mwanza. Nahisi mkianzisha hizi route nauli itakua chee.
Gwajina naye alishawaacha hewaniWasitufanyie kama TTCL walivyo tuachia vumbi hapa ndani
Kunywaa maji kidogo,Dart mwendokasi ,ni nani amewaroga?
Ni faida Gani mnapata magari yakipita vituoni bila kubeba abiria walio jaa humo vituoni?
Ni hasara Gani mnapata Mkiwasogeza abiria kutoka kimara kwenda vituo vya njiani hata kama shift ya dereva imeisha ,?
Ni faida gani mnapata kuwalipa walinzi waliopo vituo vya mwendokasi ambao hawafanyi usafi vituoni wanakuwa wanachat ?Asili ya askari ni usafi.
Furaha Gani mnapata Abiria Morocco wanakaa na ni wengi na magari yapo ila madereva wanachat bila kujali muda!
Ni Furaha Gani mnapata walemavu,wazee ,wagonjwa nawakina mama wajawazito au wenye watoto wadogo wamesimama kwenye siti zao wakati dereva yupo pamoja na askari lakini hakuna anayesimamia utaratibu
Ni faida Gani mnapata sisi tukilalamika?
Ni faida Gani mnapata kukosa viti vituon wakati bus unasubiria zaidi ya lisaa maana mabus ni express au yamejaa hata pa kisimama Abiria hawezi kupanda wakati vituon Kuna wazee,wajawazito, wagonjwa walemavu na wakina mama wenye watoto wadogo?
Ni faida Gani mnapata vioo vya vituoni mnavifunga wakati Kuna muda mabus yakiongozana Abiria hawezi kuingia kituoni Maana yupo mwisho kabisa?
Kuna siku nilikereka sana ,nilikuwa nimepanda mwendokasi kivukoni ili nishuke magomeni kanisani,gari lilikuwa limejaa kiasi Cha haja.Nilikuwa Mimi,na mke wangu na mtoto wa miaka 4.Magari yakawa yameongozana tukashushwa mwanzo wakituo.Tulijaribu kuingia kituoni tukashindwa maana kioo Cha dirishani kilikuwa kimefungwa.Nikambeba mtoto tukawa tubatembea pembezoni mwa kile kituo ili tulifikie ambalo lipo wazi, kumbuka magari mengine yanakuja kituoni Maana bus letu lilishaondoka,ila Kwa ndani Kuna askari amekaa tu.Kumbuka Mimi ni mnene kiasi na mama yenu ni mnene kiasi na tumebeba mtoto.Usalama wetu ulikuwa wapi wakati dirisha lilikuwa limefungwa?
Ni hasara Gani mapata mkiamua kama mtakuwa mashine ni mbovu mkazitoa maana hazitumiki.
Nawasilisha na nawaomba maoni yangu myajibu.
Ndio nani huyo mkuu..😳Gwajina naye alishawaacha hewani
Kuna watu wanapenda kuacha Gari nyumbani na kupanda mwendo Kasi ila deluxe Coach, hata Kwa nauli elekezi SEMA tzs 2000, ila Sio lazima Kwa watu wote na muwe mnazingatia muda Kwa abiria VIP, hii ni kuchangia mapato!! Huu usawa mnaoutaka haujawahi kuwepo dunianiTunakushukuru kwa kupitia kwenye uzi huu,
1. Suala la uchache wa Mabasi linafanyiwa kazi na katika kipindi kifupi tutakuwa tumelimaliza kabisa tatizo hilo.
2. Kuhusu madereva tunawashughulikia kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zilizopo na ikitokea umepata tatizo lolote usisite kutupigia katika namba yetu ya bure 0800110147 kwa msaada zaidi.
3.Tunaendelea kuboresha huduma zetu kila siku ndiomaana tukaamua kuja humu ili mtusaidie mawazo. Tunashukuru sana kwa mchango wako mdau.
Ni kweli kuwe na vip za mwendo kasi 100%✓Kuna watu wanapenda kuacha Gari nyumbani na kupanda mwendo Kasi ila deluxe Coach, hata Kwa nauli elekezi SEMA tzs 2000, ila Sio lazima Kwa watu wote na muwe mnazingatia muda Kwa abiria VIP, hii ni kuchangia mapato!! Huu usawa mnaoutaka haujawahi kuwepo duniani
Ntakunywa maji wakinijibu.Mkuu unajua paliponikera ni pembezoni mwa kituo nikiwa na familia?Kunywaa maji kidogo,
GwajimaaNdio nani huyo mkuu..[emoji15]
Mi simjui mkuuGwajimaa
Vituo vyote viruhusu abiria kuingia/kutoka pande zote mfano Urafiki. Kama kituo kina abiria wachache, upande wa pili kuwe na milango ya kuzunguka inayoruhusu abiria kutoka tu na sio kuingia. Haileti maana mfano abiria ametoka Kimara anaenda NMB Magomeni, akishuka pale Usalama anarudi nyuma kama anaenda Ubungo ili atoke njee wakati angetokea mbela ya kituo benki ni karibu tu. Na hichi kituo kimetanuka sana.View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.
Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku
Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka
Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania
Barua pepe: info@dart.go.tz.
#usafiri wa umma nadhifu
#mwendokasi app
Mradi wa tegeta lini utaanza!?View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.
Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku
Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka
Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania
Barua pepe: info@dart.go.tz.
#usafiri wa umma nadhifu
#mwendokasi app
Tunakuja kwa majiji makubwa kwa kuanzia , sasa tunaandaa sheria ambayo itatuwezesha kufanya hivyo tuvute subra yajayo yanafurahishaVipi mikoani hamleti miendo ya kasi