Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Huo ndio mtihani, kama mtego/kitendawili, katika njia mpya ya kupambana na biashara ya madawa ya kulevya.

Wangapi wanakamatwa na ushahidi lakini wanakana na kushinda kesi!

Tusubiri hatima ya Kiongozi wetu. Kama anahusika, kwa kweli atakuwa ameondoa ushahidi - kama ni ule tu wa kukutwa nao mikononi.

Usishangae kusikia amekutwa na ushahidi!!
 
Kwa style hii serikali yetu ikae tu iachane na hii vita, vita haipiganwi kwa style hii. Naona kama tunachezeshana ngonjera tu. Mtu aliye smart kitendo cha kumuita police huku akijua kosa lake huwezi mpekua nyumbani, ni asilimia 2 tu ha hiyo possibility, tena lambda kama wanatumia familia nzima.
 
Akikutwa nazo wamembambikia.
Hakuna mtu mzembe kiasi hicho.
hata kama kweli yalikuepo deki ya maana lazima imepita
Anaweza kujiamini kwamba kaficha mahala ambapo mtu mwingine hawezi kugundua ndani ya nyumba yake na hilo ndiyo linaweza kuwa kosa kubwa kwavile kunawatu mahodari sana kwa upekuzi.
 
Mungu tusamehe yaweza kuwa ulitupa laana Dah umetunyima akili kabisaaaaaaaaaa au tusubiri maisha bora yetu pepon mungu c kwa mateso haya
 
Kwenye bandiko la Lizaboni kuelezea kukamatwa kwa Mheshimiwa Freeman Mbowe Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa ameandika, "Wamemkamata akiwa nje ya geti ya Appartment hiyo ambayo ni miongoni mwa majengo ya siri ( Safe House) yanayomilikiwa na CHADEMA" Linaonekana kama ni neno la kawaida sana lakini ni aina ya maneno ya kizushi na yenye lengo maalum la kujenga uhalali wa ama "woga" au "uhalifu" wa Mbowe.

CHADEMA inamiliki "Safe House" kwenye nchi ambayo CCM kila siku wanasema ina amani, kwa nini? Lizaboni anaweza kutueleza hizo "safe House" zinamilikiwa na CHADEMA tangu lini na kwa nini CHADEMA wawe na nyumba za kujifichia? Lakini pamoja na uhuru wa kujieleza humu JF ni kweli inawezekana mtu kutoa shutuma kubwa kama hiyo kienyeji tu bila hata kujazia nyama zitakazoleta uthibitisho wa hoja yake?

Je hili la "Safe House" halifanani na lile la visu vya CUF ambavyo mpaka leo haijulikani vilikuwa vya nani na lile "Kontena" na visu hivyo lilikwenda wapi? kwa nini tunaanza kujenga taswira kwamba kwenye nchi yetu kuna watu ama wanajificha au wana nyumba za kufichama? Halafu watu wana majengo ya siri katikati ya jiji la Dar es salaam? Nikukumbushe Lizaboni, moto huanza na Cheche!!
 
Ni vizuri alivyokamatwa, wamuhoji kikamilifu na kwa kuzingatia sheria.sheria ichukue mkondo wake
Yote maisha!
Hahahahahahahaaaaaa! Chadema kwa kupindua maneno nyie! Ina maana walienda kumpekua hata kabla hajaripoti kituo cha polisi? Ina maana walipokutana naye tu njiani ndo wakamwambia haya twende nyumbani kwako tukakupekue? By the way je Mbowe anaishi Mikocheni?

Amelala selo kamada
 
Hivi inawezekana ukamshikilia mtu polisi halafu uende kufanya upekuzi kwake bila ya muhusika kuwepo

Inawezekana kabisa, chini ya sheria ya polisi ya kumweka mshukiwa/mtuhumiwa ndani.
 
Anaweza kujiamini kwamba kaficha mahala ambapo mtu mwingine hawezi kugundua ndani ya nyumba yake na hilo ndiyo linaweza kuwa kosa kubwa kwavile kunawatu mahodari sana kwa upekuzi.

Mbowe hajakamatwa kwa kuwa na viroba vya madawa ya kulevya.

Mbowe amekamatwa baada ya kukiuka amri ya polisi ya kujisalimisha ndani ya masaa 48

Mbowe anatuhumiwa kujihushisha na biashara ya madawa ya kulevya.

Lakini haimaanishi kwamba anahusika moja kwa moja ila ametajwa na walokwishakamatwa kwamba anahusika kwa namna moja ama nyingine.

Hivyo kujaribu kupata ukweli inabidi kumhoji mhusika ili kubaini ukweli.

Lakini raia anapoitwa kituoni kwa mahojiano na polisi anapaswa kutii amri hiyo na haijalishi ana cheo au wadhifa gani katika nchi yoyote ile duniani.
 
Jamani;
Hivi tujiulize swali kidogo tu. Hata kama ni nini au hata kama Kamanda wetu mkakamavu mwenye uwezo mkuu na resources zote za HQ Siro IQ yake ni kidogo vipi, ataenda kweli kuupoteza mda wake kuangalia vyumba vya Mbowe anakolala bila uhakika kuwa anajua anacho kifanya/kitafuta?? Never! Lazima atatoka na kitu. Mbowe jitayarishe una la kujibu. Time is out for yu

Haya unayoyasema (prejudice)
ndio yanafanya watu wasiwe na imani na Kamada Sirro na timu yake kwamba kweli Mbowe anatafutwa kwa ajili ya madawa ya kulevya
 
Haya unayoyasema (prejudice)
ndio yanafanya watu wasiwe na imani na Kamada Sirro na timu yake kwamba kweli Mbowe anatafutwa kwa ajili ya madawa ya kulevya

Mkuu, wewe unadhani kuna nini nyuma ya pazia, funguka mkuu.
 
Mbowe huyu aliyeita press conference? Nilisema huwezi kucheza na Serikali, hilo ni somo, wapinzani mna wakati mgumu sana kuelewa maana ya Serikali. Mtanyooka tu, mnafikiri nchi hii ni yenu peke yenu. Tupo Watanzania lukuki ambao tupo nyuma ya uongozi imara wa JPM.
siasa bana....ni mchezo mchafu sana, hasa ambapo itahusishwa na madaraka...madaraka ni matamu saana!!! binadamu huweza kujitoa ufahamu
 
Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe amerudishwa Polisi Kituo cha Kati Dar es salaam usiku huu baada ya Jeshi la Polisi kupekua nyumba zake Mikocheni na Kawe, tuhuma madawa ya kulevya
 
Mkuu, wewe unadhani kuna nini nyuma ya pazia, funguka mkuu.

Mkuu, dalili na maneno yanayosemwa yanaashiria polisi wameshajiandaa kumpata na hatia kwa gharama
yoyote. Hili linafanyika ili kumdhoofisha kisiasa .
 
Back
Top Bottom