Mada ya kafulila na Lissu ilihusu mambo ya sera, yaani kafulila alikuwa anatoa majibu kuhusu madai ya Lisu kisera. Watu wengine wanakuja hapa na maswali ya nani alitaka kuondoa kuondoa uhai wa Lissu. Ingawa tabia ya kuondoa uhai kweli siyo ya kuchukulia kirahisi, lakini pia inabidi ijadiliwa vizuri kuwa isiwe ndiyo sera tena. Tunajua kuwa kuondoana uhai siyo mambo mazuri natabia hiyo inatakiwa ipigwe vita sana kwani tayari imo ndani jamii yetu pia lakini tukumbushane pia kuwa haina mmiliki kwani inafanyika duniani kote na mara kadhaa wanaoifanya huwa hawana madaraka yoyote; waliomrushia risassa JFK, MLK, RFK na reagan hawakuwa na madaraka yoyote.
generalizatio hii ya kuwa kila aliyeuwawa bila kujulikana ilikuwa ni amri ya rais ni upupu wa juu ambao siyo busara kuuacha upite bila kuchambuliwa. Kwa hiyo nilitegemea kuelewashwa kuwa kuuwawa kwa Wangwe ilikuwa ni amri ya rais pia; na hivyo basi kuuwawa kwa Sokoine, Dr Mvungi, na Profesa Mwaikusa wote zilikuwa i amri za rais.
Kukiwa na baseless generalizations basi tegemea kupata majibu ya beseless generalization pia; kama unataka mada iende vizuri basi maswali ya nani alitaka kumwua nani yaondolewa hapa. Endeleeni na mada kwenye majibu ya kafulila kwa Lissu kuhusu sera kusiwe na diversion yoyote kuhusu jaribio la kuuwawa kwa Lissu kwani hakuna anayejua ni nani alipanga kuondoa uhai wa Lissu. Hizo conspiracy theories, zinazaa theories nyingine nyingi ambazo huenda hutazifurahia.
Kuhusu Wangwe umenambia ninatoa machozi ya mamba wakati hunijui nina uhusiano gani na familia ya Wangwe; ndiyo nikakushauri weka baadhi ya maneno kwenye akiba yako.