DC Jokate Mwegelo atoa siku saba kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuunda Vikundi vya Ulinzi Shirikishi katika Mitaa yao

Tusije na sababu za kijinga tuwe serious na maslahi ya wananchi....Mbona haya mambo wakati wa magufuli hayakuwepo ina maana tulikuwaga ba police wa kutosha kipindi kile??Mama amelala sana alafu yupp busy kusafiri kila siku.....Kipindi cha magufuli mtu angeshawekwa benchi by now alafu nafasi inachukuliwa na mtu mwingine....Sasa hivi hii nchi inaongozwa na watu kibao na sio mtu mmoja....
 
Jeshi la Polisi lifumuliwe liundwe upya...!!
Mitaani vijana wanageuka panya-road!
Barabarani polisi wanageukapanya-road!
Yaani mwananchi anafanyiwa unyang'anyi mkubwa tena wazi wazi!
 
Baada ya Mshikemshike wa Chanika naona wamekuja na ulinzi shirikishi, Ila ntapata mashaka pale IGP aliposema nchi iko salama ilhali kule Chanika watu wanatembezewa mapanga na kuibiwa.
Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili... Wanawapeleka vijana shule wanawapa elimu nusu nusu...
Wanawapeleka JKT then wanawatelekeza mitaani...

Ifike mahali raia nao wajitetea kwa mbinu zao...
 
Ulinzi shirikishi (community watch) upo hata nchi zilizoendelea kama vile USA.
 
Very low IQ, hivi kipindi cha Dkt Magufuli hao vijeba walienda wapi??? Yaani hii nchi inaelekea kuwa ya wapiga dili. Hapo hao wenye makampuni binafsi ya ulinzi yanafadhili hivi vikundi vya waharifu ili wenye hela waombe kulindwa na hawa vijeba. Na huko tuendako tutegemee utekaji wa watu wenye hela utaibuka kwa kasi. Ni mjinga tu anayeweza kubeza juhudi za Dkt Magufuli. Na kibaya kabisa Mkuu wa wilaya unapoibuka na kuwatukuza wezi eti watu waunde vikundi. Najua hawajui ila hivyo vikundi vya ulinzi shirikishi mwisho wa siku vitakuja kuwa na silaha na mwisho vitakuja kupindua nchi.
 
... kupambana na panya road.
Panya road inasemekana kuwa eti ni watoto ! Lakini vyovyote vile iwavyo kama hao watoto wanaweza kubeba mapanga na kuwajeruhi watu Hao ni majambazi tu kama majambazi wengine !! Wanasemaga" Usipoziba UFA utajenga ukuta " Hao walioshikwa washughulikiwe vizuri ili waeleze kila kitu ! Hata mbuyu ulianza kama mchicha !! Mdharau mwiba mguu huota tende !! Tafakari chukua hatua !!
 
Msako wa siku moja tu police wakiamua panya road wote watafutika hapa Dar.
 
... uko sahihi 100%. Watoto (under 18) probably wanajua hawabanwi sana na sheria hata kama wakikutwa na makosa including mauwaji. Sana sana watakatiwa adhabu rahisi tu kwenye mahakama za watoto na kuachiwa. Unahitajika mkakati maalumu wa kumaliza kabisa tatizo hili linalotaka kuota mizizi.
 
... kwa hiyo nini kifanyike? Magufuli alishakufa na hawezi kurudi tena forever! Hana msaada wowote kwa sasa.
 
Jamani kwani huko hakuna community police officers, kuzunguka mitaani kuhakikisha wananchi wana obey the law?? Kama hakuna its time to invest on this....

Pia, temporarily wangetumia wanajeshi kutuliza hao panya Road, wanajeshi sio lazima vita kama ile ya Urusi ije ndio mkapigane, hata hii ni vita ya ndani mtulinde pia.... au hairuhusiwi kisheria?
 
No Wilaya ya Temeka ipeleke maombi ya polisi 50 CCP Moshi na wakae na Polisi kuangalia jinsi watakavyoweza kufanya kazi pamoja na ikiwezekana, Wilaya ikipunguza mahitaji wanaweza kuajiriwa na jeshi la polisi.
Tumieni askari wa manispaa ( mgambo), huu utaratibu unaopendekeza haufaii kwa mazingira yetu
 
Nchi yetu bado ni salama Sana hatujafika huko kutumia jeshi kupambana na vijana wadogo.
 
Kwhy kipindi cha Magufuri hakuna hakukuwa na uharifu.??

Hivi nyie watu watu vichwa vyenu huwa mnaviacha wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…