DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Naomba kujua mpango wa DAWASA kufikisha majisafi Chanika Mjini. Kumbukeni pale kuna idadi kubwa sana ya watu ambao nadhani ni advantage kwenu
 
Nmesafiri yapata miez 4 narud wiki hii kuchek bili ya maji tsh 78,780

Kazi iendelee....
 
Dawasa tunaomba mjibu maswali yetu humu,..inamaana gani kuwepo humu halafu hamjibu malalako ya watu?
 
Sioni namaba ya Kinyerezi, mana tuliomba maji watu wengi tu hapa Ukonga Sabasaba karibu na Ofisi za Serikali za mitaa karibu na reli ya kati, hadi leo kimya. Tunaomba tujulishwe kinachoendelea.
 
Hivi unit 1 ni sawa na lita ngapi za maji?

Naomba anayejua anisaidie maana nahisi wasoma meter wa dawasa ni waongo kabisa na ni wezi wakubwa.
 
Hilo sijui.
Poa mkuu Nitafatilia maana nimetumiwa bill eti nimetumia unit 70 ambayo ni = 119, 253.73 !?

Matumizi yangu ya maji huwa ni lita 3000 tu kwa mwezi ambapo mara ya mwisho kulipa nililipa 10k.

Sijawaelewa kabisa dawasa kwa hizo unit 70.
 
Maji kuja machafu kama tope
kweli tangu ljumaa ya tarehe 27 hadi 29 Januari ktk maeneo ya Kibamba na Mbezi mshikamano maji yalikuwa ya tope kabisa. Tunaomba sababu na kama maji hayo yana madhara
 
Dawasa mnachosha sana
mita yangu imeharibika miezi6 sasa ime stuck hamtengenezi mkiambiwa hamji, ila ikifik tarrehe 20 natumiwa bill unit za kutosha wakati mi mwenyewe kipindi inasoma kwa mwezi nilikua natumia unit9 sizi mnanitumia unit 15
nalalamika naambiwa inabidi nilipe ndo washugulikie la sivyo wanakata maji!! uyo msoma mita mwenyewe anakuja kunikatia maji bila maelezo yani sijalipa mwezi mmoja wa 2 natumiwa bill na kuja kukatiwa maji!!! Bongo [emoji114]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…