DC aingilia kati mgogoro wa Wananchi na Luhaga Mpina mkoani Morogoro

MKUU wa Wilaya ya Morogoro,Rebeca Nsemwa,amejikuta akipokelewa na Mabango pamoja na vilio kutoka kwa wananchi wa Vijiji vya Dalla tarafa ya Bwakira na Mbwade tarafa ya Mvuha katika Halmashauri ya wilaya ya Morogoro wakishinikiza kurudishiwa ardhi yao ekari zaidi ya 1000 zinazodaiwa kuchukuliwa bila kufuata utaratibu na aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina.

Wananchi waliokusanya katika kijiji cha Dalla walisimamisha msafara wa Mkuu wa wilaya hiyo na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ukiwa njiani kuelekea kwenye mkutano na wananchi wa vijiji vitatu vya Dalla,Kongwa na Mbwade kwa lengo la kusikiliza kero zinazowakabili.

Wananchi hao wakiwa na mabango hayo yaliyobeba ujumbe mbalimbali ikiwemo kumuomba Rais Dk Samia Suluhu Hassan kusikia kilio chao kuhusu kudhulumiwa ardhi yao na Waziri huyo wa zamani Mpina.

Akiwasilisha kero hiyo kwa mkuu wa wilaya hiyo,Consolata Mchuma,awali wakati akiwa mjumbe wa Serikali ya kijiji cha Dalla,wananchi waliteseka kwa zaidi ya miaka nane iliyopita kuhusiana na tatizo hilo la kuchukuliwa kwa ardhi yao .

Alisema baada ya kutangaziwa na Serikali ya kijiji kupatikana kwa mwekezaji Mpina walikubali kumpa ekari 300 kwa kukubaliana kila ekari atatoa kiasi cha shilingi 5000 kwa mwaka huku akitakiwa kujenga madarasa manne ikiwemo mawili shule ya msingi Dalla na mawili shule ya msingi Kilengezi pamoja na kuendelea kulima lakini mpaka sasa hajatekeleza makubaliano hayo.

Alisema mwaka 2016 akiwa mjumbe wa serikali ya kijiji hicho,Mpina alileta barua ya kutaka kuongozewa eneo lingine la ekari 700 lakini wanakijiji walikataa kuongezea eneo lingine huku wakimtaka afike ofisini ili atekeleze ahadi yake lakini aliendelea kukahidi.

Alisema baadae alitwaa hilo eneo kwa madai kwamba amelinunua jambo ambalo hajahusisha kwenye mkutano wa kijiji wala kuhizinishiwa na muktasari wa kuridhiwa na wana kijiji.

Naye Diwani Mstaafu wa tarafa ya Mvuha,Marrystela Chamlungo,akiongea huku akibubujikwa na machozi,alisema pamoja na Mpina kuchuku eneo hilo lakini alidiliki kupitisha greda kwenye mazao yao na kuwasababishia hasara na alipoitwa kwaajili ya kulipa fidia aligoma kutekeleza.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Mbwade,Salumu Malozo alisema mwekezaji Mpina,amemega eneo katika vijiji vitatu vya Mbwade,Kongwa na Dalla na kusababisha kuwepo kwa mgogoro wa wananchi wa vijiji hivyo.

Diwani wa kata Mvua Mfaume Amani,alisema wakati anaingia madarakani mwaka 2015 alikuta huo mgogoro ulionza mwaka 2009 na sula hilo lilifikia kwenye vikao mbalimbali ikiwemo cha Halmashauri kwaajili ya kurudishwa kwa eneo hilo lilochukuliwa na Mpina kwakuwa taratibu hazijafuatwa.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya wilaya ya Morogoro,Halima Mtawazo alisema mwekezaji huyo alizungumza na halmashauri ya kijiji ya wajumbe 25 na kwamba maombi yake hayakukamilika kwakuwa wajumbe hao hawakuitisha mkutano wa kijiji ili kufanya uhamuzi wa kuidhinisha au kukataa kwahiyo hakumaliza taratibu zinazotakiwa.

Baada ya kusikiliza hoja mbalimbali za wananchi kuhusina na mgogoro huo,Mkuu wa wilaya Nsemwa alifikia kutoa maamuzi ya kuundwa kwa timu ya watalaam itakayopitia nyaraka za pande zote pamoja na kupima eneo shamba hilo ili kubaini ukubwa wake pamoja na kuhanisha mipaka.

Mkuu huyo wa wilaya alisema lengo la timu iliyopewa muda wa siku 14 ni kubaini uhalali wa nyaraka na upimaji wa mipaka ili kila upande uweze kupata haki yake kwenye vijiji hivyo.

Alimtaka mwekezaji Mpina kutoa ushirikiano kwa timu hiyo iliyoundwa ili kuweza kumaliza mgogoro na kuwawezesha wananchi kuendelea kushiriki katika shughuli za kilimo kwenye eneo hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu kuhusina na mgogoro huo Mpina,alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwakuwa tayari lipo tayari kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo ya Morogoro vijijini.
View attachment 2639715View attachment 2639716View attachment 2639718View attachment 2639720View attachment 2639724View attachment 2639726View attachment 2639727
Si mlisema hamtwki Mabango hayo ya nini.
 
Huyo DC awe makini Saisa anazozofanya yeye zilifanywa na kina sabaya na makonda awamu ya Tano na wote wameishia kubaya
 
Niliangalia hii taarifa kupitia ITV ukiwa na akili timamu unajua bila shaka wale wananchi wamepangwa ila sijui ni kwa kusufio gani pengine ni vile Mpina anavyowapelekea moto huko bungeni.
 
hao wananchi wanafanya utapeli tu hapo.ninachojua mpina ni lazima alifuata taratibu za kununua eneo hilo.hiyo drama ya wananchi ni kutaka kumpoka eneo hilo kwa njia ovu,na ni siasa za kipuuzi sana hizo na zikiachwa ziendelee zitaleta mtafaruku kwa wengine.mashamba wauze wao iweje leo wamgeuka au sababu leo siyo waziri au sababu amekuwa anaichalenji serikali.hizo ni ssiasa za kuharibiana hazina afya ndani ya nchi hii.
 
Yaani mabango yote yameandikwa na mtu mmoja, tena yote kwa aina moja ya boksi kutoka kwa duka la Mang, na black marker pen.

Wamewadharirisha wananchi hakika. Hata kama hoja ni ya kweli, hiyo sio approach ya hao wanaoonekana kwa picha.
Dah unatisha aisee
 
Acha upumbavu. Mabango aandike mtu mmoja halafu uwabebeshe wapumbavu kumi!!? Wewe unaona ni sawa hiyo? Au hujui kwanini iwe Mpina na wala siyo Wahuni?
Hata kama kaandika mtu mmoja kwani Kuna shida gani? Kuna ulazima gani mabango yaandikwe na watu tofauti tofauti?

By the way wewe unaona Sawa kiongozi kuwa na hekari 1000? Alafu kila siku anapiga kelele bungeni kupinga ufisadi
 
MKUU wa Wilaya ya Morogoro,Rebeca Nsemwa,amejikuta akipokelewa na Mabango pamoja na vilio kutoka kwa wananchi wa Vijiji vya Dalla tarafa ya Bwakira na Mbwade tarafa ya Mvuha katika Halmashauri ya wilaya ya Morogoro wakishinikiza kurudishiwa ardhi yao ekari zaidi ya 1000 zinazodaiwa kuchukuliwa bila kufuata utaratibu na aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina.

Wananchi waliokusanya katika kijiji cha Dalla walisimamisha msafara wa Mkuu wa wilaya hiyo na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ukiwa njiani kuelekea kwenye mkutano na wananchi wa vijiji vitatu vya Dalla,Kongwa na Mbwade kwa lengo la kusikiliza kero zinazowakabili.

Wananchi hao wakiwa na mabango hayo yaliyobeba ujumbe mbalimbali ikiwemo kumuomba Rais Dk Samia Suluhu Hassan kusikia kilio chao kuhusu kudhulumiwa ardhi yao na Waziri huyo wa zamani Mpina.

Akiwasilisha kero hiyo kwa mkuu wa wilaya hiyo,Consolata Mchuma,awali wakati akiwa mjumbe wa Serikali ya kijiji cha Dalla,wananchi waliteseka kwa zaidi ya miaka nane iliyopita kuhusiana na tatizo hilo la kuchukuliwa kwa ardhi yao .

Alisema baada ya kutangaziwa na Serikali ya kijiji kupatikana kwa mwekezaji Mpina walikubali kumpa ekari 300 kwa kukubaliana kila ekari atatoa kiasi cha shilingi 5000 kwa mwaka huku akitakiwa kujenga madarasa manne ikiwemo mawili shule ya msingi Dalla na mawili shule ya msingi Kilengezi pamoja na kuendelea kulima lakini mpaka sasa hajatekeleza makubaliano hayo.

Alisema mwaka 2016 akiwa mjumbe wa serikali ya kijiji hicho,Mpina alileta barua ya kutaka kuongozewa eneo lingine la ekari 700 lakini wanakijiji walikataa kuongezea eneo lingine huku wakimtaka afike ofisini ili atekeleze ahadi yake lakini aliendelea kukahidi.

Alisema baadae alitwaa hilo eneo kwa madai kwamba amelinunua jambo ambalo hajahusisha kwenye mkutano wa kijiji wala kuhizinishiwa na muktasari wa kuridhiwa na wana kijiji.

Naye Diwani Mstaafu wa tarafa ya Mvuha,Marrystela Chamlungo,akiongea huku akibubujikwa na machozi,alisema pamoja na Mpina kuchuku eneo hilo lakini alidiliki kupitisha greda kwenye mazao yao na kuwasababishia hasara na alipoitwa kwaajili ya kulipa fidia aligoma kutekeleza.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Mbwade,Salumu Malozo alisema mwekezaji Mpina,amemega eneo katika vijiji vitatu vya Mbwade,Kongwa na Dalla na kusababisha kuwepo kwa mgogoro wa wananchi wa vijiji hivyo.

Diwani wa kata Mvua Mfaume Amani,alisema wakati anaingia madarakani mwaka 2015 alikuta huo mgogoro ulionza mwaka 2009 na sula hilo lilifikia kwenye vikao mbalimbali ikiwemo cha Halmashauri kwaajili ya kurudishwa kwa eneo hilo lilochukuliwa na Mpina kwakuwa taratibu hazijafuatwa.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya wilaya ya Morogoro,Halima Mtawazo alisema mwekezaji huyo alizungumza na halmashauri ya kijiji ya wajumbe 25 na kwamba maombi yake hayakukamilika kwakuwa wajumbe hao hawakuitisha mkutano wa kijiji ili kufanya uhamuzi wa kuidhinisha au kukataa kwahiyo hakumaliza taratibu zinazotakiwa.

Baada ya kusikiliza hoja mbalimbali za wananchi kuhusina na mgogoro huo,Mkuu wa wilaya Nsemwa alifikia kutoa maamuzi ya kuundwa kwa timu ya watalaam itakayopitia nyaraka za pande zote pamoja na kupima eneo shamba hilo ili kubaini ukubwa wake pamoja na kuhanisha mipaka.

Mkuu huyo wa wilaya alisema lengo la timu iliyopewa muda wa siku 14 ni kubaini uhalali wa nyaraka na upimaji wa mipaka ili kila upande uweze kupata haki yake kwenye vijiji hivyo.

Alimtaka mwekezaji Mpina kutoa ushirikiano kwa timu hiyo iliyoundwa ili kuweza kumaliza mgogoro na kuwawezesha wananchi kuendelea kushiriki katika shughuli za kilimo kwenye eneo hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu kuhusina na mgogoro huo Mpina,alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwakuwa tayari lipo tayari kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo ya Morogoro vijijini.
View attachment 2639715View attachment 2639716View attachment 2639718View attachment 2639720View attachment 2639724View attachment 2639726View attachment 2639727
Hao wanakijiji ni wajinga sana walikuwa na mamlaka gani ya kumpa mtu ekari 300 wakati sheria inawataka isizidi ekari 50? Hao wanakijiji wanatakiwa washitakiwe kwa ubadhirifu wa mali za umma. Hao wananchi wametumwa na mawaziri wanaokosolewa sana na Mpina ambao ni nishati, kilimo, mifugo, ujenzi na fedha ndio wako nyuma yao ila ukweli utajulikana tu maana watasalitiana kisha wataweka peupe kila kitu hata huyo mkuu wa wilaya sijui ni kitu gani alikipanga na hao watu wachache walipopangwa kwa makusudi.

Kama hao wananchi ni wa kweli waseme pia ni viongozi gani waliojimilikisha mashamba makubwa huko Mvomero na Kilosa ambao wako madarakani sasa hivi lakini wanakaliwa kimya wakati ardhi imeporwa kwa kutumia vyeo walivyo navyo?
 
Namsihi awe mwangalifu.Asije akawa anachagiza bila kujua siasa za bungeni.
 
Hata kama kaandika mtu mmoja kwani Kuna shida gani? Kuna ulazima gani mabango yaandikwe na watu tofauti tofauti?

By the way wewe unaona Sawa kiongozi kuwa na hekari 1000? Alafu kila siku anapiga kelele bungeni kupinga ufisadi
Shida iko wapi kiongozi kuwa na ekari hizo iwapo anazimiliki kihalali?
 
Ukiwa unaropoka mambo ya Ufisadi haswa kwa hawa Ccm ,Hakikisha nawewe umsafi Kweli Kweli!!Pole sana Mpina japo najua uropokaji wako haukuwa kwalengo la uzalendo Bali Manufaa binafsi na lile genge lenu.
 
Hayo maeneo yana rutuba mno ukipata ardhi walau hekari 5 za pamoja umetoboa kama wewe ni mpambanaji wa kweli ndizi mzuzu ile laini ina mea hatari sana maeneo hayo.
 
Mwana kulitak mwana kulipata
Sukuma gang watakwambia izo ni hujuma kwa mpina ila ukwel ni kwamba serikal ya jiwe ilikua ya kifisadi, uzurumati, utapeli na baya zaid ilkua ya kiuaji
 
Back
Top Bottom