Mkuu lengo ni kuwalaza gerezani katika kuwadhalilisha, kuwavunjia heshima hata kama kufanya hivyo ni kukiuka haki za msingi za binadamu
Tulisikia mawakili wakionywa kuwa nao 'wawekwe' mahabusu. Kwa maana kuwa hakuna tena haki ila haki ni ile inayotolewa na watu kwa matakwa yao
Swala la Mbowe lina sura inayotisha ingawa wengi hawawezi kuona tatizo
Hatuongelei kama anahusika au hahusiki, tunaongelea mazingira ya siku nyingi
1. Alitafutwa kupitia Bilicana
2. Akafuatwa na Hotel zake
Ukitazama kwa umakini kuna 'political motivations' huwezi kuwaambia watu wasiamini
Tayari kuna dots watu wanaunganisha tu. Iwe kweli au si kweli wapo wanaoamini hivyo
Kinachoendelea nchini ni kitu cha hatari sana. Hivi kwanini Polisi waende kwenye TV kutangaza wanamtafuta Mbowe.
Yaani wakipewa habari za Jambazi Nyangumi wataenda kumtaka ajisalimishe kupitia TV!
Kitendo kile tu cha Polisi kukomalia kinashaka isiyo na shaka.
Pili, Polisi wanaweza kujua alipojificha Mbowe, hawawezi kuhakiki jina walilopewa kama lina usahihi. Hapa kuna nini?
Halafu kwanini Watangaze wasiende kukusanya ushahidi na kumfikisha mahakamani?
Hivi kama kuna kitu si ameshakificha, kazi ya Polisi itakuwa nini kama hawana ushahidi
Haya tumeona matokeo yake katika nchi za wenzetu. Gambia Rais amelezimika kuondoka
Zimbwabwe mzee yupo madarakani kuliko kaburu yoyote yule aliyewahi kutawala
Mugabe na Jameh wanatishwa na siasa walizofanya huko nyuma, siasa za visasi.
Tunazidi kugawanyika na kupoteza misingi yetu ya umoja, utu na upendo
Leo Tanzania inakuwa Taifa la wananchi wanaoishi kwa kutoaminiana, hofu na kihoro
Taifa limegawanyika, misingi iliyotuweka pamoja inabomoka.
Nani ajueaye kesho itakuja na ni?