David Kafulila: Ubora wa Treni ya SGR ya Tanzania unazidi treni nyingi za Ulaya

David Kafulila: Ubora wa Treni ya SGR ya Tanzania unazidi treni nyingi za Ulaya

Bandari ya Dar inaendeshwa kwa PPP kati ya TPA na DP World.

DP World ilingia Mkataba na TPA kabla hata Kafulila hajawa Mkurugenzi wa PPP, acheni kupotosha, tunataka Kafulila aseme wazi tokea achaguliwe ni mradi gani wa PPP ameuleta nchini, na unafanya kazi, mmoja tu aseme..!! Kafulila kazi kusifia sifia hata miradi ambayo sio ya PPP, mfano SGR au JNHPP sio PPP, yaani hajui hata kazi yake vema huyo..!!
 
Ukweli ni upi?
DP World ilingia Mkataba na TPA kabla hata Kafulila hajawa Mkurugenzi wa PPP, acheni kupotosha, tunataka Kafulila aseme wazi tokea achaguliwe ni mradi gani wa PPP ameuleta nchini, na unafanya kazi, mmoja tu aseme..!! Kafulila kazi kusifia sifia hata miradi ambayo sio ya PPP, mfano SGR au JNHPP sio PPP, yaani hajui hata kazi yake vema huyo..!!
Kwahiyo inasemaje?
 
View attachment 3386333

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila akiwa katika kipindi maarufu cha Mada Kuu kinachorusha na kituo cha runinga cha Utangazaji cha TBC,

Kafulila amezungumzia Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika nyanja mbali mbali akitolea mfano Ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR yenye urefu wa km 2,809 itakapokamilika itagharimu $10.4bn au TZS 26 Trilioni.

Kafulila anasema ukisafiri na treni mpya ya SGR katika kipande kilichokamilika kutoka Dar mpaka Dodoma unaweza kuweka glasi ya maji juu ya meza na isidondoke.

Endelea kumsikiliza mpaka mwisho,
Naanza kukonect dot unaweza kuta kafulila ndiye anajiita Lucas Mwashambwa hapa JF maana wameshabihiana sana kiuchawa
 
Azisifie za Ulaya, atakuwa haipendi na hiyo kazi yenyewe na kitengo chake kinamtaka kulambalamba miguu ya aliyemteua

Tanzania vipofu ni wengi sana, mtu anaweza asipewe kofia, baiskeli n.k ili apige kura, lakini anaweza pewa cheyo ili alambe miguu
Tanzania ilikuwa haina National Television hadi mwaka 2000,
Mwanzoni mwa miaka ya 1980 tulikua tunaambiwa lile jeno la kitega Uchumi ndiyo refu sana katika hii dunia, ingawa tulikuwa tunaangalia senema Avalon na Empire, wanasiasa wa nchi hii bila ya uongo hawawezi kusitawi. Na hii ndiyo athari mojawapo ya Ujamaa/socialism/communism. Unakubali kudanganywa.
 
bado hajasema treni ya mama glas ya maji haidondoki kwenye treni kama ulaya.
 
Kenya walianza kujisifia SGR kabla hawakamilisha reli yao basi ilipofika Naivasha tu wahuni aka wakora wakafika benki na kulamba dolari za kukamilisha reli, sasa wanalipa deni na reli haizalishi kitu, hivyo huyu dingi anapaswa kujisifu reli yetu ikifika Mwanza na Kigoma, kwasasa hizo ni chai tu maana gharama za uendeshaji ni kubwa kuliko mapato
 
Huyu jamaa ndio maana Hayati Werena alimuita tumbili kwa kweli hakukosea...
Anafikiri Watanzania wote hawajawahi kufika ulaya au sio...kwanza anazungumzia ulaya ipi?
 
Back
Top Bottom