DAWASCO Kimara fungueni Maji, Hali ni Mbaya

DAWASCO Kimara fungueni Maji, Hali ni Mbaya

Uko ushuani wee lol, ngoja na mie nipambane niishi huko.
Hata si ushuani mdogo wangu..uswazi vibaya mno..Ni vile tu tulijiongeza kuchimba visima vya kata ..maji hayakatiki hata iweje
 
Sie huku tunachota maji direct kwenye bomba
Kwa mwaka yanakatika Mara moja tu
Au sababu tuko karibu nao?
 
Habari wanabodi, kama Kuna mtu anamfaham Meneja wa Dawasco Kimara, tafadhali amjulishe kuwa afungue maji mchana huu kwani Hali huku mtaani ni Mbaya Sana. Siku ya 4 leo inaenda maji hakuna, na hata watu wanaouza toka kwenye matanki yao wameishiwa maji, hivyo, Hali sio ya mchezo kabisa.

Kuna Ndugu yangu anaishi hapa Nyuma ya Ukuta Wa Dawasco Kimara, anasema yaani Mtaa Mzima hakuna mwenye akiba ya Maji ndani. Watu wameshindwa kufua wikend hii kisa hakuna maji.

Kama huu ni uzembe wa Mtu fulani nashauri Waziri wa Maji amtumbue mapema Ili wezembe wengine wajifunze pia. Hali zipoje maeneo mengine Dar leo kuhusu maji
Sehemu kubwa ya DSM hakuna maji
 
Mtambo umezima toka tar 21 wanasema eti umezima jama marayaa hawaa
 
Kwa nchi za wenzetu hii ni tatizo tosha kwa Waziri wa Maji, anatakiwa awajibike.Ujue madhara ya kukosa maji Siku 4 mfululizo Lina madhara makubwa Sana kiafya. Mojawapo ni huweza kuchochea mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu,homa ya matumbo na kuharisha, hii ni kwa sababu watu wameanza kuokoteza maji huko vizimani na hakuna ajuaye usafi na usalama wake. Bora Ukatike umeme majumbani ila sio maji.
 
Habari wanabodi, kama Kuna mtu anamfaham Meneja wa Dawasco Kimara, tafadhali amjulishe kuwa afungue maji mchana huu kwani Hali huku mtaani ni Mbaya Sana. Siku ya 4 leo inaenda maji hakuna, na hata watu wanaouza toka kwenye matanki yao wameishiwa maji, hivyo, Hali sio ya mchezo kabisa.

Kuna Ndugu yangu anaishi hapa Nyuma ya Ukuta Wa Dawasco Kimara, anasema yaani Mtaa Mzima hakuna mwenye akiba ya Maji ndani. Watu wameshindwa kufua wikend hii kisa hakuna maji.

Kama huu ni uzembe wa Mtu fulani nashauri Waziri wa Maji amtumbue mapema Ili wezembe wengine wajifunze pia. Hali zipoje maeneo mengine Dar leo kuhusu maji
Tulieni nyie si ndiyo mlipigia upinzani kura kisa mmevunjiwa nyumba zenu. Tulieni hivyo hivyo dawa iwaingie
 
Back
Top Bottom