Utaratibu wa matumizi ya kadi ilisitishwa kutokana na changamoto mbalimbali za kiufundi, kwa sasa mpango wa kurudisha kadi unakaribia kukamilika na mtajulishwa matumizi yake yataanza lini na namna ya kupata kadi hizo.
1.Kadi yangu inapesa zaidi ya 50k, kutokana na kusitishwa kwa matumizi ya kadi hii pesa inamaana imepotea, ama nafanyaje ili niaipate hii fedha? Na je mlitoa taarifa rasmi kwa umma juu ya kusitishwa kwa matumizi ya kadi na suluhisho la wale ambao walishaweka hela nyingi kwenye hizo kadi?
2. Hivi zile camera matumizi yake ni nini? Wakati mradi unaanza madereva walikuwa wakiangalia kinachoendela ndani ya gari hasa kwenye usalama na kama yupo kibaka kamwibia mtu basi dereva anatoa taarifa!
Lakini kwa sasa matukio ya watu kuibiwa ndani ya mwendokasi ni mengi, na hakuna msaada wowote licha ya kuwepo kwa camera!
3. Wakati mradi unaanza vituo vilikuwa vikitangazwa ama ndani ya gani screen inaonyesha kituo kinachofuata, lakini kwa sasa matangazo ya vituo hayasikiki wala baadhi ya magari hayaonyeshi chochote kwenye screen!
Hii inasababisha watu kuvuka vituo na wengine kupotea na kuwasabishia usumbufu!
Hii hali ni kwa nini haitatuliwi???
4. Ni kwa nini huu mradi hauruhusu watu binafsi kuingiza magari yao sokoni ili kuongeza ushindani?
Inavyoonekana watu ni wengi, magari ni machache! Wapo watu binafsi wanaoweza kuagiza magari ya aina hiyo na kutoa huduma, kwa nini hawapati hiyo nafasi...!?
5. Kuna baadhi ya vitua magari hayasimami na wala abiria hawakai katika vituo hivyo, mfano Jangwani na Kkoo maeneo ya msimbazi kuna vituo viwili kimoja hakitumiki mara kwa mara!
Hivi vituo inamaana haikuonekana ni hasara baada ya kuvitengeneza...? Hivi vituo vya aina hii vipo kwa maslahi gani?
6.Zipo taasisi zilifungua akaunti huku mara ya kwanza zikaja kwa mbwembwe kwamba zitajibu kila hoja lakini mwisho wa siku zikatelekeza akaunti!
Watu wanatoa madukuduku yao kwenye nyuzi zilizoanzishwa na hizo taasisi lakini hamna majibu, ama hoja zinajibiwa baada ya mwezi na sio zote! Je
DART Mwendokasi
si mtafuata nyao kwa kuukimbia huu uzi, maana watu wameshaanza kufunguka yao hapa ila hujibu kila mmoja, unajibu baadhi tena majibu mepesi amabyo kimsingi hata hayaridhishi!