David Kafulila: Taarifa zinaonesha umasikini wa bara la Afrika ulipaa zaidi wakati ambapo misaada ya wahisani ilikuwa juu zaidi

Kumbe nia ya wazungu kutusaidia nikutaka tuendelee kuwa tegemezi?

Hakuna kurudi nyuma lazima tupambane
 
Mimi nafikiri ungejibu hoja yake kwani Mimi naona,

Wewe Kwa UCHADEMA wako unaweza usione kazi anayoifanya Kafulila lakini mbona CHADEMA hamtaki kuzijibu hoja zake?

Kafulila amekuwa na hoja ngumu ngumu kiasi ambacho hamuwezi kumpinga na hiki ndicho mlichonakiwa nacho.


Hoja Vs Hoja,

Njoo ukanushe hii
 
Lakini naamini hili sio lengo la watoa misaada,

Watoa misaada na wao wameishiwa fedha hiyo ndio sababu kubwa.
 
Kafulila kwenye hoja wewe ni mwanaume 👏👏👏👏
 
Twende kazi

Uchumi unakuzwa na uzalishaji ni kiasi gani cha hiyo mikopo ilienda kwenye usimamizi wa tija.

Either kupitia serikali au sector binafsi; na usimamizi wake wa ku recoup investment ulikuwaje.

Nipe jibu tuchague sehemu ya kupeleka lawama na sababu zake. Halafu tuanze mjadala.

Sio Kafulila wala wewe, wenye kuweza huo mjadala.

Tunaposema waty hawana uwezo is not personal, kwa sababu hata wewe nikisema twende na maswali yako mbele huna uwezo wa kujibu miaka 800 nina uhakika huo

Sasa sio namponda Kafulila out of the blue nishamsoma na kuona anaongelea vitu ambavyo yeye mwenyewe anaulewa navyo mdogo mnooo.
 
Sasa wewe unachokisema ndicho alichoandika Kafulila,

Kwamba Uchumi unajengwa kwa uzalishaji Wala sio Misaada.

Sasa hoja yako hasa ni ipi?
 
Miaka ya 60 mpaka 70, Taifa la Nigeria pesa yao Naira ilikuwa na thamani kubwa kuliko Dola ya Marekani

Yako wapi leo?
 
Sasa wewe unachokisema ndicho alichoandika Kafulila,

Kwamba Uchumi unajengwa kwa uzalishaji Wala sio Misaada.

Sasa hoja yako hasa ni ipi?
Twende kazi

Hakuna mtu atakukopesha bure tu.

Lender anataka return, hasa private lender. Hela ambazo nchi kama Tanzania ilikuwa inapata zilikuwa zinatoka wapi na kwanini tulishindwa kurudisha?

Mind you unapokopa unakuwa na collateral na economic plan ya kurudisha.

Ni vipi kushindwa kwako kulipa iwe lawama ya mkopeshaji tena kwa riba ndogo?

Zungumzia kwa mazingira ya Tanzania na riba za nyakati huo.
 
Hapo Kafulila amevimbiwa tu.
Siku akiachishwa hicho cheo akili zitakaa sawa.
 
Misaada imeua kila kitu Cha Africa
Ni kweli hata mtu akiwa tegemezi kwako miaka yote,
Basi hawezi kufanya lolote lile
Hii ni kama Taifa pia
Hebu fikiria Professor Tiba analalamika sisi kukatiwa misaada badala ya kutumia akili yake na kusema lazima tujikomboe kwa wazungu

Najua Umasikini ni Laana
 
Sasa wewe unachokisema ndicho alichoandika Kafulila,

Kwamba Uchumi unajengwa kwa uzalishaji Wala sio Misaada.

Sasa hoja yako hasa ni ipi?
Ndio uelewe kwamba nikikwambia huwezi kunijibu nina uhakika.

Na nipasema Kafulila hana uwezo wa mambo anayoongelea ni kwamba hana uwezo nayo.

Tanzania kila kitu rahisi
 
Ni wakati wa bara la Africa kuamka Sasa hali ni mbaya
 
Kafulila tunamjua anauwezo wewe ni nani mwenye uwezo lakini hatukujui?
Sema wewe ndio hunijui, lakini wenye nafasi ya kutaka kunijua tayari wananijua kwa kunitumia salamu kupitia watu wanaonijua.

Na majibu yangu kwao, I am not interested.
 
Sema wewe ndio hunijui, lakini wenye nafasi ya kutaka kunijua tayari wananijua kwa kunitumia salamu kupitia watu wanaonijua.

Na majibu yangu kwao, I am not interested.
Sasa jitambulishe na wewe watu wakujue kwa kuwa Kafulila tangu akiwa Bungeni tunafahamu ni kijana wa hoja Kali Kali
 
Sasa jitambulishe na wewe watu wakujue kwa kuwa Kafulila tangu akiwa Bungeni tunafahamu ni kijana wa hoja Kali Kali
Mwache Kafulila afanye yake, elewa tu wahusika wananijua (huko, serikalini) Iła sina interest.

Furaha yangu ni kuwananga tu wote huko serikalini; it’s never personal nk kwa maslahi ya nchi.

Nafasi za teuzi tuwaachie wengine na wengine tukubali kuna
maisha nje ya siasa; Lakini kusema hatutoacha mdomo ni mali yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…