DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Nafikiri halmashauri/jiji/manispaa wachukue jukumu la maji DAWASA kazi imewashinda, mmejaza wezi na wavuvi tuu huko maofisini
 
DAWASA nyie ni vichaa kuanzia wafanyakazi hadi viongozi wenu haiwezekani maji hayatoki, mita haizunguki, halafu mnaleta bili kubwa
Hamjielewi
 
Sasa nimeona umuhimu wa kuwa na mwanasheria wa familia, tutapambana nao kisheria watulipe na fidia
kabisaa mana ukipambana nao hivihivi, wanakujia juu kama ndo wameumba maji
afu unasagiwa kunguni unaonekana kama wewe ndo unajua sanaa..
yani bongo wanataka ukiibiwa ukigundua unyamaze
 
Mwezi wa pili sasa KISARAWE II hakuna maji.. tukiuliza tunaambiwa pump mbovu... Dawasa mnashindwa kununua pump?
 
Mwezi wa pili sasa mita hazijasomwa kinyerezi. Wengine ni wapangaji wakihama watatuachia madeni. Naomba ofisi ya kinyerezi itusaidie katika hili. Hata kama maji yanatoka mara moja moja. Tafadhali. Bora isomwe zero unit kuliko kuvusha mwezi
 
Mashirika mengine ya umma yamebadilika isipokuwa nyie DAWASA.

Mna very funny attitude towards wateja wenu, mnawaona kama wao ndio wenye shida ya huduma, badala ya kuwa na mtazamo wa Give and Take.

TANESCO walishaacha huo ushamba, badilikeni.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866

Habari zenu wanajf
Mtendaji mkuu wa dawasa habari za jioni.
Tuna muda wa wiki tatu sasa hatuna maji kabisa hapa Goba, mm nakaa goba mitaa ya kwa morgan na week ya tatu hii hatuna maji!kikawaida hua tunapataga kwa wiki mara moja lakini kwa kipindi cha hvi karibuni tunakaa hadi wiki 3 ndo tunapata maji na kupelekea kuingia gharama za kununua maji ya kwenye malori.

Wito wangu;
Tuma timu ije ifanye uchunguzi kama kuna tatizo la miundo mbinu ya maji basi lishughulikiwe na maji yaweze kutoka. Tumsaidie Rais kwenye mambo madogodogo kama haya.

Mwnanchi wa Goba
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866

Huduma yenu upande wa Ukonga haiko sawa, unaomba kuungiwa maji huambiwi kitu kinachoendelea, hadi tuwaite kwenye kikao ndio mnachukua hatua. Tafadhali Mkuu wa Ilala fuatilia ripoti ya upatikanaji maji eneohilo ujue hali halisi ya kinachoendelea.
 
DAWASA
Mimi ni mwananchi nakaa viwanja vya benki segerea maji ni ya shida mmeweka ratiba jumanne na jumatano ila maji hayatoki, mwanzo mlisema shida n presha kuna kifaa kimeharibika toka mwaka jana maji ni ya kusua sua! Mnatuumiza sana sisi wenye familia maji ya vidumu yanatuumiza sana.
Basi tupeni namba za lile gari lenu kubwa angalau tununue kwenu maana huduma ya kawaida imeshindikana.
Kiukwel DAWASA KUTOA MAJI MNAONA KAMA NI HISANI KWETU kwamba leo mtoe kesho msitoe
Mnatuumiza wananchi
 
Hello Dawasa
Naripot uvujaji wa maji barabarani.
Eneo : Sinza D Mtaa wa Kitumbi karibu na uwanja wa magoli matatu.
Naomba ishughulikiwe ksb ni tatizo endelevu

Asante.
 
DAWASA niko Kibaha maeneo ya Chuo cha Mwalimu Nyerere.

Huku Kibaha jimbo la Mheshimiwa Koka hasa eneo hili ninaloishi tuna shida kubwa sana ya maji.

Binafsi hapa tokea siku ya sensa maji yametoka mara mbili tu.

Maisha yamekuwa magumu.

Visima vimekauka.

Watoto hasa wa kike wanapotoka shule jioni ndo wanaanza kutafuta maji.

Mpaka giza linaingia watoto wanasumbuka kutafuta maji, mmeamua kuacha hata ulinzi wa watoto.

Maeneo yanayotuzunguka maji yapo shida ni hapa tu.

Naomba pia mwenye namba ya waziri mwenye dhamana ya maji aiweke hapa, pengine atasikia kilio chetu.
 
Hivi shida ya maji kutokutoka katika maeneo kadhaa hapa mjini hasa Kata ya Saranga ni nini? Maeneo hayo ni Kimara na mitaa yake kama Stop Over, Bwawani, Mji mpya, Matairini na mitaa mingine mingi. Pamoja na Dawasco au DAWASA kutoa taarifa ya ukosefu wa maji lakini haijalenga maeneo tajwa hapo juu.
 
DAWASA
Mimi ni mwananchi nakaa viwanja vya benki segerea maji ni ya shida mmeweka ratiba jumanne na jumatano ila maji hayatoki, mwanzo mlisema shida n presha kuna kifaa kimeharibika toka mwaka jana maji ni ya kusua sua! Mnatuumiza sana sisi wenye familia maji ya vidumu yanatuumiza sana.
Basi tupeni namba za lile gari lenu kubwa angalau tununue kwenu maana huduma ya kawaida imeshindikana.
Kiukwel DAWASA KUTOA MAJI MNAONA KAMA NI HISANI KWETU kwamba leo mtoe kesho msitoe
Mnatuumiza wananchi
Hicho kifaa gani kimeharibika hadi washindwe kukitolea pesa. Mama yenu anagawa pesa hovyo huku uturuki mara kwenye mechi za mpira huku watu wanakosa maji sababu ya kifaa ambacho hata hakijulikani kuwa kimeharibika.
 
DAWASA niko Kibaha maeneo ya Chuo cha Mwalimu Nyerere.

Huku Kibaha jimbo la Mheshimiwa Koka hasa eneo hili ninaloishi tuna shida kubwa sana ya maji.

Binafsi hapa tokea siku ya sensa maji yametoka mara mbili tu.

Maisha yamekuwa magumu.

Visima vimekauka.

Watoto hasa wa kike wanapotoka shule jioni ndo wanaanza kutafuta maji.

Mpaka giza linaingia watoto wanasumbuka kutafuta maji, mmeamua kuacha hata ulinzi wa watoto.

Maeneo yanayotuzunguka maji yapo shida ni hapa tu.

Naomba pia mwenye namba ya waziri mwenye dhamana ya maji aiweke hapa, pengine atasikia kilio chetu.
Yupo zake marekanj huko anakula keki na mzee wa msoga. Haujaona mtandaoni picha wakilishana keki.
 
Huku Mitaa ya SAQWARE. VUMILIA - Tegeta A, Connections mpya mlizoachia Maji Juzi, nyingi zinamwaga Maji Mitaani tangu Juzi mpk leo hii
 
Huduma yenu upande wa Ukonga haiko sawa, unaomba kuungiwa maji huambiwi kitu kinachoendelea, hadi tuwaite kwenye kikao ndio mnachukua hatua. Tafadhali Mkuu wa Ilala fuatilia ripoti ya upatikanaji maji eneohilo ujue hali halisi ya kinachoendelea.
DAwasa kibaha namba ya simu waliyoweka hapa imefungiwa hivyo wanamaana gani kuweka namba ambayo hapatikani?
 
Back
Top Bottom