Dededege inamtesa sana mwanangu, wakuu nisaidieni dawa

Samahani mkuu, inawezekana wengine tulipitwa na huo uzi.

Kama haitachukua muda wako, kwa ufupi kabisa, kijana wetu ana shida gani?
1. Ilianza lini?
2. Maendeleo ya ukuaji wake yapoje?
3. Ulishawahi kufanya EEG?
4. Dawa gani anatumia?
Shida ni degedege, anakuwa vizuri.. uzito unaongezeka.. muonekano mzuri, dawa anatumia kwa sasa sodium valproate na hio EEG sijui ni kipimo gani??
 
HUU NDIO USHAURI NILIOUBEBA, KWA WALE MLIONIPIGIA SIMU..TAFADHALI NAZINGATIA HILI..UBARIKIWE MKUU
 
Kuna dogo alizaliwa na hii kitu alifanyiwa dawa za kienyeji, alikuwa anapigwa vifagio mguuni. Ukimuona sasahivi huamini kama ndie yeye ila sijui dawa kaipata wapi. Tafuta njia hii kama utaipata
 
Eh... My God!!🤯🤯
 
Habari!
Pole na kuuguza.
Utaratibu wa kuuguza na kupata jibu kwenye tiba utategemea pia na njia utakayo izingatia.

Kwa ulinganifu wa historia fupi uliyoitoa ya tiba, bado kuna mapengo yasiyoelezeka.

Mfano:
1: Tiba ya mtoto huyu inahitaji kumhusisha daktari bingwa wa watoto pamoja na daktari bingwa wa mishipa ya fahamu.
Sina hakika kama hiki ndicho kilichofanyika.

2: Kwa msaada wa wazazi, historia ya mtoto inatakiwa ichukuliwe tangu mimba, jinsi alivyozaliwa, uchanga wake na ukuaji na mambo mengine muhimu yaliyojitokeza hapo kati.

Pia, ni nini hasa hutokea wakati wa degedege vs huambatana na nini?

Lengo ni kujaribu kujua tatizo lilianzia wapi na ni kiasi gani.

3: Kulingana na hatua ya historia, kumwangalia mtoto, vipimo vitaagizwa kulingana na yaliyong'amuliwa. Si kila degedege kipimo ni kimoja. Hii hutegemea na tatizo husika.

Mfano: mapendekezo hutegemea na aina ya degedege na chanzo. Kuna aina nyingi sana za vyanzo vya degedege vya muda mfupi na vya muda mrefu au kudumu. Kuanzia maumbile, urithi mpaka physiologia ya mwili.

4: Si kila dawa hufaa kwa kila degedege. Uchaguzi wa dawa hutegemea na aina ya degedege. Unaweza usifanikiwe na dawa hii au ile kutokana na uchaguzi wa aina ya dawa au kiasi cha dozi husika.

5: Kuna vitu pia utahitaji kutokumfanyia au kufanya ili kutokuwa chanzo cha degedege kutokea.

Hivyo, degedege si jambo la kuchukua kwa tiba ya mwelekeo mmoja. Ni suala pana, linahitaji ufuatiliaji wa karibu, uvumilivu, uelewa na uzingatifu.

Nakutakia matibabu mema.
Wape nafasi wataalamu husika hapo juu.
 
HUU NDIO USHAURI NILIOUBEBA, KWA WALE MLIONIPIGIA SIMU..TAFADHALI NAZINGATIA HILI..UBARIKIWE MKUU
Umefanya la maana, degedege inasabishwa na vitu vingi mno Kuna mdau hapo kakuuliza kama umeshawahi kufamnyisha EEG umemjibu hukujui hiko kipimo so hii inaonyesha dogo anahitaji vipimo vingi kujua chanzo Cha hilo tatizo ni nini endelea kuhudhuria hospitali hasa zenye ma Dr bingwa wa watoto Nina Imani dogo atapona tu.
 
Mshana Jr msahada wako juu ya hili swala tafadhali.
 
Shukrani mkuu
 
Shukran mkuu
 
Shu
Mshana Jr msahada wako juu ya hili swala tafadhali.
Ushauri wako mkuu Mshana Jr
 
Shida ni degedege, anakuwa vizuri.. uzito unaongezeka.. muonekano mzuri, dawa anatumia kwa sasa sodium valproate na hio EEG sijui ni kipimo gani??
kama mmefanya CT scan na haijaonyesha tatizo....

Binafsi nashauri ufanye EEG kama mdau alivyokuuliza hapo juu...I am confident enough EEG itakuwa na majibu yote...

Nina swali kwako...Je wakati wa kujifungua mtoto alilia ama alichelewa kulia?..

Ushauri wa mwisho usijisumbue kumpeleka kwa waganga wa jadi utapoteza pesa na muda wako..
 
Mmmh
 
MTOTO ALICHELEWA KULIA MKUU
 
Alichelewa kulia mkuu, ushauri wako mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…