David Kafulila: 35% tu ya kipato Cha mwanaume kinafika nyumbani tofauti na 90% ya Mwanamke

David Kafulila: 35% tu ya kipato Cha mwanaume kinafika nyumbani tofauti na 90% ya Mwanamke

Kwa kichwa ya uzi ๐Ÿ‘๐Ÿฝ๐Ÿ‘๐Ÿฝ๐Ÿ‘๐Ÿฝ

Baba huyu kanena... Maana miaka inazidi maliza uume wa wengi na hawakomi..
 
Inaongea nini hii kasongo??! Takwimu za amerika zinahusiana vipi na sisi?? Kulikua na uhitaji gani wa hiyo โ€˜postโ€™?
 
Huyu akafanye upya hiyo tafiti halafu aje hapa tena na facts mpya, tumpe na matokeo ya berlin conference 1984-1985, on to Tanzanian settings. Hela ya mwanamke ni ya kwake, hela ya mwanaume ni ya wote. Akwende zake huko USA
Utafiti unapingwa kwa utafiti kafanye kwanza wewe ili umpinge
 
View attachment 3263356

Katika salama zake za siku ya Wanawake Dunia Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila kwanza amewapongeza wanawake wote kwa kuzaliwa wanawake.

Pili, David Kafulila amerejelea Utafiti uliofanywa na UNAC ya nchi Marekani uliokuwa na majibu kwamba Wanaume sio watu wanaozijali sana familia ukilinganisha na wanawake Kwa ni 35% tu ya kipato Cha mwanaume ndio kinafika nyumbani wakati ni 90% ya kipato cha mwanamke ndio kinafika nyumbani.

Tatu, Mkurugenzi huyo amezishauri familia ziachane na imani potofu badala yake zipeleke watoto wa kike shuleni kwani wakisoma wanafaida zaidi kwenye familia zao pengine kuliko hata wanaume.

===
Wewe sio raia

Ovaa
 
Kafulila apewe tuzo kwa kuwatetea wanawake
 
Sahihi,.Hela ya Mwanamke ni ya Mwanamke na Hela ya mwanaume ni ya mwanamke
Hayo ndo maazimio ya kikao cha beijing? Ushenzi ushenzi huu ndo umefanya ndoa nyingi kuwa kama soko moko, kimsingi mahusiano ya mke na mume miaka hii yamezidi kuwa matatani
 
Hayo ndo maazimio ya kikao cha berlin? Ushenzi ushenzi huu ndo umefanya ndoa nyingi kuwa kama soko moko, kimsingi mahusiano ya mke na mume miaka hii yamezidi kuwa matatani
Haya maazimio ya Berlin yalikuwaje kuhusu Pesa ya Mwanaume?
 
huyu kafulila anaongelea wanawake gani? Hawa hawa ambao birthday yake anataka umnunulie zawadi ya smart phone halafu birthday yako anakuletea zawadi ya boxer 3 na vest
 
Shida ya hawa vilaza wa takwimu ni kushindwa kufanya reality check na hizo data zao.

1. Marekani imetoa fursa za ajira kwa wanawake na wengi wapo kwenye ajira rasmi wanapiga kazi na zinaonekana kwa macho sio huku sifa nyingi work done is equal to zero. Wanawake wanapenda zaidi sifa kuliko uwezo wao na wanachoweza fanya.

2. Nyumba nyingi huko state wanawake wanaishi under welfare programs yaani msaada wa serikali. So huwezi compare na bongo.

3. House hold za marekani nyingi ni single mother households,hakuna baba katika familia watoto wanalelewa under child support program obviously data zitaonyesha kipato cha mwanamke 99% kinatumika kwenye familia.

Kuna watu walitakiwa kubakia kuwa wanaharakati sababu wapo vema kukosoa ila sio viongozi wazuri na hawakupaswa kukaa meza za maamuzi sababu wanauwezo mkubwa wa kureason wakiwa wanakosea ila uwezo mdogo sana wa kureason wakipewa nafasi ya kuongoza.
 
Mke wake mbona alikuwa hapeleki nyumbani?
Huyu jamaa adhibitiwe anadanganya taifa kashaona mama ni kilaza ndio maana anakuja na hojaza ukilaza
 
Hayo ya Ngoswe wawaachie kina Ngoswe (wenye familia zao) wao wajikite zaidi kwenye kazi tunazowapa na kuwalipa (Huo ushauri tunaweza kupata hata pengine) Je Sera zao zinachukua kiasi gani na kumwachia ngapi mbangaizaji ili abakize mfukoni let alone kufikisha nyumbani ?!!!

Na iwapo kina kitu tunabinafsisha hata hicho wanachokichukua wanachukua ili kifanye nini ?

Mkuu Mimi ni mfuasi wako nakukubali sana tu
 
Hapo anapoongelea familia ni ile familia aliyozaliwa mwanamke, yaani kwa lugha nyingine ukioa mwanamke atahakikisha 90% ya kipato chake kinaenda upande aliotokea, halafu mkija kuachana inabidi agawane 50% ya mali za mwanaume
Ndio maana anasisitiza wazazi wawasomeshe watoto wa kike maana badae 90% inarudi kwao tena.
 
Back
Top Bottom