Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,823
- 2,466
===
Kwa mtizamo wangu Mtu pekee toka Chama Cha Mapinduzi CCM anayeweza kumnyoosha sawasawa Tundu Lissu kwa hoja mujarabu tena kwa data ni huyu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila,
Kwa utafiti wangu mdogo nilioufanya mitandaoni na mitaani ni wazi Watanzania walio wengi hasa wanaCCM wanatamani sana katika Uchaguzi Mkuu Ujao Kafulila awe ndio kampeni meneja wa Rais Samia ili kama chama tuweze kumnyoosha vizuri huyu Tundu Lissu na CHADEMA yake kwa hoja, Kali Kali na data za Kafulila.
Kila mmoja anafahamu tangu Bungeni Lissu ni mtu mwenye akili na hoja sana mbaya zaidi wakati huu anasaidiana kwa karibu na John Heche Pamoja Godbless Lemma hawa wote ni watu wenye hoja Kali, Kali.
Kwa sababu hiyo, Chama Cha Mapinduzi CCM lazima kijipange kuvurumushiwa hoja kali kali toka kwa hawa vinara wa Upinzani kuanzia sasa ndio maana watu kama akina David Kafulila, Hampfrey Polepole, Dkt Bashiru Ally Kakurwa wanahitajika Sana kwa Sasa.
Sijatumwa na Mtu ni kihere here changu tu katika kutafuta ushindi wa Chama.
Kidumu chama Cha Mapinduzi.