Dawa ya Vumbi la Kongo 'hensha' yapigwa marufuku Tanzania

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania, limepiga marufuku matumizi ya dawa aina ya Hensha maarufu kama Mkongo kwa binadamu, na kwamba tayari limekwishaifutia usajili baada ya kubaini imechanganywa na dawa za kuongeza nguvu za kiume (Viagra).

Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Prof. Hamisi Masanja Malebo, ametoa kauli hiyo Julai 27, 2022 mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Profesa Malebo alisema baraza katika uchunguzi wake, lilibaini dawa iitwayo Hensha maarufu Mkongo, yenye usajili namba TZ17TM0027, ilikutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume iitwayo sildenafil, kwa jina maarufu la biashara Viagra ama Erecto.

Alisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na miongozo ya usajili wa dawa za tiba asili na mbadala.

Alisema kituo hicho kimetakiwa kuhakikisha kinaiondoa sokoni mara moja dawa hiyo, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki.

CHanzo: Habari Leo
Prof. Masanja hana adabu.
 
Wao kama akina nan?
 
Kama nawaona vile wazee wa kujibusti wanavyosoma habari hii huku wameshika tama 😂

Naona ile vicks itapanda bei, ngoja nianze hii biashara huenda nikatajirikia humu.
 
Wanaume wasiojielewa walikuwa wanajimaliza wenyewe..
IMG_20220727_174800.jpg
 
Back
Top Bottom