Dawa ya Umaskini, madeni, ukata, mifuko kutoboka, uhitaji, kufilisika hii hapa!

Dawa ya Umaskini, madeni, ukata, mifuko kutoboka, uhitaji, kufilisika hii hapa!

INTRODUCTON.

Leo naongea na wote wenye uhitaji wa pesa, Kila mpango wako kupata pesa umekwama,

Naongea na wote wenye ukata wa pesa, walioajiriwa na Wana mishahara lakini wanadaiwa Kila Kona, mshahara hautoshi.

Naongea na wenye biashara ndogo na za kati ambao wanafanya juhudi zote kujitoa walipo kiuchumi lakini wanazidi kudidimia kwenye dimbwi la Umaskini.

Naongea na wote wenye madeni Sugu Kila Kona, wangependa kulipa madeni hayo Ili wawe huru lakini hawaoni njia ya Kupata kipato kulipia, ndo wanawaza kukopa tena.

MY LIFE EXPERIENCE.

Nilipokuwa kidato Cha SITA, jobless, wakati nikisubiri mchakato wa kujiunga na chuo kikuu, nilirudi nyumbani kwetu.

Nikiwa nyumbani, nilipata shida sana kuishi nyumbani bila KAZI yoyote Kwa kipindi kile.

Siku moja, nilipewa pocket money na Mzee ya Tshs 20,000, nilikuwa na mahitaji mengi zaidi ya pesa niliyopokea, nilishukuru kupokea pesa hiyo kidogo na kuondoka kwenda kununua mahitaji yangu binafsi,

Nilinunua mahitaji machache na nilibakiwa na 2,000 tu.

Jumatano siku iliyofuata ilikuwa siku ya maombi Kanisani kwetu, niliondoka nyumbani mdogo mdogo nikielekea Kanisani, njiani nilinunua vitu vingine vidogo vidogo na kubakia na shs 600.

Nilianza kupata mawazo sababu pesa imeisha na mahitaji yangu hayajaisha na sijui lini tena ntabahatisha kupata pesa ingine.

Nikiwa njiani kuelekea Kanisani, niliwaza nisitoe sadaka niitunze hiyo 600 Ili ilinde mfuko wangu maana sikujua lini tena ntapata pesa,

Nikiwa katika kuwaza huko, ndipo lilinijia wazo la kumjaribu Mungu kupitia matoleo.

Niliwahi soma BIBLIA (Malachi 3:10-12). Nikakutana na andiko linaloongelea jinsi ya kumjaribu Mungu Kwa matoleo.

Niliwaza kuwa, sh 600 niliyonayo ni ndogo, isingenifikisha popote, kwanini nisiitumie hiyo kumjaribu Mungu?

Niliongea na Mungu ndani ya NAFSI yangu na kumwambia Mungu, Ewe mwenyezi Mungu, umesema katika neno lako kuwa nikujaribu Kwa matoleo na ZAKA Ili nisipungukiwe, Nami Leo hii naitoa pesa hii yote,akiba pekee niliyonayo Ili nione ikiwa utanibariki au la, nililenga kumjaribu Mungu kupitia neno lake.

Nilitoa sadaka Ile na kuondoka kurudi nyumbani, wakati natoa sadaka Ile ilikuwa saa tisa jioni,

Ilipofikia saa mbili usiku, nilipigiwa simu na Rafiki yangu ambaye Yeye baada ya kumalisha masomo, alipata ajira ya mkataba Mahali Fulani. Aliniambia kuwa anajisikia kunitumia pesa kidogo Kwa ajili ya matumizi madogo muda huu nikiwa Sina KAZI.

Haukupita muda, message mbili za mpesa ziliingia Kwa kufuatana, Nilipoangalia, alikuwa amenitimia 30,000/=

Tangu hapo, maisha yangu ya utoaji yalibadilika, Kila kipato nilichokipata nilitenga sadaka kwanza na kuinenea nilichotaka sadaka hiyo ifanye.

Hadi sasa navyoongea nawe, ninaishi maisha yangu vizuri sana, sio tajiri sana, lakini sipingukiwi na chochote ninachohitaji.

Nikiona naeekea kuishiwa, huchukua akiba kidogo niliyonayo huenda kuitoa nikinuia mahitaji ambayo ningependa Mungu anisaidie kuyatimiza na hujibiwa Kwa haraka sana.

SOLUTION.

-Kwa wenye Madeni.
Chukua pesa yote kidogo uliyonayo, tafuta mtumishi wa Mungu anayeishi maisha magumu, mpe sadaka hiyo, inenee sadaka Yako Yale Mungu ungependa akutendee.

-Kwa wanaopokea mshahara na haufiki mwisho wa mwezi.

Chukua mshahara wako Tenga sadaka kabla ya kufanya matumizi yoyote, peleka sadaka Yako Kwa maskini au wahitaji maskini, au hospitalini Kwa walioshindwa kulipa gharama za matibabu, au peleka Kwa mtumishi wa Mungu inenee sadaka Yako na utanipa majibu.

-Wazee wa betting.

Chukua pesa ambayo umepanga kupeleka betting, nenda tafuta familia maskini, wanunulie chakula na mahitaji, inenee sadaka Yako ukimwambia Mungu, nakujaribu Kwa sadaka hii, utaniambia majibu.

- Kwa Wafanyabiashara.

Chukua pesa kwenye mtaji wako, usitoe mabaki, Chukua sadaka kubwa itakayokuuma, ichukue peleka Kwa wahitaji mahispitalini, wapewe ombaomba barabarani, au toa Kwa wahubiri INJILI mabarabarani Kisha mwambie Mungu kuwa unamjaribu Kwa kupitia neno lake mwenyewe na asipolitimiza ni Yeye sasa.

HAKIKA Mungu hawezi vumilia jaribu Hilo, atakujibu haraka iwezekanavyo, Mimi nakushuhudia maisha ninayoishi halisi Hadi Leo.

NB: Wanaokwenda Kwa Waganga na wachawi kutafuta utajiri ni "WAPUMBAVU" Kwa maana Mungu ameruhusu ajaribiwe kupitia matoleo na hawezi shindwa kuwajibu sawasawa na NENO lake.

Amen.

Karibuni Kwa maswali na shuhuda Kwa watakaochukua ushauri huu na kuufanyia KAZI[emoji120]
Mungu huyu huyu ambae kuhani wake mkuu wa Dunia anasema watu wa jinsia moja tuoane!!

Sawa tumekusikia mchungaji
 
Barikiwa sana,Uzi mzuri,umeinua kiwango Cha Imani yangu Kwa namna Fulani....hakika nitamjaribu Mungu
Mimi ndo kamekuwa kamchezo kangu kitambo sasa.

Nikitaka kuanza ujenzi, naanza na sadaka,

Naweza Anza ujenzi nikiwa na lak 5, nitajenga Hadi namaliza laki Tano Iko pale pale,

Natumia ktk ujenzi nalipa Kila kitu na haikauki, Kila nikienda kazini napata ya kijaziliza laki 5,

Majirani wasonifahamu hudhani labda mm ni Tajiri sana kumbe wap!!
 
Mungu huyu huyu ambae kuhani wake mkuu wa Dunia anasema watu wa jinsia moja tuoane!!

Sawa tumekusikia mchungaji
Huyo Si kuhani wake mkuu duniani ikiwa anasema machukizo hayo.

Jikite kwenye mada mjaribu Mungu kupitia matoleo na uje utupe ushuhuda.

Amen
 
Uwaambie pia sio watoe sadaka halafu waende wakawaf.ire watoto wawatu..watasema kila siku wamerogwa..watende pia matendo mema.
Huwezi pata pesa za Muujiza wa Mungu halafu upate ujasiri kutenda UOVU.

HAKIKA Imani Yako ikikua, utazama deep kumtafuta kumjua Mungu zaidi.

Ubarikiwe.
 
Sahihi na nimeshuhudia mkuu
Share nasi ushuhuda wako kama hutojali,

Watu humu tukiwaambia maandiko yasemavyo wanadhani ni hadithi, lakini tukishuhudia uhalisia wa applicability wa kulitumia NENO la Mungu kuleta matokeo chanya wataamini na kuepuka kwenda Kwa " WAPUMBAVU " Waganga na wapiga tunguli.
 
Ety kupata pesa za haraka!!

Wachungaji wa siku hizi mna shida sana.
Ndio, njia hii Mungu hujibu haraka sana.

Imagine una akiba pekee ya lak 2 Kwa Mfano,

Ukiichukua yote na kumjaribu Mungu Kwa kuwapa maskini chakula, au wenye uhitaji,

Mungu hawezi kuruhusu ulale njaa,

Atajibu haraka sana.

Nikuambiayo Si hadithi, ninatumia njia hii Mimi.

Amen
 
Mimi ndo kamekuwa kamchezo kangu kitambo sasa.
Kamchezo!!!?????

You can't be serious we mtoto, Mungu hajaribiwi kijinga namna hiyo like you do.

Huyo Mungu unayemchezea hako kamchezo utakuwa unamjua mwenyewe tu, Siyo huyu Mungu mkuu wa Ibrahim, isack na yacob.
 
Ubarikiwe.

Baraka za Mungu hazina majuto.

Mungu Mbinguni anatushangaa tunapolia ukata na wakati amekataza mwanadamu kumjaribu Mungu Kwa mengine isipokuwa katika matoleo, sadaka na ZAKA.

Amen
kuna jambo nimelipata kuna magumu napitia sana ni mwaka wa pili chungu sana kwangu ngoja nifanye na nishitakie baadhi ya mambo juu yake
 
Ndio, njia hii Mungu hujibu haraka sana.

Imagine una akiba pekee ya lak 2 Kwa Mfano,

Ukiichukua yote na kumjaribu Mungu Kwa kuwapa maskini chakula, au wenye uhitaji,

Mungu hawezi kuruhusu ulale njaa,

Atajibu haraka sana.

Nikuambiayo Si hadithi, ninatumia njia hii Mimi.

Amen
Ungewashauri kwanza wachungaji wenzio watumie hiyo njia uchwara ili waache kulia lia shida kwa waumini.
 
Good,
Yatupasa tutambue kwamba chochote ambacho MUNGU ametubariki ndani yake ameweka mbegu.
Tusile mbegu bali tupande mbegu
 
Daaah hivi hapa wanaruhusiwa kutukana? Au niku dm kwa matusi makubwa sana
Usitukane,

Nenda kamjaribu Mungu Kwa kuwanunulia chakula yatima wanaorandaranda usiku huu Kwa akiba ndogo iliyo nayo ukimjaribu Mungu sawasawa na (Malachi 3:10-12).

Amini nakuambia, utajibiwa haraka sana, na utarudishiwa zaidi ya ulichotoa.

Amen
 
Good,
Yatupasa tutambue kwamba chochote ambacho MUNGU ametubariki ndani yake ameweka mbegu.
Tusile mbegu bali tupande mbegu
Amen,

Dunia ingejua kuwa kipato mtu akipatacho Si chake pekeake,

Mungu humpa mtu riziki na ndani ya riziki hiyo Huwa ameweka pesa Ili iende Kwa wengine kupitia sisi,

Ukila yote pekeako, unakula mbegu,

Ubarikiwe.
 
Kamchezo!!!?????

You can't be serious we mtoto, Mungu hajaribiwi kijinga namna hiyo like you do.

Huyo Mungu unayemchezea hako kamchezo utakuwa unamjua mwenyewe tu, Siyo huyu Mungu mkuu wa Ibrahim, isack na yacob.
Mungu ameruhusu kujaribiwa kupitia matoleo pekee.

So Mbingu zinatushangaa kuwa wahitaji ilhali IPO KANUNI ya kumjaribu Mungu na hatuitumii kupata pesa.
 
Sifanyi tena huu useenge labda Mungu anipe hayo maelekezo yeye mwenyewe
 
Amen, kuna siku kuna hela nilikua naiexpect muda mrefu na ikawa imekwama. Sasa hiyo siku, nilikua nasikiliza video ya mafundisho ya kiroho, mchana hivi. Katika kusikiliza prayer request, nikasikia mama mmoja akituma message namna ambavyo anapitia shida kali sana. Kumbuka na mm hapo nina shida na hela.

Sasa kwenye simu nilikua na 23000. Nilivyoingia kwenye yale maombi, nikasikia Roho Mtakatifu anasema omba namba ya huyo mama umtumie hiyo 20k. Nikataka kuobject kwamba mi mwenyewe apeche, Roho akanisisitiza sana. Basi nikasema sawa, hakuna shida. Baada ya prayer session, nikapiga simu redioni kurequest namba za huyo mama. Immediately nimekata ile simu, baada ya dkk moja, ikaingia ile hela niliyoisubiri kwa muda mrefu iliyokuwa imekwama.

Nilimshangaa sana Mungu. Sometimes ukiwa tayari kumtoa Isaka, Mungu huleta mwanakondoo na kukurejeshea tumaini mara moja. Hakika Bwana yu mwema.
 
Sifanyi tena huu useenge labda Mungu anipe hayo maelekezo yeye mwenyewe
Itakuwa ulienda kupeleka sadaka Yako Kwa manabii wa uongo, wakakufunga.

Nenda saizi mpe Jirani Yako maskini mhitaji, au kamlipie maskini aliye hospitali, mnunulie madawa na lipa bill zake utaniambia.

Ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom