Nilikwambia siku nyingi uwe unanisalimia unaniringia, mpaka uletewe vithibitisho!Kumbe huwa mshangazi wewe nitaanza kupa heshima yako
Duh siwatakiYeahp as long as sio kibonge
Naam mkuu,hiki ndo kinacho fanyika kwa wengi aidha kwa kujua ama kuto kujua..Hamna anachofanya hapo. Ni anakaza mwili tu kuwa fiti ila hawezi punguza uzito.
Daaah ukweli mchungu huuMkuu hakuna dawa ya kupunguza unene,hakuna, yaani eti unywe kidonge halafu usijinyime kula au kufanya mazoezi eti uzito upungue,hiyo dawa haipo,kama ipo ni sumu mfano Ozempic ni sumu inayoleta upofu.
Kuna msemo wa kiingereza unasema " you can't eat your cake and have it" na hicho ndo unachokitaka wewe. Yaani hutaki kuumia halafu unataka upungue,nakwambia tu haiwezekani.
Ratiba yako ya kazi hata sio ngumu,,unaweza kuamka saa kumi na moja alfajiri ukafanya mazoezi hadi saa kumi na mbili. Pia unatoka kazini mapema sana,unaweza kufanya mazoezi baada ya kutoka kazini hata masaa mawili kila siku,ni wewe hujataka.
Pia nadhani unakula vyakula vibaya eg vyenye mafuta mengi,pia hapo kwenye pombe,sidhani kama ukipunguza kunywa pombe hata siku moja utakufa au utaumwa.
Kupunguza uzito ni kitendo ambacho sio rahisi na lazima ulipie gharama,hakuna shortcut,haipo.
Mwisho: Nakuchana live ,kama hutaki kujinyima ili upungue pressure na sukari vitakufundisha ujinyime kwa lazima. Kama hutaki kujinyima pombe ili upungue,pressure na kisukari vitakufundisha kujinyima pombe kwa lazima. Hapo bado hujaambiwa una matatizo ya uzazi mbegu zimekuwa nyepesi kwa kula hovyo hovyo, na hayo matatizo ya afya siku hizi yanawakumba vijana wadogo miaka 29 kushuka chini.
Chaguo ni lako,jinyime na ufanye mazoezi sasahivi au subiri baada ya miaka kadhaa magonjwa yakulazimishe kufanya mazoezi na kula vyakula vinavyotakiwa.
Have a nice day.
Wanashida gani ?Duh siwataki
Lazima tuambizane ukweli mkuu,vijana wadogo wanaoumwa pressure,kisukari, moyo,figo kwa sababu ya lifestyle ni wengi mnoo na wanazidi kuongezeka kila siku. Tena wewe unaekaa kila siku asubuhi hadi jioni ongezea matatizo ya kiuno na mgongo,utaumwa mgongo hadi utaje majina ya mababu zako. Usipochukua tahadhari you are next yaani you are next.Daaah ukweli mchungu huu
hawana shida yoyote!Wanashida gani ?
Wee misosi huwezi acha, tafuta watu wakuloge au kuchua mkopo ukuendeshe puta.Hapa hiyo siwezi
Wewe hatukupi dawa tunakusimanga mpaka ukonde.Nimekosa dawa kabisa wakuu?
Kama una shida wewe ndio unitafute Mimi.Kichwa cha Habari
Natafuta dawa ya uhakika ya kupunguza uzito (Kilo 105, Futi 6). Ahadi ya malipo ipo, sitaki msaada wa bure.
Wakuu salama,
Nipo hapa nikiwa na nia ya dhati kabisa ya kufanya biashara na mtu mwenye suluhisho la uhakika. Niko siriaz na sijiomba msaada, kama una dawa inayofanya kazi kweli, nitakulipa vizuri sana.
Mimi ni kijana wa miaka 26, nina urefu wa futi 5.5 mpaka 6 hivi, lakini uzito wangu umefika kilo 105. Kiukweli unene huu kuwa chibonge na kitambi umeanza kunikata mawazo na kuondoa muonekano wangu wa ujana
Kabla hamjaniletea yale mapendekezo ya kawaida, naomba niweke wazi mtindo wa maisha yangu ili anayeleta dawa ajue anadili na mazingira gani
Sina muda wa mazoezi, Ratiba yangu ni ngumu Naamka saa 12 asubuhi, naingia kwenye shughuli zangu ambazo asilimia 90 ni kukaa tu kuanzia asubuhi hadi jioni, Nikitoka saa 10 jioni natumia usafiri wa gari hadi nyumbani Hakuna muda wa kutembea wala kukimbia.
Siwezi kuacha kula au kupunguza msosi Hapa tusidanganyane, siwezi kukaa njaa.
Mimi ni mnywaji, Kila siku jioni lazima nitoke kwenda kupata kileo hadi usiku Sinywi bia, mimi ni mtu wa pombe kali na sibadili brand matumizi yangu ni Hanschoice kila siku. Na kama mnavyojua, pombe kali inataka msosi mzito mzito, kwa hiyo suala la Diet hapa halipo.
Kutokana na mazingira hayo, suluhisho pekee ninalolitaka ni dawa maalum ya kukata wese na kupunguza mwili bila kunitegemea mimi nifanye kazi ya ziada ya kukimbia au kushinda njaa.
Kama wewe ni una duka la dawa za asili/kisasa, au una siri ya dawa yoyote ya uhakika ambayo imeshawahi kukata kitambi na uzito kwa mtu mwenye mtindo wa maisha kama wangu
Shusha nondo zako hapa chini jinsi dawa yako inavyofanya kazi.
Njoo PM tufanye biashara. Gharama sio tatizo, ilimradi tu isiwe utapeli na iwe na matokeo yanayoonekana.
Nawasilisha kwa heshima wakuu.