Waheshimiwa Viongozi na Wanachama wa Chadema Dar es salaam, Siku ya leo Mwenyekiti wa Chama Mhe.Freeman Mbowe akiwa Kwenye Mkoa wetu wa Dar es salaam, Ameamua kwenda Central police baada ya kuwepo na Taarifa nyingi kwenye vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuwa anahitajika Police.
Taarifa za kusema ya kwamba jeshi la police limemkamata na kumpeleka Central police ni taarifa za uongo ambazo hatujui zinataka kulenga kitu gani...Taarifa sahihi ni Kwamba Mhe.Freeman Mbowe ameamua kwenda baada ya taarifa kuzagaa kuwa anatafutwa.
By Henry Kilewo
Katibu Mkoa wa Dsm