DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

Yuko sahihi kabisa. Kiitifaki inatakiwa kufika sehemu kabla ya bosi wako
 
Nategemea kusikia "Jerry piga kazi" na kapromosheni Fulani!!! Inastaajabisha sana! Sidhani kama mkurugenzi alichelewa kwasababu ya kunywa chain ni majukumu hayohayo! No kuvumiliana, no staha na ustaarabu ni vitukovituko tu working like machines!!!! Horrible experience!!!
 
Huyu yatamkuta yaliomkuta Kipindi akiwa Yanga. Hatacheleweshwa. MAANA huu NI ujinga tu
 
Nijuavyo DED kwa mafungu wapo vizuri zaidi,Mara nyingi DC, wanaomba hata mafuta.Awe na akiba ya maneno.
Ndiyo inavyokuwa... Huyo jeri ashukuru tu yalaiti mie ndiyo ningekuwa huyo DED afu ndiyo anategemea kwenye mafungu yangu nimwezeshe hakuna rangi ambayo angeacha kuona
 
Mkuu wa wilaya hayupo juu ya ded, wote ni wateile wa Rais kwa level ya wilaya.
 
That is not how we are supposed to serve.

Kama mwanachama mtiifu wa CCM ambayo inajukumu la kuisimamia Serikali.

Naomba mheshimiwa D.C. aonywe na mamlaka ya uteuzi.
Hata saa mbovu kuna muda inakuwa sahihi!
 
Mbona Gambo ametulia tu.. Au ndo kujishitukia kwamba anadharaulika
 

Ila na huyo mwenye PHd analo la kujifunza toka hapo, mtu umesoma na una malengo yako uwe msomi ulobobea uwe profesa, from no where unateuliwa tu kijingajinga na wewe unakubali,tena anaekuteua anajinasibu ni kichaa na wengi mnajua bado mnakubali kuteuliwa.Basi mkubali na kutukanwa na mabashite yake.Uprofesa sahauni.
Kwa taarifa ni kuwa waraka umepelekwa kwenye vyuo vyote vya umma kuwa mwanataaluma yoyote aliyeteuliwa na jiwe,akishindwa huko alikopelekwa basi asipokelewe pindi atakapoomba kurudi baada ya kutumbuliwa alikoteuliwa.
Kazi mnayo
 
Jerry amefanya makosa sawa,lakini PhD holder naye alikubalije kuwa DED?PhD holder unakuwa DED!? Haya yote yasingemkuta.
Teuzi za kisiasa waachiwe wanasiasa,wataalam tufanya kazi zetu za kitaaluma,hii
itatuepusha na maumivu kama haya.
 
Kama yule jamaa aliyetukanwa ni Phd holder basi naitilia mashaka Phd yake. Phd holder anashindwa hata ku counter diplomatically mpaka aliyekutukana ajione umemtoa nishai. Au Phd holder atashindwaje kujiuzulu baada ya matusi yale? Utamtizamaje mkeo au wattoto wako watawatuzamaje wenzao shule? Mara mkeo ukimgombeza anakwambia, " Hasira zako zote unazimalizia kwangu, lakini kwa bosi wako unakuwa kama mwari anayetaka kupoteza bikira!
 
Mfumo wa vichaa utajitenga na werevu. Sio wote ni vichaa kama jiwe anavyojiaminisha ingawa "vichaa vichaa hivi" ni wengi zaidi.
 
Kiongozi unatakiwa kujipambanua mapema kwa watu unaowaongoza ili wakujue misimamo yako, yuko sahihi jerry, ngoja awanyooshe watendaji wake waliokuwa wanafanya kazi kwa mazoea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…