Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

image.jpg
 
I guess Mbowe anatumia madawa ya kulevya ndo maana alikuwa anapiga chenga.Ngoja tusubiri majibu ya mkemia
 
Tundu Lissu: Mbowe amekamatwa na Jeshi la Polisi

Tumaini Makene: Mbowe amejipeleka mwenyewe Polisi

Wenye akili wanajua nani ni mkweli na nani ni propaganda
Kwahiyo akili yako imejua nin?
 
Waheshimiwa Viongozi na Wanachama wa Chadema Dar es salaam, Siku ya leo Mwenyekiti wa Chama Mhe.Freeman Mbowe akiwa Kwenye Mkoa wetu wa Dar es salaam, Ameamua kwenda Central police baada ya kuwepo na Taarifa nyingi kwenye vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuwa anahitajika Police.

Taarifa za kusema ya kwamba jeshi la police limemkamata na kumpeleka Central police ni taarifa za uongo ambazo hatujui zinataka kulenga kitu gani...Taarifa sahihi ni Kwamba Mhe.Freeman Mbowe ameamua kwenda baada ya taarifa kuzagaa kuwa anatafutwa.
By Henry Kilewo
Katibu Mkoa wa Dsm
Asa hakujua haya au alitaka publicity kwanza
 
MH MBOWE ALIENDA MWENYEWE POLICE

Propaganda za Makene hizo achana nazo .Mtu mzima akienda kujisaidia haja kubwa kichakani hujidai anaenda kuangalia kama mitego yake ya wanyama pori imenasa chochote.Hapa atakuwa alizingirwa akatoka mkuku kwenda polisi huku akiwa kashikiliwa ule mkamato wa TANGANYIKA JEKI na watoto wa kamanda SIRO
 
Kwa jinsi ulivyo andika uzi huu, bila shaka una element za Uchochezi

Hapana hawa ni kati ya wale UVCCM waliokuwa trained kwa ajili ya kufundisha watanzania tuchukiane kwa kutegemea na itikadi zetu.

Hata mbuyu ulianza kama mchicha.Vita vya Rwanda na Burundi havikuanza ghafla vilianza hivi,chuki kuwa kubwa ikashindwa kuvumilika
 
Waheshimiwa Viongozi na Wanachama wa Chadema Dar es salaam, Siku ya leo Mwenyekiti wa Chama Mhe.Freeman Mbowe ameamua kwenda Central police baada ya kuwepo na Taarifa nyingi kwenye vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuwa anahitajika Polisi kwaajili ya mahojiano.

Taarifa zinazo sambaa kwamba jeshi la polisi limemkamata na kumpeleka Central police ni taarifa za uongo ambazo hatujui zinalenga nini taarifa sahihi ni Kwamba Mhe.Freeman Mbowe ameamua kwenda baada ya taarifa kuzagaa kuwa anatafutwa, na Jeshi la Polisi,hivyo nayeye kama Kiongozi anataka kujua nini hasa jeshi hilo linahitaji.

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa.
 
Taarifa nilizopata kutoka kwenye chanzo changu cha kuaminika ni kwamba, Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE ametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi baada ya jitihada za kukimbia na kujificha kushindikana.

Mbowe amekamatwa maeneo ya Mikocheni ambako alienda kujificha ili asikamatwe na Jeshi la Polisi.

Kwa sasa wapo njiani kuelekea Central ambako atahojiwa kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya pamoja na kulisababishia usumbufu na gharama jeshi la polisi.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Mbowe amekamatwa akitolewa kwenye Appartment Moja kwenda nyingine akitumia gari Nyeusi, Tinted yenye namba za usajili T 830 DEW aina ya VX. Wamemkamata akiwa nje ya geti ya Appartment hiyo ambayo ni miongoni mwa majengo ya siri ( Safe House) yanayomilikiwa na CHADEMA

Kwa jinsi ulivyo na chuki, unafikia na ghiliba sishangai umeandika ulichoandika.

Lakini kinacho nishangaza mimi ni namna Mods wa JF wanavyokuacha na uongo wako kila uchao. Na sitashangaa impunity ikiendelea katika hili pia.

Yote tisa, kumi ni namna Cyber Crime ilivyo na double standards kwa makada.
 
Back
Top Bottom