DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)
Hizo namba zenu hampokei,Nina tatizo toka wiki iliyopita nimeripoti pale kinondoni naambiwa nenda mafundi wanakuja hawaji na napewa namba za mafundi ambazo hazipatikani mna matatizo Sana. Tatizo langu baada ya kufunga meter zenu mypya bili imekuja kubwa Mara Tatu nilivyokuwa nalipa kuchunguza Kuna Bomba mafundi hawakufunga vizuri linamwaga maji nimeripoti wala hamji muone tatizo badlands yake naambulia msg za vitisho za kukatiwa maji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tunaomba account namba yako tuweze kushughulikia
 
Dwasco kwa kweli hamtutendei haki ni kwanini mmewaunganishia wakazi wa kwembe vijijini kule malamba mawili hamkufika. na kuna tetesi ya kuwa sisis wa kwembe mpakani tunahesabiwa kuwa maji yameshaunganishwa kote. tunataka kujua ilikuwaje mkaunganisha maji wachache na wengine tumekosa kuunganishiwa. taafadhari sisi sote tunahitaj huduma na sio kutubagua
 
Nyie DAWASCO,mnatuletea maji lini hapa Kimara Melenia? Tumekuja hapo Mara kadhaa mnatupiga danadana.
Halafu watendaji wenu hapo kimara wanazungusha watu na kushawish wapewe rushwa.
Hebu liangalieni hili,tutawalipua soon,tuleteeni maji.wengine tuliambiwa tulipie 76 elf ,tumefanyahivyo lkn wapi mpaka sasa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maji yanakatika sana kwa wiki ayaweza toka mara 3 usiku tu au mara 1 asubuhi mwezi sasa,mna nini?
Wapi huko? Huku kwetu tabata mwananchi maji yapo tatizo mabomba yanavuja kila mara na mafundi wameshindwa maana wakiziba leo kesho panavuja pale palipozibwa jana.

Yaani hadi mito imejaa maji ya bomba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Milima sio ishu. Mwanza kuna milima mikubwa lakini maji mpaka juu kilimani na yanatoka kila siku na cha kushangaza Mwanza uwezi kukuta Mabomba yamepasuka pasuka kama Dar es salaam tatizo menejimenti ya Dawasco imekaa kirushwa Rushwa tuu ndio maana Mh. Raisi alisema yule Mtalemwa wa Dawasco ajistaafishe mwenyewe pasipo serikali kumlazimisha kustaafu. Lakini nashangaaa kimiya mpaka Leo inamaana kaleta ukaidi kwa Mh. Raisi.

Aliaambiwa ajistaafishe mwenyewe amefanya kazi tokea Magufuli yupo Sekondari mpaka Leo hiii mzee hataki kuachia ofisi
Huyo alisha staafu. Punguza chuki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

TABATA KISUKURU KITONGOJI CHA MIGOMBANI, ENEO LA KILIMANJARO BAR MPAKA SASA BADO TUNAPIGWA DANADANA LICHA YA KUBADILISHIWA MITA, MAJI HAYAJATOKA, MARA TUNAAMBIWA ANASHUGHULIKIA OBEID, AKIPATIKANA OBEID ANASEMA TUMTAFUTE MAKELELE TUKO NJIA PANDA ILI HALI MAENEO JIRANI YOTE MAJI YANATOKA
 
Mnafanya Kazi ' Kihuni ' sana kwani tokea jana Saa 5 asubuhi hadi muda huu naandika huu uzi maeneo mengi ya Kinondoni hayana maji na kibaya zaidi ' ukataji ' huu wa maji umekuja bila taarifa yoyote ile hasa ya katika Radio au Tv na sina uhakika kama hata katika ' Mtandaoni ' wenu mlitoa taarifa yoyote ya ' Katizo ' la Maji.

Hivi ni kwanini mmetutesa hivi lakini? Wana Kinondoni tumewakosea nini? Kiliwashinda nini kututaarifu tu mapema ili tuweze kujipanga mapema na tusije pata hii shida? Kwahiyo mmetukatia haya maji ili tukaoge na kujisaidia baharini au?

Hakuna taasisi ambayo nilikuwa naiheshimu nchini kama DAWASCO ila kwa ' Upuuzi / Upupu ' wenu huu sasa nimeanza ' Kuwadharau ' na mmetukera Watu wengi sana wa pande hizi za Kinondoni.

DAWASCO Kinondoni hali ni mbaya jamani hebu turudishieni basi haraka hayo maji wengine tukaoge na tukajisaidie kwa amani na uhakika kwani kwa hali ilivyo sasa kama hamtayarudisha hayo maji basi eneo lote la Kinondoni litakuwa na harufu isiyo na utofauti wowote na ile inayosikika maeneo ya dampo.

Nawasilisha.
 
Hii kero kubwa sana, mpaka sasa hivi, hakieleweki
 
na wana matangazo yao humu... lakini hawaendani na huduma wanayo itoa
 
Njoo nikuuzie maji ww na majirani zako ya kisima safi kabisa mm dawasco nishawasahau zamani sanaaa

Argue don't shout
 
na wana matangazo yao humu... lakini hawaendani na huduma wanayo itoa

Na usishangae hata Meneja wao sasa hivi ' ameunyuti ' tu huku ' akiukodolea ' huu uzi bila hofu yoyote huku akikuna tu Kitambi chake.
 
Mkuu nataka kwenda ' Kuyashusha ' sasa lakini kila nikiwaza DAWASCO walichotufanyia yenyewe yanarudi ' Kunako '.
Hahahaha vumilia tu, maji muhimu sana,

Hawa DAWASCO wanachofanya sio kabisa, utashangaa na Siku ya Leo inapita tena
 
Back
Top Bottom