David Kafulila ni hazina kwa Taifa letu, anapaswa kutumiwa vyema kwa maslahi mapana ya nchi

Mnaumia sana CHADEMA .ninyi endeleeni kupambana na hali zenu na akili mgando mlizonazo huko huko.zisizo weza kukipeleka chama popote pale zaidi ya kukitumbukiza shimoni.
Nakusisitiza.Usidhani kila anayekupinga ujinga wako ni mwanachama wa "NLD"!Pambanua mambo wewe mlima njegere.😂😂😂
 
What difference is he going to make in pool full corrupt and filthy individuals...

CCM !? Kuna Nini kipya
Kwa hiyo wewe shida yako ni kutaka kuona na kufahamu nini anavyokwenda kubadilisha? Basi napenda kukwambia ya kuwa Kafulila mmoja tu ni hazina kubwa kwa Taifa na mwenye uwezo wa kuleta mageuzi makubwa sana ya kisera. Angalia rekodi zake kwote alikopita kutumikia Taifa letu kuanzia akiwa RAS Songwe,RC Simiyu na Sasa Mkurugenzi mkuu PPP. Ni mtu aliyeacha alama katika kila eneo. Mfano kule Simiyu alipambana mpaka kufikia kuona pamba ikiuzwa kwa bei ya 2200 kwa kilo bei ambayo haijawahi kuwepo katika Historia ya Taifa letu tokea lipate uhuru.
 
Yeye ndie sio...ndo wa kwanza...huko CCM!?

Kaeni kimya. Mnatia aibu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeendelea kumfuatilia na kufuatilia mahojiano mbalimbali ambayo amekuwa akifanya na ambayo amefanya kupitia vyombo vya habari kuelezea mambo mbalimbali kuanzia uchumi,uwekezaji,biashara na mengine mengi. kila mtu pasipo kujali itikadi yake ya Kiasia au chama chake anakili kuwa Mheshimiwa David Kafulila Ni Hazina kubwa kwa Taifa letu na anapaswa kutumiwa vyema kwa maslahi mapana kwa Taifa letu.

Nimeona namna anavyoitetea na kuisemea vyema serikali yetu chini ya Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa ufasaha ,hoja ,takwimu na ushahidi wa kiutafiti na wa ukweli. Anaeleza kwa lugha nyepesi ambayo watu wanamuelewa vyema sana huku mitaani na kuielewa vyema sana serikali yetu kupitia ufafanuzi wake anao utoa.

Anaeleza kwa utulivu,upole na unyenyekevu mkubwa sana. Angalia namna alivyoelezea juu ya Deni la Taifa,ongezeko la watalii hapa nchini ,suala la ajira na ukuaji wa uchumi wetu. Akaeleza kuwa pamoja na kwamba watu wanasema Deni limekuwa lakini uchumi wetu umekuwa zaidi ndani ya Muda mfupi wa Rais Samia kutoka Dolla Billioni 66 mpaka Dolla Billion 85. Akaeleza pia kuwa kukopa siyo dhambi bali inategemea unakopa kwa ajili ya nini.akasema kama unakopa kwa ajili ya kulipa mishahara hapo ndio inakuwa tatizo.

Mheshimiwa Kafulila amekuwa mtetezi mkubwa sana wa Rais Samia na serikali yake kupitia vyombo vya habari na mitandao. Anaifanya kazi hiyo kwa weledi na uzalendo mkubwa sana.anawafumbua macho watu wengi sana ambao wengi walikuwa wamepofushwa akili na macho na upotoshaji wa baadhi ya watu wenye nia mbaya na chuki binafsi na Mheshimiwa Rais na Serikali yake.

Mheshimiwa David Kafulila amefanikiwa kwa hoja nzito na kwa lugha rahisi na kwa takwimu kuzizima na kuzisambaratisha kabisa kama mvuke hoja za upinzani walizokuwa wanazitumia kupotosha wananchi hususan wale wasio na uelewa wa baadhi ya mambo hususani ya kiuchumi.

Mheshimiwa David Kafulila mbali na usomi wake mkubwa lakini unamuona ni mtu mnyenyekevu na mzalendo wa kweli kwa Taifa letu. Ni mtu na kiongozi aliye nyooka kama rula. Hanaga kupinda pinda. Ni mtu ambaye kwake nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi. Hata umshambulie kwa lugha kali utaona yeye amebakia katika utulivu na kujibu kwa hoja. Katika hili mnaweza kurejea mapambano ya hoja bungeni wakati wa sakata la Escrow namna alivyokuwa mtulivu katika kutoa hoja na kutetea hoja zake.

Mheshimiwa David Kafulila Ni chuma na kiongoz anayekubalika kwa hoja zake na watu wa vyama vyote iwe upinzani na ndani ya chama chetu cha CCM.kwa sababu yeye wakati wote husimama katika hoja na kuitetea hoja kwa takwimu.

Mheshimiwa Rais Aendelea kumtumia Mheshimiwa Kafulila kwa sababu ana mapenzi mema na Taifa letu na ni mzalendo na amekuwa mtetezi wake kwa yote ayafanyayo. wakati unakuta wengine wamejikausha tu pale serikali inaposhambuliwa kwa hoja za upotoshaji. Mheshimiwa Kafulila amekataa kabisa kivitendo kukaa kimya pale anapoona kuna watu wanapotosha mambo kwa lengo la kuichongaisha serikali na wananchi au kuifanya serikali ichukiwe na wananchi.amekuwa akitoka hadharani na kujibu mapigo kwa hoja na takwimu na kusambaratisha kabisa mijadala ya kiuopotoshaji.

Mheshimiwa David Kafulila Ni Hazina kwa Taifa letu tunayepaswa kumtumia kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Ni mtu safi, mzalendo na mchapa kazi kwelikweli. Ndio maana huwezi ukamkuta na doa la rushwa au ufisadi au matumizi mabaya ya madaraka katika maeneo mbalimbali aliyoitumikia Taifa letu. Zaidi utakuta alama njema za kiutendaji alizoziacha katika maeneo aliyopita na kukumbukwa kwa uchapakazi wake ulioleta matokeo chanya.

Watanzania tunapaswa kuwatia moyo na kuwaunga mkono wazalendo aina ya Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan na David Kafulila. Tukikaa kimya tukaacha wakashambuliwa na wenye maslahi yao binafsi tutakuwa tunawakatisha tamaa na kuwapa ushindi mafisadi na wenye kulinyonya Taifa letu kwa mirija.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kafulila ni mtu mzuri nakubaliana na wewe Lucas Mwashambwa
 
Mnalipwa...
Shame
Yeah, We paid to defend our future country regardless what.
Hata wewe tukigundua unachukia rushwa kwa moyo na nafsi yako toka ndani ya roho yako tutakuunga mkono tu
 
Sio hazina tu ni Lulu.
Kama Taifa lazima tuwaecourage watu wanaosacrifice maisha kwaajili ya watu sio mtu akifa ndio ooooh ooohhh stupid
 
Back
Top Bottom