Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Waheshimiwa Viongozi na Wanachama wa Chadema Dar es salaam, Siku ya leo Mwenyekiti wa Chama Mhe.Freeman Mbowe akiwa Kwenye Mkoa wetu wa Dar es salaam, Ameamua kwenda Central police baada ya kuwepo na Taarifa nyingi kwenye vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuwa anahitajika Police.

Taarifa za kusema ya kwamba jeshi la police limemkamata na kumpeleka Central police ni taarifa za uongo ambazo hatujui zinataka kulenga kitu gani...Taarifa sahihi ni Kwamba Mhe.Freeman Mbowe ameamua kwenda baada ya taarifa kuzagaa kuwa anatafutwa.
By Henry Kilewo
Katibu Mkoa wa Dsm
 


Habari yako kwanza umeiandika kiunafiki, pili imejaa umbea wa kike, tatu we ni fara wa kutupwa kwa kushangilia ushenzi unaoendelea Tanzania ya leo. Watawala wameanzisha chuki kubwa mabyo kidokidogo inashika inaanza kuchipua, subirini utakuja kuona mwisho wake.
 

hivi kama anahatia kulikuwa na shida gani kuandika summons na kumpelekea kama walivyofanya kwa MASOGANGE??Au kwa sababu MAsogange ni chakula ya wakubwa???Ni aibu kuona haya yanatendekea kwenye nchi ambayo Vyama vingi vimekuwepo kwa almost 20 years,na hakuna vitu kama hivi vilivyokwisha tokea.

Unadhani tunalipeleka wapi TAIFA?/Hivi Taifa ni la wanachama wa CCM tu?Basi gaweni TAIFA tujue upande huu ni CCM na upande huu ni wapinzani ianwezekana tukawa na amani kwa wale ambao tunaamini katika vyama vingi
 
Mbowe ameenda mwenyewe police acheni kuzusha mambo. Tulijua tu mlikuwa tu mnasubiri mzushe kuwa amekamatwa na police
 
endeleeni kushangilia tu, mkija kustuka bei za chakula zinapanda kila uchao na uchumi unazidi kudorola. Nchi ya Viwonder still loading
 
nishastuka watanzania tukipelekwa kwa mkemia mkuu tupimwe wote tutakutwa wachafu tu wengine washapiga pombe za kutosha na sumu sumu kibao za kuku wa kisasa da sijui asee
 
Kwa nini alikataa kujisalimisha mpaka amekamatwa. Kuna jambo analohofia?

Alitaka sheria na taratibu zifuatwe,hakuna mahali ambapo Polisi inaita watuhumiwa kwa kupitia Runinga au redio.
 
Mhe. Iddi Azani mbali na tuhuma zote aaaah! Akachukua gari lake huyoo Polisi. Akajieleza akaruhusiwa. Ukijiheshimu unaheshimiwa. Ukijishusha unainuliwa.
Mie kanikosha zaidi Gwajima.Yaani kajisafisha hahitaji hata kwenda mahakamani kudai kusafishwa.Hakuna tena anaemtaja Gwajima
 
...
.....Mkuu we kiboko umemchomoa.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…