Dededege inamtesa sana mwanangu, wakuu nisaidieni dawa

Acha upuuzi. Mrudishe mtoto hospitali.
 
"Nilifanya CT-SCAN baada ya kushauriwa na watu" hapo ndio lilipo tatizo maana umeshauriwa na watu kwenda kufanya kipimo badala ya ma Dr na humu ndani pia tegemea kupata matongo pori ya Kila aina.
 
Pole sana mkuu.

Wangu alianza kusimama akiwa na miezi 13, baada ya hapo alipokomaa akawa anatembea kwa kukimbia(kwa asilimia kubwa) wako hajapitiliza sana.

Vuta subira, omba Mungu atatembea tu.
 
Usijali, umepata hii. Kesho nakupigia ili uipate hapo singida chap

Dawa za miti Asili ni zuri sana... Tatizo ukisasa ndo unazidi kutupoteza.... Na kusahau chimbuko letu la dawa asili.

Nakumbuka siku nilikatwa na panga mkononi, lile jeraha hawakunipeleka hospital, Nilitumia mti asili koshona kile kidonda.
 
Mpeleke akatibiwe kienyeji tatizo dogo Sana hilo
 
"Nilifanya CT-SCAN baada ya kushauriwa na watu" hapo ndio lilipo tatizo maana umeshauriwa na watu kwenda kufanya kipimo badala ya ma Dr na humu ndani pia tegemea kupata matongo pori ya Kila aina.
Kwani mkuu JF hamna matabibu wa kumshauri
 
Pole ndugu yangu.
Ngoja tuone wajuvi na wenye uzoefu na hili jambo wanasemaje.
 
Samahani mkuu, inawezekana wengine tulipitwa na huo uzi.

Kama haitachukua muda wako, kwa ufupi kabisa, kijana wetu ana shida gani?
1. Ilianza lini?
2. Maendeleo ya ukuaji wake yapoje?
3. Ulishawahi kufanya EEG?
4. Dawa gani anatumia?
 
Mm ninakuja mp kwko kukupa dawa ya asili yenye kutibu tatizo
 
Hili swala la kusimama jitahid ikitokea kasimama Kwa bahati mbaya au ukamsimamisha akasimam Kwa sec kadhaa/Dak inakubid umpitishie mwichi / mtwangio ktikati ya miguu yake kutoka nyuma! Njia ya pili inakupasa unyoe mavz yako hrf yakaange kwenye chungu yakisha ungua upate unga wake hrf unamchanja pande 4 za kiunoni yaaan mbele chini ya kitov,nyum,kulia na kushoto, hrf unammalizia na kwenye miguu usawa wa magoti kulia na kushoto Kila ukichanja unampaka hiyo kitu! Hii imesaidia wengi sana jaribu dawa unayo mwenyewe
 
Sawa mkuu
Poleni sana. Mimi nakushauri usichoke kuzunguka hospital. Kuna ugonjwa mwingine unaweza kuzunguka hospital hata nne kabla hujapata dr atakayetambua tatizo. Jingine uwe mwangalifu kwani binadamu siku hizi wamekuwa wanyama. Kuna mtu anaweza kuwa na ujasiri wa kutumia shida yako na akakupiga fedha nyingi kwa kisingizio cha kuwa anakupa dawa. Nakushauri usitoe fedha kwa hizi dawa za kienyeji kwani wengi ni matapeli. Mwenye nia nzuri atakusaidia kwanza mtoto akipona ndiyo utajua cha kufanya.
 
Aisee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…