DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Napendekeza hili shirika muwape DP World maana mmeshindwa kulisimamia. Unakaa kituo saa zima kusubir gari tena ni asubuhi watu wanawahi katika shughuli zao. Ukiachana na wahujumu wengine uchumi wa taifa, basi Dart ni shirika jingine linahujumu uchumi wa taifa hili. Kama mmeshindwa, tuwape waarabu pia watuongoze , sisi waafrika hatuwezi kujiongoza.
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
hamfanyi kazi maoni wala malalamiko, endeleeni kufanya mnavyojisikia.
 
Gari zimepunguzwa njia za kimara gerezani na kivukoni Hadi kibaha
Kama mlikua hamjajiandaa na route ya mbagala kwanini mmeanza Kwa kitesa watu wa route zingine nimeamka saa 11 asubuhi hakuna gari zote Zinapita zimejaa tena Kwa kupishana zaidi dakka 50 vituo vimejaa watu Wana Sonya tu

Uongozi wenu na watendaji wote hamjielewi
 
Msome Kweli maoni na myafanyie kazi...Sio baadae mkimbie jumla jumla
 
Mimi naanza na Hili la Barabara zenu kuwa finyu sana mbeleni ina maana mtajitanua kwanini msipange mapema ili baadae mkiongeza ruti msianze kubomoa huku jenga kule bomoa huku jenga huku lipa fidia hapa
 
Pia Kuna hii miundombinu inayojengwa eneo la uwanja WA karume machinga complex, Kuna daraja la juu mmekwepa Kwa kuhatarisha watumiaji WA Magari Wakati WA matumizi, ila Cha kusikitisha zaidi Kuna sehemu mmeshindwa kuweka njia ya waenda Kwa miguu kutokana na uwanja WA karume, mmeshindwa nini kuwasiliana na wahusika WA uwanja na ukuta ukavunjwa na kupata njia iliyo sawa ili kuepusha ajali!? Fikiria kama Mtu ni mlemavu WA baiskeli atapitaje pale!? Ataingia barabara kubwa ndio arudi Kwa waenda Kwa miguu!? Nimeangalia ndani ya uwanja eneo hili Kwa ndani zimejaa taka TU, Wasimamizi na Tanroads watumie Weledi kidogo, fanyeni mazungumzo tunajenga nyumba Moja, ni Bora ikawa salama
Na kwanini walemavu au hata wasio walemavu wapite eneo la mradi? Ni heri hata wazunguke kuliko kupita eneo ambalo hawana uelewa wa usalama wake. Ni hatari.

Ingawa hawa dart ni wabovu lakini wao miundo mbinu ambayo bado inajengwa inawahusu nini?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Hilo la usalama si lazima uwangoje dart wawasilishe malalamiko, hata wewe unaweza kuwasilisha sehemu husika kwa njia ya batua pepe. , ukaambatanisha na picha.
 
Wanajazaje abiria utadhani magunia, hawaoni kuwa abiria ni wengi kuliko mabasi yao, kwahiyo wataendelea kuoperate hivyo, hivyo ndo kawaida ile tuizoee? ? Na why hawafanyi service magari yanajibandukia makorokoro , viti vimechanika. Na why hawarekebishi vituo vyao ambako abaria wao wameyabomia yale machuma wakikimbilia kujazana kwenye mabasi yao, wamesahau ile ni huduma ya jamii, hawana fungu la regular maintenance? Watamaintain vipi huduma in the long run, hawajui usipoziba ufa utajenga ukuta?
 
Tunashukuru kwa mchango wako, kwa sasa tuko katika mchakato wa kukamilisha sheria ya DART ambayo itatupa mamlaka ya kwenda kuanzisha huduma katika miji mingine mikubwa kama , Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma, Tanga n.k. , kwahiyo wana Mwanza msiwe na wasi wasi tutawafikia.
Mi I think mngeboresha huduma Dar kwanza kuhamia mikoani mingine ni ishara kuwa mko comfortable na huduma mnayotoa Dar, nendeni Netherlands mkaone huduma za trum zinavyofanya kazi mje mlinganishe na hizi mnatoa Dar, bado sana. Huko mikoani Bajaj zimecover poa sana movement za mijini hata vipanya vimesanda na kuondoka vyenyewe
 
Ondoeni utaratibu wa pesa, ongea na makampuni ya simu watu wajaze kadi zao prepaid wateja waingie stand kwa kadi, mtaokoa billions, how on this world bado mnaamini mtajiendesha kwa cash? Technology imetapakaa ya digital bado mko na cash kweli, are you for real au mnajiandaa kufa in the near future? Tengenezeni kadi wateja wazinunue kwenye makampuni ya simu kisha toa deadline after this date hakuna cash, game over. Cadi ziwe rechargeable kwa huduma za kifedha za simu au banks, you can have option for single use card kwa occasional passengers mbali ya hapo vituoni. There should be no money exchange among your staff wafanye huduma siyo kupokea cash.
2. Tangazeni watu wawekeze mpate hela ya kununua mabasi mengi , mtaweza kupanua faster huduma zenu. Kwasasa mnabeba watu flani tu wa kipato cha chini, mngeboresha huduma mngecover kila mkazi wa mji, mnajikoseshea mapato, watu wanataka huduma zenye hadhi siyo mnavujiana majasho na baadhi ya wateja wenu wanafanya ujinga kwa wanawqke kisa mbanano, make sure only few people wanasimama the rest wakae, hizo ndo huduma standard siyo kama hizi mnazotoa, ni aibu .
 
Dust bins zipo lakini katika baadhi ya mabasi zimeondolewa ama kwa kuibiwa ama kwa kuharibiwa , tunajitahidi mara kwa mara kuhakikisha zinakuwepo na zinatumika ipasavyo, suala la ulinzi wa mali za umma ni la kila mmoja wetu hivyo tujitahidi kuwa walinzi na wa mali za umma, nimesema hivyo kwasababu kuna watu wanadiriki hata kukata handle za kujishika ndani ya mabasi wakati abiria amesimama. Tuwaombe wananchi kuwa walinzi wa mali za umma na kuimarisha usafi kwa ujumla katika mradi Anajiona mjanja kuleta comment ambayo haina kichwa wqla miguu. Watu wanzungumzia vitu serious wewe umekqzana na mavazi ya wanawqke. Mnakera sana

Wee niache wakati kubambia kutamu. 🤣🤣🤣🤣 Aya bana kama nyie hamtachukua hatua basi nggoja niwaite mataliban waje wawasaidieni kazi
Unajiona mjanja kwa kuleta comment haina kichwa wala miguu. Watu wanzungumzia ishu serious wewe umekazana na mavazi ya wadada. Hasara sana
 
Mi I think mngeboresha huduma Dar kwanza kuhamia mikoani mingine ni ishara kuwa mko comfortable na huduma mnayotoa Dar, nendeni Netherlands mkaone huduma za trum zinavyofanya kazi mje mlinganishe na hizi mnatoa Dar, bado sana. Huko mikoani Bajaj zimecover poa sana movement za mijini hata vipanya vimesanda na kuondoka vyenyewe
Kurudi Kwenye bajaji ni umaskini na kurudi nyuma, hii ni indication ya unemployment, mji huwezi kuwa na madereva boda boda 20,000 na bajaji 10000 na ukaita maendeleo, na pia abiria wao hawana usalama WA Maisha Yao,
 
Huduma mnazotoa haziridhishi, na hii hutokana na usimamizi mbovu, mnakatisha watu tiketi na kuwajaza vituoni kwa zaidi ya saa nzima na wakati mwingine unakuta magari yamepaki pembeni. Pia mabasi yanajaza watu mpaka kero, boresheni huduma iakisi na kuendana na jina halisi ya mabasi yaendayo haraka.
 
Ondoeni utaratibu wa pesa, ongea na makampuni ya simu watu wajaze kadi zao prepaid wateja waingie stand kwa kadi, mtaokoa billions, how on this world bado mnaamini mtajiendesha kwa cash? Technology imetapakaa ya digital bado mko na cash kweli, are you for real au mnajiandaa kufa in the near future? Tengenezeni kadi wateja wazinunue kwenye makampuni ya simu kisha toa deadline after this date hakuna cash, game over. Cadi ziwe rechargeable kwa huduma za kifedha za simu au banks, you can have option for single use card kwa occasional passengers mbali ya hapo vituoni. There should be no money exchange among your staff wafanye huduma siyo kupokea cash.
2. Tangazeni watu wawekeze mpate hela ya kununua mabasi mengi , mtaweza kupanua faster huduma zenu. Kwasasa mnabeba watu flani tu wa kipato cha chini, mngeboresha huduma mngecover kila mkazi wa mji, mnajikoseshea mapato, watu wanataka huduma zenye hadhi siyo mnavujiana majasho na baadhi ya wateja wenu wanafanya ujinga kwa wanawqke kisa mbanano, make sure only few people wanasimama the rest wakae, hizo ndo huduma standard siyo kama hizi mnazotoa, ni aibu .
Tunashukuru kwa ushauri wako, tumeshakamilisha mfumo wa kadi na kadi zimekamilika ,kinachosubiriwa kwa sasa ni kukamilika kwa mageti ya kuingilia vituoni ambayo yako katika hatua za mwisho za kukamilishwa, masuala ya kutumia tiketi za karatasi itakuwa historia, kwa sasa unaweza kukata tiketi yako kidijitali kwa kutumia Mwendokasi App ambayo inapatikana kwenye App srore na Android ipakue kwenye simu yako uanze kuitumia sasa ni rahisi na inaokoa muda. Utaratibu wa card top up ni kwamba utaweza kuongeza pesa kwenye kadi yako kwa kutumia mitandao ya simu, benki, ama kwa mawakala watakaoainishwa, serikali haijalala iko kazini na matokeo ya hiki nilichokieleza mtayaona muda sio mrefu kuanzia sasa.
 
Hii route ya Gerezani to Mbagala, muiache indelee hata baada ya 77, inatuheshimisha
Hii inafikia ukomo tarehe 14 mwezi huu, ilikuwa mahsusi kwa ajili ya maonesho ya sabasaba tu, kumbuka mkandarasi bado hajamaliza kazi hivyo ni lazima tusitishe huduma ili amalizie kazi na sisi tujipange kutangaza zabuni ya kumpata mtoa huduma rasmi katika njia hiyo ambayo ni awamu ya pili.
 
Huduma mnazotoa haziridhishi, na hii hutokana na usimamizi mbovu, mnakatisha watu tiketi na kuwajaza vituoni kwa zaidi ya saa nzima na wakati mwingine unakuta magari yamepaki pembeni. Pia mabasi yanajaza watu mpaka kero, boresheni huduma iakisi na kuendana na jina halisi ya mabasi yaendayo haraka.
Tunakamilisha mfumo wa ITS (inteligent transport system) ambao utasaidia sana katika upangaji wa route na ugawaji wa mabasi kulingana na mahitaji ya kituo husika, kwa sasa mambo mengi yanafanyika manually ndio maana wakati mwingine changamoto zinakuwepo.
 
Ondokeni muwawachie Dubai Public Transport, watuwekee mabasi ya umeme na waendeshe wao hilo shirika.

Nyinyi ni wezi watupu mmejazana hapo.

Tazameni mambo ya kisasa haya:

View attachment 2675495
Mfano uliotoa sio wa BRT, hii ni tram ni usafiri maalum wa mijini unaotumia reli, usafiri wetu ni wa Mabasi yanayopita katika njia maalum (exclussive lanes) ambazo ni maalum kwa ajili ya Mabasi pekee. Tunakamilisha utaratibu wa kumpata mtoa huduma kamili maana huyu anayetoa huduma kwa sasa ni mtoa huduma wa mpito. Iamini Serikali yako mambo yanakwenda kubadilika.
 
Back
Top Bottom