==
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila katika ukurasa wake wa tweeter ( X ) amemtetea na kumpongeza Rais wa Tanzània Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupata ripoti nzuri ya CAG,
Bwana David Kafulila anasema Rais Samia na katika Kipindi chake hiki kifupi na kwa mujibu wa ripoti ya CAG ameongeza zaidi hati safi kutoka 800 za wakati wa Hayati Dkt John John Magufuli hadi 1,295 za sasa.
David Kafulila anaendelea kwa kusema vilevile Dkt Samia Suluhu Hassan amepunguza hati chafu kutoka 10 za Wakati wa Hayati Dkt Magufuli hadi 1 wakati huu wa Dkt Samia.
Wakati hati zenye mashaka nazo zikipungua kutoka hati 81 za Wakati wa Hayati Dkt Magufuli mpaka hati 5 za Wakati wa Rais Samia Sasa,
Kwa matokeo haya na Kwakuwa namba hazidanganyi Huenda Rais Samia hapigi sana kelele kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake ila yeye Sasa anatenda kazi zake kupitia kalamu kimya kimya kama alivyowahi kukaririwa na vyombo vya habari wakati flani.
==
==