Kwa furaha kubwa kabisa napenda kuwataarifu wana JF kuwa kwa tukio litakalotokea leo tarehe 24/07/2023, mjadala wa Dp world ndio unafika mwisho, tujipongeze wote tulioshiriki. Ahsanteni sana. ========== Mdau mwingine pia aliandika: Tumelumbana weee, tumeelezana weee, Kuna wale vichwa maji...
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu akiwa Mkoani Kagera, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, amemjibu Kinana aliyewatuhumu Viongozi waandamizi wa CHADEMA kukosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hasani aliyewafutia kesi. Lissu amesema, hawawezi kushukuru kwa kufutiwa kesi za uwongo...
Nimesikia kwamba Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Samiah Sukuhu Hassan hataki kusikia maoni ya wananchi wake juu ya mkataba wenye ukakasi wa ugawaji bure wa Bandari zote za Tanganyika.
Sina shaka habari hizi ni za ukweli, maana nimeona video clip, na it seems aunthentic. Sasa hapa kuna maswali mazito ya kujiuliza, na kuna maoni ya kutoa.
MASWALI.
1.) Je, ni kosa kutoa maoni juu ya utendaji mbovu wa serikali kuhusu mkataba huu? Kwamba ukitoa maoni hasi basi zinakuwa ni kelele? Sisi tunakupigia kelele?
2.) Je, hoja za wananchi (au kelele kama ulivyoamua kuziita) umezisikia vyema? Majibu yake ni yepi, kwanini usijibu hoja za msingi za hao wapiga kelele ili waache kupiga kelele? Au unazipenda hizi kelele?
MAONI
Kama mtu akiziba masikio, namna bora ni kuweka loud speaker na kumsogelea karibu, hadi akimbie yeye.
==========================
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?
3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!
6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amekiri kuwa ni kweli tangu Bunge la Tanzania liliporidhia azimio la Nchi ya Tanzania kuimarisha mahusiano yake Nchi ya Tanzania na Nchi ya Dubai hasa katika maeneo ya Kiuchumi na Kijamii, kumekuwa na mijadala mingi, maoni, ushauri na hofu za Uwekezaji nchini...
Kwa furaha kubwa kabisa napenda kuwataarifu wana JF kuwa kwa tukio litakalotokea leo tarehe 24/07/2023, mjadala wa Dp world ndio unafika mwisho, tujipongeze wote tulioshiriki. Ahsanteni sana. ========== Mdau mwingine pia aliandika: Tumelumbana weee, tumeelezana weee, Kuna wale vichwa maji...
Kutoa maoni sio kosa bali kosa ni kulazimisha maoni yako yafanyiwe kazi.
Angalau sasa watu wanaongea na kutoa yao ya moyoni kabla ya hapo ni mwendo wa kupotezwa au kushughulikiwa.
Kama wabunge wamepitisha mi nakushauri fanya yako yanayoihusu familia, Kama vipi nenda ukaandamane uvunjwe kiuno. Mama kabeba dhamana ya kuwaletea maendeleo wananchi kwahiyo usimpangie namna ya kuleta hayo maendeleo, nenda kaandamane au subiri 2025 utoe hukumuu yako kwenye sanduku la mpiga kura
Huyo unaemtisha nani sasa? Kwani sasa hivi amani ipo Acha kuwa na akili ndogo kisa hongo ambayo utakufa na kuiacha huku vizazi na vizazi vikipoteza uhalali wa nchi yao
Ngoma inogile, Mbunge wa Iringa mjini Jesca Msambatavangu amesema ni kweli kabisa Mkataba wa Bandari hauna Muda ni wa Milele na hilo ni jambo zuri kwa sababu unaweza kuvunjwa Wakati wowote si hauna Muda. Jesca alikuwa akihutubia kwenye mkutano wa wana CCM wa Iringa mjini. Je, unakubaliana na...
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
UTANGULIZI rais Samia ameshasema yeye atajibu kwa vitendo na pia Kuna fununu kuwa hata wasaidizi wake wameambiwa wasijibu maana hakuna kurudi nyuma tena KIHISTORIA Hakuna jambo liliwahi kushindikina kimvuatano Kati ya CCM na upinzani na upinzani ukashinda kama lipo litaje ? Hakuna taasisi...
Rais Samia, Waziri Mabarawa na katibu mkuu wao ktk wizara anayo ongoza Mbarawa ni kutoka Zanzibar na ndio waliouza bandari za Tanganyika wakaacha kuuza za Zanzibar. Nyakati zote Wazanzibar wamekuwa wakijiita na kujivunia Uzanzibari wao kama taifa. WazanzibarI wanacho kitambulisho cha ukaazi cha...
Ushahidi wa kimazingira. Circumstantial evidence ni kuwa huu mkataba mbovu kuna watu wamekula rushwa. Taifa letu linahitaji mashushushu kama hayati Lyatonda Mrema. Leo hii tungejua kila mtu namna alivyohongwa na kuisaliti Tanganyika.
Mwezi mmoja uliopita ROSTAM AZIZ Alitangazia Umma kwamba mahakama zetu hazifai kwamba eti zinaingiliwa kwa maelekezo! Maneno hayo mazito kutoka kwa Rostam hayakuwa ya burebure! Bali ni maneno ambayo yalitoka kwenye kinywa cha mtu anaemaanisha wala siyo kuteleza! Pamoja na Rostam kuombwa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.