Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,823
- 2,466
Katika salama zake za siku ya Wanawake Dunia Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila kwanza amewapongeza wanawake wote kwa kuzaliwa wanawake.
Pili, David Kafulila amerejelea Utafiti uliofanywa na UNAC ya nchi Marekani uliokuwa na majibu kwamba Wanaume sio watu wanaozijali sana familia ukilinganisha na wanawake Kwa ni 35% tu ya kipato Cha mwanaume ndio kinafika nyumbani wakati ni 90% ya kipato cha mwanamke ndio kinafika nyumbani.
Tatu, Mkurugenzi huyo amezishauri familia ziachane na imani potofu badala yake zipeleke watoto wa kike shuleni kwani wakisoma wanafaida zaidi kwenye familia zao pengine kuliko hata wanaume.
===