Dawa ya Umaskini, madeni, ukata, mifuko kutoboka, uhitaji, kufilisika hii hapa!

(Yakobo 4:3).

Hata mwaomba Wala hampati,Kwa Sababu mwaomba vibaya, Ili mvitumie Kwa tamaa zenu.


NB: Nenda kafanye nilichokuagiza, Mungu asipokujibu Rudi kuniita mwongo.
Nipe mstari unaosema tumjaribu Mungu...
 
Amen ubarikiwe.

Hakuna njia Rahisi kupata pesa kama kumjaribu Mungu Kwa matoleo, sadaka na ZAKA.

Mungu atusaidie.
 
Nimeshakugundua wewe ni mtoto wa mchungaji umekuja kivingine kupalilia sadaka za babaako
 
Itakuwa ulienda kupeleka sadaka Yako Kwa manabii wa uongo, wakakufunga.

Nenda saizi mpe Jirani Yako maskini mhitaji, au kamlipie maskini aliye hospitali, mnunulie madawa na lipa bill zake utaniambia.

Ubarikiwe.
Hiki umesema nitajaribu
 
Kwahiyo hiyo 600 uliitoa sadaka ya kujimaliza ?
ila ulipopokea mkwanja huku kumbuka 10%.
Safi sana
 
Nimeshakugundua wewe ni mtoto wa mchungaji umekuja kivingine kupalilia sadaka za babaako
Mimi ni mtoaji, naijua KANUNI hii Mungu aliyoweka ya kumjaribu Kwa matoleo.

Sijaweka namba kuomba sadaka, nimeelekeza pelekeni sadaka Kwa wagonjwa hospitalini, wasio na uwezo nk nk.

Mjaribu Mungu hata sasa,

Utakuja na ushuhuda hapa.

Amen
 
Hiki umesema nitajaribu
Amini nisemacho,

Njia hii ni Kweli, Mimi ni aiishi. Sipingukiwi na chochote nachohitaji.

Kumbuka mstari (Malachi 3:10-12). Uutumie huo kumkumbusha Mungu utakapomjaribu na kuweka AGANO nae.

Amen
 
ndugu yangu kwakweli naomba ellimu kidogo kuhusu sadaka
1.ivi nikitoa sadaka bila kuisemea maneno kwa utaratibu uliotoa ile inaenda kua hazina yangu mda wowote ninaweza mkumbusha Mwenyezi Mungu niitumie?
2.lakini pia kama naenda kutoa sadaka kwa utaratibu uliopendekeza yaani kwakuisemea sadaka kwa kuyapa maneno yangu uhai juu ya ile sadaka, na mimi ni mtenda dhambi je nitatakiwa nipate sala ya toba kabla ya kuisemea maneno sadaka na kuitoa ?
 
Na mstari unaosema Mungu hajaribiwi pia Upo!!

This is a complex material
Mungu hajaribiwi, amekataza,

Kwenye ZAKA, matoleo na sadaka ametoa mwanya ajaribiwe.

Tumia Siri hiyo Ili usipungukiwe,

Hutakopa, utakopesha bila kutaka urudishiwe ulichokopesha.

Kukosa pesa na kupungukiwa ni uchaguzi wako.

Amen
 
Sadaka Ina mdomo inaweza kusema yaliyo ndani ya moyo wa mtoa sadaka.

Si Kila sadaka inahitaji kuinenea, zingine unatoa tu.

Pia ni muhimu kutubu na kujitakasa kabla ya Kutoa sadaka, Kutoa sadaka bila kutubu ni kujipalia makaa.

Bt ambao ni wageni, wasomjua Mungu sana, ni sawa kumjaribu kupitia sadaka na baadae utapata maelekezo juu ya nini Cha kufanya.
 
Hao wahitaji walioko mtaani wanatokea kwenye familia..


Saidia familia yako

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
Mungu ameelekeza sadaka zipelekwe hekaluni, Kwa wajane, wahitaji, wagonjwa hospitalini nk nk.

Ndugu na family Yako kuwasaidia ni WAJIBU wako Si sadaka hiyo.
 
Ndaga 🤝🤝
Ila hapo kwenye ombaomba sishauri
Kwingine kote sawa,naunga mkono hoja!
 
Kwahiyo hiyo 600 uliitoa sadaka ya kujimaliza ?
ila ulipopokea mkwanja huku kumbuka 10%.
Safi sana
Nimesema hapo juu kuwa,

Baada ya Muujiza huo, maisha yangu yalibadilika hata Leo,

Nisipotoa sadaka, sipati hatua yoyote maishani Hadi nitoe kwanza.

Ubarikiwe.
 
Ndaga 🤝🤝
Ila hapo kwenye ombaomba sishauri
Kwingine kote sawa,naunga mkono hoja!
Maskini wapo tangu enzi na enzi.

Mungu ameagiza tuwape msaada maskini.

Asema, amhurumiaye maskini......

Ubarikiwe. Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…