DC aliyetumbuliwa atoa waraka mzito kwa Naibu Waziri mpya wa TAMISEMI

Halmashauri nyingine mpaka wakuu wana Idara wa NJAA kinoma. Sasa imagine, watumishi wa chini?
 
Alichofanya Basila sisemi ni uongo au havifanyiki ila hapa hakuwasilisha kwa naibu waziri amewasilisha kwa umma au amemsemelea naibu waziri

Sijajua kama nia yake ni kumsaidia mwananchi au kumtia hasira mwananchi!?
 
Ana hoja nzuri na yenye mashiko lakini kwa nini hakuyasema hayo yote alipokua kwenye ulaji? natamani ujasiri huo angekua nao alipokua ndani ya mfumo, lakini pia nimkumbushe tuu kwamba hapa uswahilini siku zote msema ukweli hua hapendwi aendelee na shughuli zingine za kumuingizia kipato tuu
 
Wilaya ya ubungo hasa jimbo la kibamba liko zaidi ya ICU,hakuna maji,barabara,huduma za kiafya e.t.c,huwezi amini kama jimbo la kibamba liko dar aisee
Mbunge Mtemvu amelala usingizi wa pono, hapambani kutafuta barabara za kiwango cha lami au zege, mfano kata ya kibamba ilitakiwa barabara ya dkt William Shija ijengwe walau kwa zege ila wala hakuna hata dalili, kata nzima ina kilometa zisizozidi 4 za lami, wakati pale kwa Msuguli kwenda Malamba wamejenga lami nzuri kabisa na tena wamejenga nyingine ya zege ili ikaungane na lami. Kimara Korogwe wana barabara ya zege sasa madaladala yanapita huko, kibamba diwani kalala yoo..hakuna maendeleo.
 
Unaiaibisha Liverpool kwa mawazo fyongo kama haya.
Unawezaje kuona kuwa kuiba ni haki ya mtumishi?
Kama huwezi kufanya kazi bila kuiba ni afadhali uache kazi uende huko mtaani ukaibe vizuri.
Eti tena unamalizia na 'YNWA', umeniudhi kweli, ingekuwa ni zile enzi zetu ningekutukana vibaya sana. Huwezi kui-identify Liverpool fc, timu bora zaidi kuwahi kutokea England, na mawazo ya ujizi. Koma kavisa.
Tena ubadili na hiyo ID yako!
 
Huyu nae analia Lia mno,sasa DC na wewe unalia Lia,unashindwa kufanya maamuzi,ni ujinga kwenda kwenye kadamnasi na vyombo vya habari ukaanza kulalamika kuhusu wakurugenzi wanavyokukwamisha,sasa unataka wananchi wafsnye nini?ile haikuwa platform ya kufikisha Malalamiko yake,ilibidi amwandikie Raisi,au waziri mkuu,au waziri wa tamisemi sio kulia Lia mbele ya wananchi
 
Huna akili
 
Watanzania walivyo mafisi unadhani angeweza kudhibiti bila kufanyiwa figisu??? Na hapo usikute alitaka kudhibiti wamemfanyia hujuma hadi katolewa nafasi yake, nchi yetu ni kama imeshalaaniwa
 
Jamani si anaandika kama raia?
Nafikiri akisikilizwa atasaidia maboresho
Kwanza tatizo anafunguka kinafki.
Alipokua na cheo kwenye Wilaya hiyo hiyo hakufanya chochote, ametoka kwenye cheo ndio anaongea hapo tumueleweje kama sio alikua na ugomvi na mkurugenzi.
 
Kwani hakuna mamlaka za kushughulikia na kushughulika na hao?

Pesa zinakuja then hazitumiki harafu unasema watu wanakingiwa kifua,how and why? Hakuna ukweli Kwa hili.

Kuhusu miradi kutokamilika hii inawezekana Kwa sababu Halmashauri nyingi hazina Wataalamu Wala Vitendea kazi vya kutosha na hata pesa zinazokuja Huwa hazitoshi Kiasi kwamba inatakiwa Nguvu ya Wananchi ilinkukamilisha..

Hili ni tatizo sehemu nyingi ila Hali sio mbaya kama mtumbuliwa anavyoeleza.
 
Kutoka malamba mwisho kwenda king'azi ile barabara ni muhimu sana lakini sijui kama mbunge na diwani wanaifikiria,kwenye suala la maji safi na salama huko king'azi mpaka leo wananchi wanatumia maji ya tope,za chini ya kapeti zinadai huyo mtemvu ana canter za kuuza maji na ndio anatia ugumu wa maji ili yeye na macartel wenzake wa maji waendelee kuuza maji kwa raia,huduma ya afya wananchi ndio awaelewi kabisa!
 
Kwanza hicho mnachosema wizi sio kihivyo ila gharama za ujenzi ziko Juu,Vitendea kazi hakuna harafu pesa za Miradi zinakuja bila pesa za Usimamizi huu ni upuuzi wa Serikali.

Mie nimesimamia hii miradi najua,eti ujenge bweni la Watoto 180 Kwa mil.75 Kwa standards za kihandishi ,na Huwa wanaleta mil.150 mabweni mawili hii haiwezekani..

Kwenye mradi wa hivyo niliwahi dokoa 500k tuu lakini tulikamilisha bweni 1 na lingine likaishia kwenye boma..

Hapo hakuna pesa za Usimamizi na ni fixed kiasi kwamba makadirio ya serikali hayawezi maliza hizo miradi ni ndogo mno.eti darasa classic wanaweka mil.15 au 20 haitoshi maana darasa standard Kwa vipimo wanavyoleta si chini ya mil.25
 
Sio swala la mbunge Wala nini hapo ni serikali iongeze Bajeti Tarura.

Tarura Nchi nzima Wana mtandao wa Barabara zaidi ya km 180,000 na zinazaliwa Kila siku kadiri mijininavyokua harafu Bajeti yake ni Bil.800 tuu ikiwemo Mishahara na uendeshaji Sasa unategemea nini hapo?
 
Huyua akapatiwe ushauri nasaha, maana haamini Kama katumbuliwa.
Hata kama mnamchukia alichosema ndio ukweli..

Hii Nchi ukisimama kwenye mstari umeondoka,refer ya Omary Mgumba RC wa Tanga aliyetumbuliwa..

Nyie mnaolalamika Leo ndio hao hao ambao Huwa mnalaumu serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…