DC aingilia kati mgogoro wa Wananchi na Luhaga Mpina mkoani Morogoro

DC aingilia kati mgogoro wa Wananchi na Luhaga Mpina mkoani Morogoro

Simple Mpina aachane na hilo shamba then tuone wataanza movie gani, awapige humo humo

..akianza kupoteza mali familia itamlilia na mwisho atasallimu amri.

..moja ya sababu iliyomrudisha Sumaye Ccm ni kilio na lawama za familia kuhusu mali allizonyang'anywa kwasabau ya kuwa mpinzani.
 
Waziri wa Nishati, Januari Makamba na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba hawahusiki kufadhili fedha kwa ajili ya mpango huo wa kumchafua Mpina.

Hata kama Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ni NDUGU YAKE NA FESTO SANGA ambaye ni MSAIDIZI wa MWIGULU NCHEMBA lakini mh mwigulu hahusiki na kuratibu suala hilo kwani yuko bize kuandaa bajeti kuu ya serikali na mh Makamba naye yuko bize na kuandaa bajeti yake kesho bungeni.

"hizo tuhuma kwamba Mwigulu na Makamba ndio wamefadhili huo mkutano wa kumchafua mpina sio wa kweli na vyombo vipo vinaweza kuchunguza kujua ukweli wa jambo hilo, hiyo ni ziara ya kawaida ya mkuu wa wilaya ya morogoro kusikiliza kero za wananchi" amesema mmoja wa watu wa karibu wa makamba na mwigulu.

Baada ya taarifa hiyo kutoka kwenye vyombo vya habari watanzania wengi waliihusisha na mambo ya kisiasa na kuwayaja mwigulu nchemba na makamba kuwa ndio wametoa pesa nyingi kulipa waandishi wa habari na kuwalipa watu wa kuongea kwenye mkutano.
 
..akianza kupoteza mali familia itamlilia na mwisho atasallimu amri.

..moja ya sababu iliyomrudisha Sumaye Ccm ni kilio na lawama za familia kuhusu mali allizonyang'anywa kwasabau ya kuwa mpinzani.
System imekamatwa na mafisadi hakuna namna
 
Waziri wa Nishati, Januari Makamba na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba hawahusiki kufadhili fedha kwa ajili ya mpango huo wa kumchafua Mpina.

Hata kama Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ni NDUGU YAKE NA FESTO SANGA ambaye ni MSAIDIZI wa MWIGULU NCHEMBA lakini mh mwigulu hahusiki na kuratibu suala hilo kwani yuko bize kuandaa bajeti kuu ya serikali na mh Makamba naye yuko bize na kuandaa bajeti yake kesho bungeni.

"hizo tuhuma kwamba Mwigulu na Makamba ndio wamefadhili huo mkutano wa kumchafua mpina sio wa kweli na vyombo vipo vinaweza kuchunguza kujua ukweli wa jambo hilo, hiyo ni ziara ya kawaida ya mkuu wa wilaya ya morogoro kusikiliza kero za wananchi" amesema mmoja wa watu wa karibu wa makamba na mwigulu.

Baada ya taarifa hiyo kutoka kwenye vyombo vya habari watanzania wengi waliihusisha na mambo ya kisiasa na kuwayaja mwigulu nchemba na makamba kuwa ndio wametoa pesa nyingi kulipa waandishi wa habari na kuwalipa watu wa kuongea kwenye mkutano.
😂😂😂

Umehojiwa na nani?
 
Acha upumbavu. Mabango aandike mtu mmoja halafu uwabebeshe wapumbavu kumi!!? Wewe unaona ni sawa hiyo? Au hujui kwanini iwe Mpina na wala siyo Wahuni?
Kinyeo chako
 
Huyo DC awe makini Saisa anazozofanya yeye zilifanywa na kina sabaya na makonda awamu ya Tano na wote wameishia kubaya
usilinganishe majambazi na mama wa watu anayetimiza wajibu wake, hapo amekosea nini yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya hiyo wilaya
 
Niliangalia hii taarifa kupitia ITV ukiwa na akili timamu unajua bila shaka wale wananchi wamepangwa ila sijui ni kwa kusufio gani pengine ni vile Mpina anavyowapelekea moto huko bungeni.
wapangwe wa nini, Mpina hana ubavu wa kuipelekesha serikali yule ni fisadi tu waxha ashughulikiwe hana akili
 
MKUU wa Wilaya ya Morogoro,Rebeca Nsemwa,amejikuta akipokelewa na Mabango pamoja na vilio kutoka kwa wananchi wa Vijiji vya Dalla tarafa ya Bwakira na Mbwade tarafa ya Mvuha katika Halmashauri ya wilaya ya Morogoro wakishinikiza kurudishiwa ardhi yao ekari zaidi ya 1000 zinazodaiwa kuchukuliwa bila kufuata utaratibu na aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina.

Wananchi waliokusanya katika kijiji cha Dalla walisimamisha msafara wa Mkuu wa wilaya hiyo na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ukiwa njiani kuelekea kwenye mkutano na wananchi wa vijiji vitatu vya Dalla,Kongwa na Mbwade kwa lengo la kusikiliza kero zinazowakabili.

Wananchi hao wakiwa na mabango hayo yaliyobeba ujumbe mbalimbali ikiwemo kumuomba Rais Dk Samia Suluhu Hassan kusikia kilio chao kuhusu kudhulumiwa ardhi yao na Waziri huyo wa zamani Mpina.

Akiwasilisha kero hiyo kwa mkuu wa wilaya hiyo,Consolata Mchuma,awali wakati akiwa mjumbe wa Serikali ya kijiji cha Dalla,wananchi waliteseka kwa zaidi ya miaka nane iliyopita kuhusiana na tatizo hilo la kuchukuliwa kwa ardhi yao .

Alisema baada ya kutangaziwa na Serikali ya kijiji kupatikana kwa mwekezaji Mpina walikubali kumpa ekari 300 kwa kukubaliana kila ekari atatoa kiasi cha shilingi 5000 kwa mwaka huku akitakiwa kujenga madarasa manne ikiwemo mawili shule ya msingi Dalla na mawili shule ya msingi Kilengezi pamoja na kuendelea kulima lakini mpaka sasa hajatekeleza makubaliano hayo.

Alisema mwaka 2016 akiwa mjumbe wa serikali ya kijiji hicho,Mpina alileta barua ya kutaka kuongozewa eneo lingine la ekari 700 lakini wanakijiji walikataa kuongezea eneo lingine huku wakimtaka afike ofisini ili atekeleze ahadi yake lakini aliendelea kukahidi.

Alisema baadae alitwaa hilo eneo kwa madai kwamba amelinunua jambo ambalo hajahusisha kwenye mkutano wa kijiji wala kuhizinishiwa na muktasari wa kuridhiwa na wana kijiji.

Naye Diwani Mstaafu wa tarafa ya Mvuha,Marrystela Chamlungo,akiongea huku akibubujikwa na machozi,alisema pamoja na Mpina kuchuku eneo hilo lakini alidiliki kupitisha greda kwenye mazao yao na kuwasababishia hasara na alipoitwa kwaajili ya kulipa fidia aligoma kutekeleza.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Mbwade,Salumu Malozo alisema mwekezaji Mpina,amemega eneo katika vijiji vitatu vya Mbwade,Kongwa na Dalla na kusababisha kuwepo kwa mgogoro wa wananchi wa vijiji hivyo.

Diwani wa kata Mvua Mfaume Amani,alisema wakati anaingia madarakani mwaka 2015 alikuta huo mgogoro ulionza mwaka 2009 na sula hilo lilifikia kwenye vikao mbalimbali ikiwemo cha Halmashauri kwaajili ya kurudishwa kwa eneo hilo lilochukuliwa na Mpina kwakuwa taratibu hazijafuatwa.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya wilaya ya Morogoro,Halima Mtawazo alisema mwekezaji huyo alizungumza na halmashauri ya kijiji ya wajumbe 25 na kwamba maombi yake hayakukamilika kwakuwa wajumbe hao hawakuitisha mkutano wa kijiji ili kufanya uhamuzi wa kuidhinisha au kukataa kwahiyo hakumaliza taratibu zinazotakiwa.

Baada ya kusikiliza hoja mbalimbali za wananchi kuhusina na mgogoro huo,Mkuu wa wilaya Nsemwa alifikia kutoa maamuzi ya kuundwa kwa timu ya watalaam itakayopitia nyaraka za pande zote pamoja na kupima eneo shamba hilo ili kubaini ukubwa wake pamoja na kuhanisha mipaka.

Mkuu huyo wa wilaya alisema lengo la timu iliyopewa muda wa siku 14 ni kubaini uhalali wa nyaraka na upimaji wa mipaka ili kila upande uweze kupata haki yake kwenye vijiji hivyo.

Alimtaka mwekezaji Mpina kutoa ushirikiano kwa timu hiyo iliyoundwa ili kuweza kumaliza mgogoro na kuwawezesha wananchi kuendelea kushiriki katika shughuli za kilimo kwenye eneo hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu kuhusina na mgogoro huo Mpina,alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwakuwa tayari lipo tayari kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo ya Morogoro vijijini.
View attachment 2639715View attachment 2639716View attachment 2639718View attachment 2639720View attachment 2639724View attachment 2639726View attachment 2639727
Igizo la kipumbavu sana hili kuwahi kutokea
 
Back
Top Bottom