DC Alberto Msando akopa milioni106 benki ili kuwajengea wamachinga sehemu ya kufanyia biashara

DC Alberto Msando akopa milioni106 benki ili kuwajengea wamachinga sehemu ya kufanyia biashara

Hata siku moja usimwamini mwanasiasa.
Kama ameamua mkopo wake liwe jambo la wazi, aweke hadharani executed term loan / loan agreement tujionee kwa macho yetu.

Na pia collateral gani ameziweka ku secure huo mkopo?

Mkopo ni wa muda gani?

Kama amekuwa guaranteed na kazi yake, vipi akitenguliwa kesho?
Hiyo ni unsecured loan mkuu hata wewe unaweza kukupa kama una kazi ya maana
 
Hata siku moja usimwamini mwanasiasa.
Kama ameamua mkopo wake liwe jambo la wazi, aweke hadharani executed term loan / loan agreement tujionee kwa macho yetu.

Na pia collateral gani ameziweka ku secure huo mkopo?

Mkopo ni wa muda gani?

Kama amekuwa guaranteed na kazi yake, vipi akitenguliwa kesho?
Naam Mkuu. Wengi hili wanaliangalia juujuu na kwa wepesi sana. Je hayo mashimo atayafukiaje???
 
Tunaongelea habari ya yeye kuwasaidia wamachinga mkuu...

hiyo mambo sijui traitor, msaliti wa demokrasia, muuaji mkubwa, mkandamizaji wamachinga wa morogoro hawaijui, hata sisi wengine hatukuelewi labda uje na ushuhidi
Mimi nasubiria mtu azungumzie alivyoweka ufundi wakati akishika lichupi la msanii malaya Gigi Money
 
Hakuna benki Tanzania inakata makato makubwa hivyo, uongo mtupu.
 
Kazi ya kuteuliwa haiwezi ku secure mkopo. In case of default, Benki ita recover vipi Hilo deni?
Msando ni tajiri,halafu unsecured ni hiyo hiyo kwa watumishi ,una pledge kuachia nssf na mafao mengine yote
 
Tunaongelea habari ya yeye kuwasaidia wamachinga mkuu...

hiyo mambo sijui traitor, msaliti wa demokrasia, muuaji mkubwa, mkandamizaji wamachinga wa morogoro hawaijui, hata sisi wengine hatukuelewi labda uje na ushuhidi
Umesema Msando asitoe ushahidi kwa Bujibuji sababu Bujibuji hajulikani ni nani na hapohapo wewe unataka upewe ushahidi wa usaliti wa Msando bila kujitambulisha wewe kama nani😄😄🤣

Nchi hii bwana
 
Benki wao hawawezi kukupa nyaraka za mteja. Hizo huhifadhiwa kwenye dossier huko strong room.
Mteja ndio yeye anayeweza kuonyesha nyaraka zake. AZIWEKE HADHARANI
Ni kama mbunge kuonesha Salary Slip ya Mshahara wake bungeni. HUWA HAWATAKI (Wabunge) KABISA, yaani hata wale waliomaliza ubunge, wawe wa CCM au Upinzani nao hawataki, zinabaki porojo tu.
 
View attachment 1939573

Kinachonisikitisha Mbunge na baadhi ya Madiwani tuliowachagua wanajipanga kumkwamisha.
Wanadai maamuzi ya kukopa ni yake binafsi hivyo wao hawatahidhinisha ili hilo Deni lilipwe na Halmashauri hivyo itabidi alilipe yeye binafsi
DC hawezi kukopa kwa niaba ya halmashauri na kama alikopa hilo ni jukumu lake msimamizi mkuu wa Halmashauri/pay master ni Mkurugenzi

Yote kwa yote mtu mwenye kulipwa 3.1m hawezi kukatwa 2.8m wakati kuna kodi na makato mengine hapo hilo ni chaka
 
Kama anakatwa Tsh. 2.8 kati ya 3.1 anajikimu vipi huyu mtu? Tungekuwa na Mamlaka za Uteuzi zenye akili huyu Bwana alipaswa akamatwe ajieleze huu utopolo alioongea.. Ila hapa kwetu tusishangae akapewa u-RC kabisa.
Kwani anachanzo kimoja tu cha kujiingizia pesa?
 
Hili ni somo zuri sana kwa wale wanaowaona wamachinga kuwa tatizo na kuja na mapendekezo kwamba wafukuzwe mijini.

Hongera kwa Alberto Msando kwa uwezo wako mkubwa wa kuona tatizo sio wamachinga ila miundombinu, na hongera tena kwa kutatua tatizo badala ya kulalamika na kutumia nafasi yako kuumiza hawa raia.

Hawa ndio viongozi tunaowataka Tanzania ya sasa. Viongozi wenye uwezo wa kutatua matatizo papo kwa papo na sio kuongeza matatizo

View attachment 1939651




Wale mtakaochukizwa na hili ameweka wazi kwamba alifuata taratibu ili kuondoa manenomaneno
Mwanasiasa Akikuambia KUMEKUCHA USIMWAMINI toka Nje kaangalie

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Ninavyojua Mimi utumishi na hazina ( Lawson) hawawezi kuidhinisha makato ya zaidi 2/3 ya mshahara wa mtumishi.
Aseme analipa kwa vyanzo vingine na sio mshahara
 
Huo mradi uliibuliwa na yeye mwenyewe kwa mawazo yake au na wamachinga kwa kuzingatia mahitaji na upatikanaji wa wateja?
Kama nini yeye ndiye aliyeibua basi huo ni mradi binafsi kwa jina la machinga yeye katumia fursa tu
Kama ni mradi wa machinga hiyo ni white elephant project maana kiasili machinga hawakai sehemu moja wao wanafuata wateja wao walipo sio mteja amfuate mmachinga
 
Back
Top Bottom