Kwanza PK ni special guest katika mikutano ya Davos.
Pili, jana hakukutana na Zelensky pekee bali pia alikutana na Antony Blinken.
Isitoshe PK alikutana na bwana Jacob Stausholm ambae ni boss wa Rio Tinto, waifahamu Rio Tinto weye? Hii ni kampuni kubwa ya uchimbaji madini duniani. Hivyo hapo patafutwa ushirikiano (partnership) na uwekezaji na hawa wote wauliza masuala kama usalama na stability.
PK pia kakutana na bwana Jean Todt ambae ni mwakilishi wa umoja wa mataifa aneshughulikia masuala ya usalama barabarani hivyo hapo suala la barabara safi na mikeka ya uhakika kurahisisha usafiri murua wa barabara yaani "mobility" yaangaliwa.
Mkutano na Blinken ni mwendelezo wa mazungumzo ya Rwanda na mabeberu kuhusu mgogoro wake na Congo DRC.
Kama hufahamu mwezi Novemba mwaka jana mkurugenzi wa Usalama wa taifa wa Marekani (DNI) bi Avril Haines alizuru Rwanda kuzungumza na PK na suala ni stability.
Hivyo PK na Ndyashimiye walikutanishwa ili kujadili tensions zilizopo sasa hivi kwamba Congo DRC walalamika kwamba PJ atumia Proxy groups za M23 na kundi jingine ni Matabala au something kusababisha issues.
Hivyo PK huwa haendi bure kwenye hivi vikao vya DAVOS ambavyo hukutanisha maglobalists.
Umenipata hapo?